Mtazamo wangu juu ya uundwaji wa baraza la mawaziri!

CBZ usipatazame sana hapo ulipoangukia, utaona damu yake inamemwagika uende hospitali ukatibiwe halafu tena kesho ujikwae.

Dili na wapi ulijikwaa, ili kama kuna kisiki ukiondoe ili kesho ukipita usijikwae tena.

Usiwe kama mfalme mmoja aneyeamini kuwa kuwa kugawa neti Malaria haitakubalika wakati kuna mazaria ya mbu yamejaa na hayafanyii kazi yoyote.
Je watu watembee barabarani wamejifunika neti??:A S-alert1:
 
hapa unamaanisha nini? sijakuelewa hata kidogo!
 

Hapo ulipomalizia na mimi nihighlight ndipo tulipojikwaa CBZ.
Hawa mafisadi wanapeana vyeo utadhani sisi tumezaliwa tuwatumikie wao milele na sisi watutawale melele
 
Naona tunakuwa wepesi saana wa kusahau. Kuna mbunge mmoja wa CHADEMa aliteuliwa kuwa kwenye ile tume ya madini, mpaka leo hii anaitwa msaliti na majina mengine. Kwakuwa nchi hii tumeamua kuwaachia CCM waitafune basi tukae kimya kabisa.
 
Hata mie namkumbuka alilianzisha Zogo la Buzwagi.
Ila nae kwa maoni yangu namuona yuko RIGID ila SIYO STABLE.
 


Asante sana ndugu yangu, kama ulivyosema huu ni mtazamo wako tu. Nami sioni vema kukulaumu kwa kuwa na mtazamo huu ingawa nina tofautiana na wewe kidogo tu, kwanza hilo suala la rais wa chama fulani kuteua waziri kutoka miongoni mwa wabunge wa vyama vya upinzani haliwezekani.

Nasema haliwezekani kwa sababu, wakati wa uchaguzi mkuu kila chama huingia kwa kunadi ilani yao ya uchaguzi ambayo itakuwa ndio muongozo au vipaumbele vya serikali yao watakayounda iwapo watachaguliwa katika uchaguzi husika.

Sasa inapotokea chama fulani kushinda ni lazima yule mshindi wa urais atateua mawaziri kutoka katika jopo la wabunge wa chama chalke ambao wapo tayari kuitekeleza ilani yao ya uchaguzi na pia kulinda maslahi ya chama chao. Hapa akiweka waziri kutoka chama pinzani inawezekana kutokea mgongano wa kisera ndio maana huwa hawafanyi hivyo.

Na hata kama wewe ndio mbunge toka chama pinzani ukateuliwa na rais kuwa waziri, je utakuwa na amani kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kingine hata kama ina mapungufu eti kisa tu ni ili rais awateue na wapinzani pia kwenye baraza la mawaziri.

Ujinga mwingine utakaotokea hapa, iwapo rais atateua mawaziri kutoka cahama cha upinzani, chama hicho kwa mtazamo wangu kitakuwa kimepoteza sifa ya kuitwa chama cha upinzani kwa sababu tayari kipo ndani ya mfumo wa utawala ikishirikiana na chama tawala.

Jambo la msingi, naona ni lazima tupate katiba mpya itakayoondoa tatizo hili ikiwa ni pamoja na kuzuia wabunge wasiwe mawaziri ila kazi yao iwe ni kuwawakilisha wananchi bungeni. Pia imtake rais kuteua mawaziri kulingana na wasifu wao kielimu na uzoefu kushika wizara zinazoendana na taaluma zao.Katiba mpya pia imvue rais madaraka ya kuteua wabunge kwa maana wabunge ni wawakilishi wa wananchi, sasa hawa wanaoteuliwa na rais wanawakilisha wananchi au serkali?

Nasisitiza kwamba tuahitaji katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Naona tunakuwa wepesi saana wa kusahau. Kuna mbunge mmoja wa CHADEMa aliteuliwa kuwa kwenye ile tume ya madini, mpaka leo hii anaitwa msaliti na majina mengine. Kwakuwa nchi hii tumeamua kuwaachia CCM waitafune basi tukae kimya kabisa.
Nimezungumzia 'uwaziri'...
 
Asante mkuu, nimekusoma!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…