Mwabhleja
JF-Expert Member
- Jan 27, 2016
- 1,351
- 2,061
Salam Ndugu,
Awali ya yote napenda niweke wazi kwamba mimi si mtumiaji wa madawa ya kulewa ya aina yoyote ile ya kilevi. Vile vile sijawahi kuvuta sigara wala kuwa mrahibu wa chochote. Pia siyo mtaalamu wa masuala ya madawa wala sina uzoefu wa kina kuhusiana na madawa ya kulevya isipokuwa nimekuwa mfuatiliaji wa habari, tafiti na sheria mbalimbali zinazohusiana na masuala ya madawa.
Pamoja na hayo, pia nimekuwa nikiutumia muda wangu wa ziada kujisomea hususani masuala ya ubinadamu na demokrasia ya kijamii. Nimepata kufahamu kuhusu mambo muhimu matatu:
1. Utajiri mkubwa walionao wafanya biashara wa madawa ya kulevya unatokana na kanuni kubwa mbili za kiuchumi (Supply & Demand) kwa kuwa uhitaji wa madawa umekuwa mkubwa kuliko usambazaji wake hivyo bidhaa hiyo inauzwa kwa bei gari.
2. Warahibu wengi wa madawa ya kulevya waliopoteza mwelekeo kimaisha ni kwasababu walitumia dozi kubwa kuliko inavyostahili sawa na ambavyo mtu yeyote anaweza kuzidisha dozi ya Kwinini na baadaye akapata madhara.
3. Sheria kali na uwekezaji mkubwa katika kupambana na biashara/matumizi ya madawa ya kulevya bado haijawa suluhu ya kukomesha usugu wa tatizo
MAPUNGUFU KATIKA HOJA ZA WAPINGA BIASHARA NA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA
a) Kumekuwa na hoja kwamba madawa ya kulevya ni hatari kwa afya ya binadamu
-Inawezekana ni kweli, lakini vile sigara zilizohalalishwa, pombe na aina mbalimbali za vyakula ni hatari kwa afya ya binadamu pindi mtumiaji anapozidisha. Je, endapo kungekuwa na kipimo au dozi halali isingesaidia kupunguza athari za kiafya kwa watumiaji?
b) Kumekuwa na hoja kwamba watumiaji wanaweza kusababisha ajari barabarani au kazini.
-Ni kweli, lakini vile vile mtu aliyegombana na mkewe nyumbani na kuendesha akiwa amepanic anaweza kusababisha ajali. Mtu ambaye hajafuzu vema katika fani ya udereva anaweza kusababisha ajali, mtu aliyekunywa pombe halali vile vile anaweza kusababisha ajali sawa na mtu mwenye mawazo ya kukosa ajira anayetanga tanga barabarani Kwanini basi hoja ya ajali iwe na mashiko kwa madawa ya kulevya tu?
c) Madawa ya kulevya yana urahibu (addicts)
- Ni kweli, lakini vile vile sigara, pombe, kahawa, bao, utazamaji wa video za ngono na mitandao ya kijamii huchangia pakubwa katika kuathiri maendeleo ya watu binafsi na taifa kwa ujumla basi ni kwanini urahibu katika maeneo hayo haujahalamishwa?
d) Kumekuwa na hoja kwamba wahusika ni wahalifu na wanajihami kwa silaha
- Inawezekana, lakini hii haitokani na kuhalamisha matumizi pamoja na biashara hiyo. Huenda ingekuwa halali kusingekuwa na kujihami kama ambavyo wavuta sigara hawajihami.
e) Watumiaji huathiri akili zao na huweza kujinyonga ama kudhuru afya zao
- Inawezekana, lakini vile vile kuna idadi kubwa ya watu wanaojidhuru ama kujinyonga kwa ajili ya mapenzi, siasa, michezo ama dini hivyo sababu hii ni dhaifu.
f) Sheria kali ndiyo njia pekee ya kutatua tatizo la urahibu na biashara za dawa za kulevya
-Inawezekana, je hakuna uwezekano kwamba suala hilo ni la mtu binafsi, malezi na muhusiano ya kijamii? Mbona sigara zimehalalishwa na zimeandikwa ni hatari kwa afya ya binadamu lakini si wote tunaovuta na kukubaliana na madhara?
-Kwanini serikali ikose mapato ya cocaine wakati huo huo inakubaliana na mapato ya sigara na pombe zinazodhuru afya za raia kama ilivyo kwa dawa nyingine?
IKUMBUKWE:
Si lengo la uzi huu kuchochea matumizi wala biashara ya madawa ya kulevya bali ni mwanzo wa fikra mpya kuhusiana na namna bora ya kukabiliana na changamoto za kijamii pasipo kusababisha janga jingine. Karibuni