Mtatiro(CUF), Nape(CCM) na Erasto Tumbo(CDM) "LIVE" on MLIMANI TV Leo saa 2 usiku

Cuf & ccm bora ungeandika ccm &ccm-b maana ni wamoja na hata wakijifanya wanapingana ni unafiki tu wa siasa....sisi tunajua ni wamoja na pale angekuwepo mwakilishi wao mmoja tu.........
 
Unachokosea ni kwamba wote ni watendaji katika vyama vyao, naibu katibu mkuu ni mtendaji na makatibu wa itikadi ni watendaji kwa hiyo mtatiro(Naibu katibu mkuu) na nape - katibu wa uenezi hawana tofauti kubwa sana, ambacho ni muhimu kukitizama ni kuwa wote bi vijana wenye uwezo mkubwa wa kujenga hoja na wana uwezo wa kushawishi mambo fulani.

wewe ndiye unakosea, ama unachanganya mambo.

mimi ninafahamu kwamba wote ni watendaji, lakini kaimu katibuy mkuu na katibu wa itikadi na uenezi ni nafasi mbili tofauti, zingatia hilo!!

suala la kwamba wao ni vijana liko wazi na halihitaji debate.

swali la msingi ni kwa nini kila tukio cuf wanampeleka mtatiro??
 
Kwa CUF kitengo hicho kinaitwa KURUGENZI YA HABARI,UENEZI NA HAKI ZA BINADAMU, inaongozwa na Mhe. Amina Mwidau(MB) - Viti maalum kutoka mkoa wa Tanga(M.A in Mass Communication). Kwa sasa yuko bungeni na kipindi kiko Dar kwa hiyo inahitaji upeleke mtu mwingine, na kwa sababu Nape ni mtu wa propaganda kali inahitaji apambane na watu wenye uelewa mkubwa thats why tumempeleka Mtatiro kwa kuamini uwezo wake.

Lakini katika programu mbalimbali za TV na REDIO tumekuwa tukiwapeleka watu tofauti, siku kadhaa zilizopita katika mjadawa wa asubuhi TBC alikwenda AMINA MWIDAU mwenyewe na mara nyingi sana tunawapeleka watu tofauti, Mtatiro ni mmoja wao tu na hatuna Ubaguzi.

Kwa sasa ASHURA Mustapha yuko busy na umaliziaji wa dissertation yake ya M.A na akikamilisha najua mtamuona akitumika kwa shughuli kama hizi.

Nadhani nimekujibu vizuri.

Nimekupata vizuri mkuu,

Ila ashura mustafa alikuwa anawafaa sana, huyu mbunge simuoni kama ana uwezo mkubwa wa kukabiliana na propaganda hata kama ni msomi mzuri kiasi hicho.
 
UDSM unayoiongelea ni ipi? kila mtu alikuwa UDSM bradha.

UDSM hiyo uliyo kuwa wewe mimi sijawahi kuwa hapo, nimemfahamu mwita kupitia Daudi Deo. Siwezi kumuita kichwa hata mkimuweka kwenye wodi mirembe.
 
Wewe ongelea hizo vyeo vyenu vya CUF, vya UDSM usiongee kwa kuwa nilikuwa behind kumpa vyeo vyote hivyo, aliletwa ofisini kwangu na Daud Deo nimsaidie nikafanya hivyo kwa kuwapa fund na back up ya watu wangu wote wa UDSM, hakuwahi kushinda na anaogopa uchaguzi. Kwa vyeo vya CUF kama mwenyeketi ni Lipumba sishangai hata mkiokota mwehu akawa katibu mkuu.
Kaka tusaidie Daud Deo yuko wapi maana nilihisi na yeye ni jembe?!!, vp kapotelea wapi?
 
UDSM hiyo uliyo kuwa wewe mimi sijawahi kuwa hapo, nimemfahamu mwita kupitia Daudi Deo. Siwezi kumuita kichwa hata mkimuweka kwenye wodi mirembe.
Kwa hiyo wewe unahusika na kuweka viongozi wehu kwenye nafasi mbalimbali eeh!!
 
Kumbe bajeti inajadiliwa na kamat ya chama?????hata nape kaijadili na kuirekebishaaaaaa?????bajet ni ya sisiemuuuuuu
 
Nape anazungumzia performance ya bunge kwamba upinzani umepinga kila kitu hata waliyopendekeza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom