Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Mtatiro: UKAWA imeinyanyua CUF

Ngaliba Dume

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,710
Reaction score
3,685
UKAWA IMELETA MAPINDUZI MAKUBWA SANA YA SIASA HAPA TANZANIA.

Hongereni sana Ubungo. Mimi sitakwenda Bungeni lakini mtu kama Kubenea anakwenda. Ni jambo kuu sana kwangu.

Kule Kinondoni CUF tuna kijana wetu mzuri anaitwa Mtulia Maulid, nikitoka ngome nakwenda kumuunga mkono kwenye majumuisho. CUF inaleta kijana machachari sana kutoka hapa Kinondoni.

Pale Temeke yupo Mtolea wa CUF huyu naye hadi sasa anaongoza. Kule Mbagala yupo Kondo Bungo wa CUF naye anaongoza. Ni faraja kubwa sana kwangu, vijana hawa wote wakawashe moto bungeni. Sisi tutawasaidia sana tukiwa nje ya bunge na huwenda ufanisi wao bungeni ukatokana na ushauri wetu huku nje.

CUF pia imetuletea SAKAYA, huyu ni samaki na huwezi kumfundisha kuogelea, kule kusini tayari tuna Kuchauka wa Newala, tuna Katani wa Tandahimba, tuna Bobali wa Mchinga, tuna ----- Bungala wa Kilwa kusini, tuna Musa wa Tanga Mjini n.k.

Bado vijana kadhaa wa CUF pia wanaelekea kushinda kwenye majimbo mengine.

Siyo hivyo tu, CUF pia imepata na itaongoza halmashauri kadhaa ikiwemo Tanga Mjini, Newala, Tandahimba, Kilwa n.k. Haya ni maeneo ambayo tumepata madiwani wengi.

HAYA NI MAFANIKIO MAKUBWA SANA KWA CUF..

Tokea chama chetu kilianzishwa hakikuwahi kupata zaidi ya wabunge wawili Tanzani Bara na hakikuwahi kuwa na halmashauri hata moja.

Ndiyo maana mimi ni mtu nayeamini sana katika ushirikiano. Leo CUF inapata wabunge wengi bara, inaelekea kuongoza halmashauri kadhaa...Hii ndiyo faida ya kujitosa kwenye ushirikiano.

Tulipokuwa tunaanzisha UKAWA kuna watu walisema CUF itamezwa. Mimi nimeendelea kushikilia msimamo kuwa CUF haiwezi kumezwa kwani hivi sasa ina wabunge wengi zaidi kuliko ilivyowahi kutokea. Chama chochote kinakuwa VIBRANT na kukua kinapopata wawakilishi wengi zaidi. Huu ni mwanzo mzuri sana kwa CUF na UKAWA yenyewe.

UKAWA inapaswa kushughulikia changamoto zake zilizosababisha kukosa baadhi ya majimbo muhimu na kujiwekea utaratibu bora kwa uchaguzi ujao.

Mtatiro J,
Segerea.
 
vipi jimbo la utete mbona hawatangazi mpaka sasa, wakati viti vya udiwani karibia vyote wameshinda CUF?
 
Mwaka 2005 ilikuwaje??

Compare and contrast
 
siku zinavyosogea mbele mamluki waliochangia ndoto zetu za kuunganisha upinzani zinafeli watajipambanua na tutaikomboa Tanzania toka kwa mkoloni mweusi ccm. peooopleeeesss
 
Ngaliba Dume

Huu ndo ukweli kuwa CUF imepata faida kubwa. Pole sana Mtatiro kukosa Ubunge lakini ni kweli kuwa unaweza kufanya kazi nzuri zaidi kuijenga CUF hata ukiwa nje ya Bunge.
 
Last edited by a moderator:
Kazi iliyopo ni kuanza kujipanga na kujiimarisha mapema sana,viongozi wa vyama waandae strategies za kujenga vyama imara na kuhakikisha kwamba we formally aggragate our parties into strong coalition. Nadhan wabunge wa UKAWA waliolazimisha kugombea jimbo moja wamejifunza jambo...
 
Huyu ni mkomavu sana kisiasa, hata kushindwa kwake ni matokeo ya kutosahihisha kosa la UKAWA kuwa na wagombea wawili jimbo moja. Leo hii tungekuwa tunaongelea ushindi wake. CCM wamepeta kupitia mvutano na utengano. Bado hana kinyongo katoa kauli positive. Viva Mtatiro and others like you!! Tunahitaji watanzania wa aina yako wengi zaidi.
 
Mtatiro ni hazina ya viongozi wachache sana taifa hili linapaswa kujivunia kabisa
 
Hongera kwa ukomavu na upeo mkubwa wa kisiasa. Kwa maumivu uliyopata mtumwingine asingeweza kutiririka hivyo hadi apate ushauri nasaha.
 
Mtatiro ww ni kiongozi wa mfano, wakati wa shida kuu viongozi wakweli wanaonekana
 
Mtatiro ni hazina kwa taifa letu..ni zaidi ya mwanasiasa!!
 
Mtatiro alikuwa anashinda kirahisi segerea msaliti mmoja wa chadema akarusisha fomu kinyemela akamharibia
 
hongera Mtatiro kwa ukomavu wa kisiasa. Bado nakumbuka heshima yako pale UDSM!
 
Back
Top Bottom