MTAZAMO: Soka la Tanzania huchezwa na walioshindwa maisha na waliofeli masomo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
126,599
241,426
Baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nimebaini jambo hilo, kwamba wachezaji wengi wa soka wa nchini Tanzania wala hawakuwa na ndoto hiyo bali wengi wameingia huko kama Plan B. Na ni baada ya kushindwa maisha ama kufeli masomo.

Kwa mfano katika maeneo ambayo elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa watoto, Upanga, Masaki, Oysterbay au Mikocheni hakujawahi kuzalisha wanasoka.

Lengo la andiko hili si kuponda wanasoka wetu , bali ni kuanzisha mjadala wa kujua kisa cha kutothaminiwa kwa mpira wetu kiasi cha kuwafanya wazazi wakwepe kuwaingiza watoto wao.

Nini kifanyike ili soka iweze kuvutia kila mmoja na ionekane kama chanzo halali cha ajira ?
 
Mtoa hoja umechemka,usizungumze tu kwa story za vijiwen,lig kuu ya tanzania kuna wachezaj kibao wana jiwe la kwanza,na baadh nawafaham wamemaliza masters,mfano kipa wa toto /nadhan baadae alienda tim ya mbao,ana MA yule jamaa,ungezungumza kuhusu wale wa zaman angalau,ila sema nao fursa za shule ziliwabana maana zilikua chache au uduni wa maisha,ila baadae walivyopata cent wakapiga shule vizur tu,mfano leodeger Tenga,tatizo lenu vijana wa leo mkipata hivyo videgree vyenu mnahis nyie ndio wasomii
 
Mkuu huo ni ukweli mchungu sana umeusema. Wapo watakaokutukana lakini umesema kweli kabsa. Ndio maana hatusogei popote. Subiria mawe sasa.
 
Mtoa hoja umechemka,usizungumze tu kwa story za vijiwen,lig kuu ya tanzania kuna wachezaj kibao wana jiwe la kwanza,na baadh nawafaham wamemaliza masters,mfano kipa wa toto /nadhan baadae alienda tim ya mbao,ana MA yule jamaa,ungezungumza kuhusu wale wa zaman angalau,ila sema nao fursa za shule ziliwabana maana zilikua chache au uduni wa maisha,ila baadae walivyopata cent wakapiga shule vizur tu,mfano leodeger Tenga,tatizo lenu vijana wa leo mkipata hivyo videgree vyenu mnahis nyie ndio wasomii
Tena hiyo zamani unayoisema ndio kipindi pekee ambacho wanasoka wa Tanzania walikuwa wasomi , maana wengi waliibukia umiseta , kumbuka kwamba hivi sasa vipaji vinatokana na ndondo cup .
 
Hivi Pele, Maradona, Messi, CR7, Zidane, De Lima, Ronaldinho, Figo. Wanaelimu gani?
Wanaelimu za academ boraa kabisaa walizofundishwa toka utotoo..mamboo ya elimu hususan ya bongoo n nyokooo ..wakina boko hana elimu lkn msakuzi kule wameshajiwekezaa vya kutoshaa na maishaa yanaendeleaa ...maisha n ww jinsi utakavyoweza kupambana nayo ..
 
Tatizo kubwa ni kukosekana academia za michezo,vijana kufunzwa mapema kabisa,kuucheza mpira na kujengwa kiakili kuwa mchezaji mkubwa,hapa kwetu kocha wa timu ya Taifa eti anafundisha jinsi ya kupiga mpira,jinsi ya kutoa pasi...hivyo vyote vilipashwa kufundishwa kule utotoni kabisa kwenye academia...
 
Mpira ni wa uswazi sehemu zote duniani tena basi kuna vipaji vingi vimepotea kuliko hivi unavyovyishuhudia uswazi ngangari hakuna lelemama na ili uwe unakubalika basi football ndio ilikuwa kigezo. Mifumo mibaya pia inachangia klabu kama Barcelona wana la masia pale huwaangalia vijana katika nyanja nyingi sio mpira tu na stadi nyingine wakiona huna kipaji wanakutafutia elimu nyingine.
 
Soka ni mchezo wa watu masikini (kwa wachezaji) na ni wa watu matajiri (kwa mashabiki na wamiliki wa timu)

Hii ipo hata ulaya, chukulia mfano wa A.Sanchez.. Pia kuna matajiri waliolazimisha chukulia mfano Beckham.
 
Soccer ni mchezo wa watu masikini ambao ndio huwa wanaona ni njia pekee itakayo wasaidia kutoka kimaishaa maana kwao kupata elimu bora ni mtihani wengi huishia kufanya kazi zile za mwisho kama udereva, kufanya usafi, kulinda mifugo, kuuza maduka, kusafisha viatu.. Na matajir wao huwa wanafocus kuwaandalia mazingira mazuri ya badae watoto wao ndio maana huwapeleka shulee nzuri na badae kuja kuwa viongozi wakubwa wa serikali na makampuni makubwa... Ndio maana hata ukiona kina Pele, messi, Ronaldo, Ronaldinho.. N. K wakaamua kuwekeza nguvu zao kwenye na hata familia zao zilikua radhi kuwaachia maana zilijua shule haita wafikisha mbalii bora mungu amewajaalia vipaji na ametokea mtu wa kuviendeleza basi haina neno. Hata athletes wakubwa wote duniani hawana shulee angalia NBA na michezo mingine. Hivyoo michezo ni kimbilio la watu maskinii kama vile matajiri wanavyoshindana kwenye shulee
 
Soka ni mchezo wa Maumivu sio bongo tu,Angalia ata mastaa wa Dunia wa Soka,Mazoezi asubuhi, jioni,kuumizwa,kuvunjika,kutukanwa na mashabiki na kupigwa pia, Watoto wengi wa kishua hawana moyo huo wa kupambana wana alternative nyingi za maisha.
 
Asante kwa ushahidi .
 
Kwanza aliokwambia waliokulia Upanga na Mikocheni ndio wasomi nani? Tuliokulia na kusoma Dar ndio tunaujua ukweli, kuna watoto wa Masaki kibao wanakwenda shule alimradi tu.
 
Huku kwetu Tandika MwembeYanga mzazi anaweza kumuachisha mtoto shule ili akacheze mpira , je huko kwingine mzazi anaweza kukubali ujinga huo ?
 
Watu wanaangalia maslahi mkuu, hata mimi wa Mtoni Mtongani, siwezi kumwachisha mwanangu shule kwa ajili ya timu kama Mji-Njombe. Lakini kama timu na mkataba wa kueleweka hata mtoto wa Profesa anaweza kuacha shule.
 
Baada ya uchunguzi wangu wa muda mrefu nimebaini jambo hilo, kwamba wachezaji wengi wa soka wa nchini Tanzania wala hawakuwa na ndoto hiyo bali wengi wameingia huko kama Plan B. Na ni baada ya kushindwa maisha ama kufeli masomo.

Kwa mfano katika maeneo ambayo elimu ni kipaumbele cha kwanza kwa watoto, Upanga, Masaki, Oysterbay au Mikocheni hakujawahi kuzalisha wanasoka.

Lengo la andiko hili si kuponda wanasoka wetu , bali ni kuanzisha mjadala wa kujua kisa cha kutothaminiwa kwa mpira wetu kiasi cha kuwafanya wazazi wakwepe kuwaingiza watoto wao.

Nini kifanyike ili soka iweze kuvutia kila mmoja na ionekane kama chanzo halali cha ajira ?
Kwani mtu huitwa msomi akifikia ngazi ipi ya elimu? Tuanzie hapa kwanza.

Kama msomi ni mtu mwenye degree nakuendelea basi uko sahihi kulingana na mtazamo wako.

Kama msomi ni mtu yoyote aliye na ngazi ya elimu kuanzia elimu ya msingi basi umechemka vibaya.

Binafisi, najua kwamba mtu yoyote mwenye ngazi ya elimu kuanzia elimu ya msingi ni msomi. Hivyo siyo kweli unachozani.

Nirudi kwenye swali lako la msingi kuwa nini kifanyike. Yapo mengi ya kufanya ila binafisi kubwa nafikiri, elimu zaidi kuhusu umuhimu wa Michezo kama ajira zingine itolewe kwa Wazazi/walezi.

Hii itasaidia kutolewa muda wa kutosha zaidi kwa watoto kushiriki ktk mchezo wa mpira wa miguu kuliko ilivyo sasa. Swali kwako, umewahi kufikiria kukuza kipaji cha mtoto/mdogo wako na siyo kumsaidia kimasomo/kielimu pekee?

Hivyo swala hili lianze na Mimi, Wewe na yule ili mpira wa miguu uonekane kuwa ni ajira kama ajira zingine kwa wazazi na kwamba siyo kwa ajiri ya walioshindwa shule ya darasani/maisha.
 
Back
Top Bottom