Mtazamo: baadhi ya tabia za wanawake wa kileo zinazofanya ndoa au mahusiano yasidumu

iMad

JF-Expert Member
Aug 4, 2013
1,833
742
1.ubishi na ujuaji
Siku hizi ni jambo la kawaida kukuta msichana ni mbishi (argumentative) na mjuaji, anabisha na kuweka ujuaji sana (wakati mwingine hata mbele ya watu) huku kukiwa hana nia yoyote ya kusaidia au kuleta suluhu bali kujionesha anajua kuliko mme au mchumba wake.
Hii tabia ya ubishi na ujuaji wanawake wengine wanaihalalisha, mpaka wakati mwingine wanajiita strong women au strong black women lakini mara nyingi unakuta ni kwenye kuharibu na kujionesha.

2.kuendeleza maisha yale yale(ujana) wakati mtu yupo kwenye comitment either ya ndoa au uchumba(serious).
Hii wakati mwingine inajionesha kwenye kukataa kubadilisha life style mfano kwenye mavazi, kupost na kutumiana picha za ajabu kwenye mitandao(facebook, instagram, whatssup, badoo nk na unakuta mtu ana yote hiyo), lakini pia kuendelea kuhangaika na marafiki sana na kupoteza muda na focus ya kujenga maisha ya ndoa au uchumba na mara nyingi mkikatazana mtu hulalamika kuingilia uhuru, bila kujua mkishakuwa wawili mmekubaliana ni lazima kusucrifice, ikiwepo na uhuru kidogo pia.

3.kulaumu na kulinganisha
Hii maranyingi hutokea mwanamke anamlinganisha mme au mchumba na watu wengine, bila ya yeye kuweka input yoyote au kuweka chochote mezani kusaidia hali iliyopo labda inasababishwa na wanawake wengi wasiojitambua kuambiana wao wanatakiwa watafute wanaume wenye hela tu kwa hiyo hawaangali potential, nachomaanisha hapa kushidwa kuangalia potential ni mfano kipindi obama alikutana na michelle, mitchelle alikuwa juu, alikuwa preceptor wa obama, lakini michelle aliona potential akastic nae tunaona walipoishia.
Lakini wakati mwingine inaweza kusababishwa na immaturity au kushidwa kujitambua(kuigana) au kutoka background za kimaskini.

4.Mambo ya kuiga
Hili kwa mtazamo wangu naona linasababishwa hasa na kule kushidwa kujitambua, kujua(define) mtu anayotoka, uvivu wa kufikiri na kukosa goals(malengo) kwenye maisha. Kwa mfano unaweza kuta mtu anahadithiwa tu na rafiki yake ofsini kwamba mume wake au mchumba wake anamfunga viatu basi nae akirudi nyumbani anadai kufungwa viatu bila kujali mazingira na aina ya mtu aliyenae
Tunaona hata hapa MMU BAADHI ya wasichana wanavyopelekana, mtu flani akipost kitu hata kama ni cha ajabu watu wanaunga mkono, mtu akimtukana mtu nao wanakandamizia juu, mtu akitangaza mchumba na wote wanataka kutangaza nk

5.kushidwa kujithamini na kujitunza
Mimi nimeonana na wanawake
wengi(kwenye kazi yangu) ambao wako 28 -35 yrs wanatamani sana warudi miaka 21 wafanye uchaguzi upya kuhusu namna ya kuthamini na kuitunza miili yao, kungonoka ni tamu na kila mtu anafanya, lakini wasichana wengi wanajitoa ufahamu kwa sababu wanampa kila mtu, ni kama unasema mtu kajikataa, unakuta mtu kila mwezi anatibiwa UTI na PID, na pia kuna wasichana wengi hawajui kati ya vitu vinavyosababisha ugumba ni ABORTION mimi nimeshuhudia hospital za manispa hapo DSM wasichana wa chuo wanavyofanya abortion lakini ndoa isipojibu anamsingizia Mungu wakati kuna abortion, au mtu alishapata chronic PID au STI kama gonorhoea ambayo husababisha ugumba
NB: wakina dada ambao mnapata fursa ya kuingia sehemu kama jf mjaribu kulearn something na kuelimisha wengine nje ya hapa..comment kupinga, kucheka, kubeza,lakini kwa kujenga au sio..?
 
Mda wote yuko na sim mkononi anapapasa,kila mtandao wa kijamii yupo na picha za udaku ameweka.Sim yake iko bize mda wote kama Dalali wa nyumba,vyumba,frem na viwanja.
Ni kweli mkuu Dr. unakuta mtu yupo kwenye mitandao yote na kote anawakilisha kote kaweka mapicha na maisha yake kayaanika kote
 
wote huo ni utoto, puberty at adult age,

most of women wakishafika 30's huwa wanajitambua,

hizo quarrels zinaisha kabisa...
Hivi mkuu unajua kwa mwanamke miaka 30 ni mingi sana..? Hata kibailojia pia anakua kashafika mbali kidogo
 
Hivi mkuu unajua kwa mwanamke miaka 30 ni mingi sana..? Hata kibailojia pia anakua kashafika mbali kidogo

ni kweli mkuu,

ila jaribu kufuatilia, ukosefu wa majukum na kichwa kuwa chepesi kutokana na kuwa na mambo machache ndio hupelekea mwanamke kuwa msumbufu na kuwa na viburi visivyo na msingi..

kawaida wanawake wa umri 18 mpaka 25 huwa bado wako katika kizazi cha smartphone, bado hawajaingiwa na majukum mazito both internal and external...

Jaribu kufuatilia wanawake wa 30+ utaniambia..
 
wote huo ni utoto, puberty at adult age,

most of women wakishafika 30's huwa wanajitambua,

hizo quarrels zinaisha kabisa...

Mara 100,000,000,000,000 uoe mwanamke mdhungu, kuliko kuoa mwanamke mweusi mwenye kuiga ya wadhungu.
 
Mara 100,000,000,000,000 uoe mwanamke mdhungu, kuliko kuoa mwanamke mweusi mwenye kuiga ya wadhungu.

Hivi ulikua wapi zinc?ukiiga lazima ukosee sawa tu na ukijamba kwa hasira....litakutoka ....!!
Umenena mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hivi ulikua wapi zinc?ukiiga lazima ukosee sawa tu na ukijamba kwa hasira....litakutoka ....!!
Umenena mkuu

Kiongozi mwekundu, mi nipo. Wanawake black america ambao ni weusi wananyea debe, wameleta matabaka kwenye familia.
No woman No cry by Bob marley
 
Last edited by a moderator:
ni kweli mkuu,

ila jaribu kufuatilia, ukosefu wa majukum na kichwa kuwa chepesi kutokana na kuwa na mambo machache ndio hupelekea mwanamke kuwa msumbufu na kuwa na viburi visivyo na msingi..

kawaida wanawake wa umri 18 mpaka 25 huwa bado wako katika kizazi cha smartphone, bado hawajaingiwa na majukum mazito both internal and external...

Jaribu kufuatilia wanawake wa 30+ utaniambia..
Ni kweli kabisa..nmekupata ile maturity na kujitambua wakati mwingine inaendana na age na mzingira(hasa majukumu)..
 
Mda wote yuko na sim mkononi anapapasa,kila mtandao wa kijamii yupo na picha za udaku ameweka.Sim yake iko bize mda wote kama Dalali wa nyumba,vyumba,frem na viwanja.

Lol! huyo msichana/ mwanafunzi ambae hana kazi,,,,,,,,,, wengine mda wa jf tunapata tabu
 
Ni utoto tu, tukikua tutaacha ingawa inaweza kua ndo too late tayari. Ladies, we have to grow up and behave more maturely

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom