mchemsho
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 3,212
- 867
Taarifa ya Mh. Zitto kutangaza kukusanya saini za wabunge 70 ili kupata uhalali wa kuitisha kura ya maoni ya kutokuwa na imani na waziri mkuu iwapo mawaziri wanaolalamikiwa hawatajitathmini na kujiona kama bado wanastahili kuendelea kuwa mawaziri. Binafsi inanikumbusha malumbano ya mwaka jana kati ya Zitto na Mkullo, ambapo zitto alitoa taarifa bungeni kwamba serikali imefilisika na haina fedha hata za kulipa mishahara.! Kwa upande wake waziri mkullo alimjia juu zitto na kumnanga eti anajitafutia umaarufu, malumbano yaliendelea ndani na nje ya bunge, mwisho wa siku ukweli ulijitenga , kweli serikali imeishiwa na madeni yanaongezeka. Lakini pia hapo jana bungeni zitto alimtuhumu mkullo kwamba ndie waziri anaengoza kwa safari za nje na ndio wizara inayoongoza kwa madudu. Kwa maoni yangu naona zitto ameitega serikali ili mkullo aondoke na yeye asimame kifua mbele. Nawasilisha.