Mtazamo wangu: Canadian Drinking Water vs Hill Drinking Water

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Dec 8, 2014
1,698
1,253
Habari wakuu.

Kwanza naomba kudeclare, hili sio tangazo la biashara.

Tuendelee, kwa sisi wakaazi wa mjini Dar es Salaam hasa wafanya biashara wa vinywaji baridi na watumiaji wa bidhaa hizo ni mashahidi kuwa kuna maji ya kunywa yanatamba sana mitaani (sokoni), kwa lugha ya kibiashara zaidi yanaitwa Hill.

Hill yamekuja kwa kasi sana na kukimbiza sana. Naomba kueleza yafuatayo kuhusu. Maji ya Hill kwa sasa yamekuwa kama bidhaa ya magendo. Hayapatikani kwa urahisi. Ukiweka oda unaletewa baada ya mwezi mmoja au zaidi. Imekuwa bidhaa adimu mno. Hii yote ni kwa sababu wazalishaji wamezidiwa uwezo na watumiaji.

Demand exceeds supply kiasi ambacho hata hawaelewi wafanyeje. Kuna tetesi kuwa ili uyapate maji yako basi ukatembeze bakshishi kwa "meneja" ndio uletewe cartons zako ulizo oda. Otherwise utasubiri sana. Na ukiletewa leo huletewi tena mpaka mwezi upite wakati ukishushiwa cartons elfu 1 leo zinaisha siku hiyo hiyo. Jamaa wanaringa sana.Imekuwa kero kuyauza maji yao.

Sisi wafanyabiashara wanatupa tabu sana. Wamemtoa kwenye reli Afya sasa wanatamba wao.

Sasa kuna kitu "kipya" kimsingi si maji mageni kwa jina la Canadian, nayo watu wanayaelewa sana. Demand inazidi kuongezeka. Nataka kuwaambia wazalishaji wa Canadian komaeni hapo hapo. Kazeni sana mtawatoa hawa jamaa kwenye reli na mkamate soko. Kisha msifanye kama wao mtapotea.

Soko la maji Tanzania ni kichefuchefu sometimes, waulizeni Afya, Maisha na Uhai ndio wanajua vizuri. Mwenzenu Masafi anajikongoja kibishi. Mtu akija nataka Hill, simple tu, Hill sina nna Masafi, haya niwekee katoni 40 na Uhai 5.

Nyie Hill endeleeni kuringa. Canadian njia nyeupe kutawala soko.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afya alikuja vyema ila kuna mahali alifeli, maana maji yake yameanza kuwa na ladha yenye kuchoma ulimi. Kuna mengine yanaitwa ice drop yako vizuri sana ila nayo hayapatikani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Canadian yanauzwa sana kwa Mwamposa et al, wajikite huko kwanza.... kuhusu Hill demand imezidi uzalishaji hivyo tunakamilisha mbinu tuanze ‘kuyafoji’ mtaani huku tupige hela.
 
Back
Top Bottom