Mtazamo: Sitashangaa kuona dola inapanda ghafla na shilingi kuporomoka wakati wowote kuanzia sasa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Baada ya barua inayodaiwa kuandikwa na BOT(ambayo mpaka sasa haijakanushwa wala kutolewa ufafanuzi na mamlaka husika) yenye kuonyesha kusudio la serikali kuchapisha note siku za baadae, ni wazi barua hiyo inaweza kupekelea shilingi yetu kushuka thamani dhidi ya dola na fedha zingine za kigeni wakati wowote kuanzi sasa.

Kwanini nadhania hivi?

Kwanza naomba niweke wazi kuwa mimi si mchumi na wala sio mtaalumu wa mambo ya fedha bali natumia tu commonsense kufikia conclusion hii.

Kwa mtazamo wangu, iwapo barua hii itaendelea kusambaa mitandaoni na kila mtu akabaki na tafsiri juu ya hiyo barua huku serikali ikikaa kimya, ni wazi watu wataamimi kuwa kweli serikali inakusudia kuchapisha notes na hivyo wananchi, hasa matajiri na wafanyabiashara, wataanza kuchukua hatua za kujihami.

Hatua ya kwanza na ya haraka ni kwa matajiri na wafanyabiashara hawa kubadili hela zao (hela za kitanzania) ili wapate fedha za kigeni ambazo ni stable (hard currency) hasa dollar.

Kitakachokwenda kutokea ni demand ya dollar kupanda na hivyo kuifanya thamani ya dollar kupanda dhidi ya shilingi yetu.

Pia, katika kujihami huko, watu wanaweza kuanza harakati za kuhamishia fedha zao nje ya nchi in terms of dollar, etc hata kwa njia haramu.

Ni mtazamo wangu pia hata kama serikali itakanusha ila watu bado watakuwa na wasiwasi kwani hata hiyo barua ukiiangali, ni vigumu kusema imefojiwa.

Kingine nachojiuliza ni nini itakuwa athari ya hali kwenye hii miradi mikubwa tunayoitekeleza kwa kutumia fedha za kigeni endapo kweli hali hii itajitokeza.

Mwisho.Maadam barua hii imevuja na watu wameanza kuitafsiri tofauti tofauti, ni vizuri serikali ikajitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi wa hili jambo mapema iwezekanavyo ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Wako wanaoweza kutafuta ufafanuzi kutoka BOT juu ya madai haya na kuna ambao hawatafanya hivyo kwasababu mbalimbali na badala yake wataamua kujihami tu wakisubiri muda uthibitishe ukweli ni upi.

Time will tell.
 
Idd Amini: "What is the major complaint of Ugandans about
my reign? "
Governor: "Your exellence, majority are complaining that there
is no money in circulation"
Idd Amini: "If Ugandans are complaining about money
scarcity, PRINT MORE!".
Governor: "As you wish".

Sent from my TECNO CA6 using Tapatalk
 
Ni lini shilingi ilipanda dhidi ya dollar kwa muda mrefu?
Ndoto labda wananchi watakapoachwa kusomeshwa no.Ukisomesha no watu unategemea nini.Check wenzetu uwasaidia watu wao ili wapande zaidi. Sisi tunawashusha ili waishi kama mashetani
Screenshot_2018-08-29-10-06-02.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baada ya barua inayodaiwa kuandikwa na BOT(ambayo mpaka sasa haijakanushwa na mamlaka husika) yenye kuonyesha kusudio la serikali kuchapisha note siku za baadae, ni wazi barua hiyo inaweza kupekelea shilingi yetu kushuka thamani dhidi ya dola na fedha zingine za kigeni wakati wowote kuanzi sasa.

Kwanini nadhania hivi?

Kwanza naomba niweke wazi kuwa mimi si mchumi na wala sio mtaalumu wa mambo ya fedha bali natumia tu commonsense kufikia conclusion hii.

Kwa mtazamo wangu, iwapo barua hii itaendelea kusambaa mitandaoni huku serikali ikikaa kimya, ni wazi watu wataamimi kuwa kweli serikali inakusudia kuchapisha notes na hivyo wananchi, hasa matajiri na wafanyabiashara, wataanza kuchukua hatua za kujihami.

Hatua ya kwanza na ya haraka ni kwa matajiri na wafanyabiashara hawa kubadili hela zao (hela za kitanzania) ili wapate fedha za kigeni ambazo ni stable (hard currency) hasa dollar.

Kitakachokwenda kutokea ni demand ya dollar kupanda na hivyo kuifanya thamani ya dollar kupanda dhidi ya shilingi yetu.

Pia, katika kujihami huko, watu wanaweza kuanza harakati za kuhamishia fedha zao nje ya nchi in terms of dollar, etc hata kwa njia haramu.

Ni mtazamo wangu pia hata kama serikalo itakanusha ila watu bado watakuwa na wasiwasi kwani hata hiyo barua ukiiangali, ni vigumu kusema imefojiwa.

Kingine nachojiuliza ni nini itakuwa athari ya hali kwenye hii miradi mikubwa tunayoitekeleza kwa kutumia fedha za kigeni endapo kweli hali hii itajitokeza.

Time will tell.
Ingawa umesema ukweli tegemea mvua ya matusi kutoka kwa wana wa lumumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom