Mtatiro amvaa Mkurugenzi TAKUKURU

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na na siyo kumtishia mbunge huyo.

Mtatiro%2012.jpg

Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza sana Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa series ya matukio hayo yanayohusisha rushwa.

Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.

"TAKUKURU siyo mahakama na kwa kweli haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro

Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?

Pamoja na hayo Mtatiro amesema kutokana na kauli za Mkurugenzi wa TAKUKURU haitabaki salama kwa kauli na mienendo ya namna hiyo ikiendelea kutolewa.
 
Huyo boss wa Takukuru anadhani watu watakaa kimya bila kumshinikiza, ni nani asiyejua vyombo vingi vya nchi hii vinavyofanya kazi kwa kujivuta? Cdm walitangaza miezi kadhaa nyuma kwamba hao madiwani wameondoka kwa kupewa rushwa, ni hatua gani walichukua mpaka sasa. Sawa tuchukulie ndio utendaji wao wa kizembe, sasa ushahidi umeletwa ni hatua gani mpaka sasa wanechukua? Sanasana ni vitisho visivyo na maana. Hao Takukuru kazi imebaki kuchunguza watu wenye kutofautiana na watawala.
 
Kama hakuelewa maelezo ya Mkurugenzi wa takukuru basi huyu Mtatiro naye ni mburura. Kwanza aende akamalizane na Professor Lipumba.
 
Tuliambiwa hao Taasisi ya Kutetea na Kuikuza Rushwa inawachunguza wale wote waliopokea rushwa ya pesa za wizi za Escrow, lakini siku zinazidi kuyoyoma tu hatusikii lolote lile kuhusiana na uchunguzi huo. Sijui hata wanachunguza nini wakati ushahidi uko wazi kabisa kwamba akina Chenge, Tibaijuka, Ngeleja, Gurumo walipokea mabilioni ya pesa za wizi.

Halafu dikteta uchwara, mwizi na muongo utasikia anajigamba kwamba anapambana na ufisadi na ubadhirifu kumbe ni UONGO MTUPU!
 
Huyo boss wa Takukuru anadhani watu watakaa kimya bila kumshinikiza, ni nani asiyejua vyombo vingi vya nchi hii vinavyofanya kazi kwa kujivuta? Cdm walitangaza miezi kadhaa nyuma kwamba hao madiwani wameondoka kwa kupewa rushwa, ni hatua gani walichukua mpaka sasa. Sawa tuchukulie ndio utendaji wao wa kizembe, sasa ushahidi umeletwa ni hatua gani mpaka sasa wanechukua? Sanasana ni vitisho visivyo na maana. Hao Takukuru kazi imebaki kuchunguza watu wenye kutofautiana na watawala.
Exactly
 
Hivi Mtatiro alishaenda ofisn kwake Buguruni?
Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na na siyo kumtishia mbunge huyo.

Mtatiro%2012.jpg

Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza sana Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa series ya matukio hayo yanayohusisha rushwa.

Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.

"TAKUKURU siyo mahakama na kwa kweli haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro

Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?

Pamoja na hayo Mtatiro amesema kutokana na kauli za Mkurugenzi wa TAKUKURU haitabaki salama kwa kauli na mienendo ya namna hiyo ikiendelea kutolewa.
 
Kumbe kamvaa kupitia facebook.
Kichwa cha MTATIRO HAKIWEZI KUELEWA MAELEZO YA TAKUKURU
 
Mtatiro anakurupuka TAKUKURU haifanyi kazi kwa mitulinga.
Kama TAKUKURU ingekua inafanya kazi kama Mtatiro na bendera fuata upepo wa chadema wanavyotaka,basi mfalme Mbowe angekua matatani saa hizi kwa kuuza chama kwa Lowassa kwa bilioni tano
 
Pengine siku za huyo kamishna wa TAKUKURU zinahesabika maana hawa jamaa wa TAKUKURU ndiyo vinara wa kula rushwa hapa nchini.
Na isitoshe kwa nini Kaimu wake ana cheo kikubwa kuliko yeye KIJESHI?Asome nyakati aache kukurupuka takukuru mnalipwa MISHAHARA NA POSHO KWA KODI ZETU HICHO KIBURI CHA NINI?
 
Mtatiro anakurupuka TAKUKURU haifanyi kazi kwa mitulinga.
Kama TAKUKURU ingekua inafanya kazi kama Mtatiro na bendera fuata upepo wa chadema wanavyotaka,basi mfalme Mbowe angekua matatani saa hizi kwa kuuza chama kwa Lowassa kwa bilioni tano
hamuwezi kumaliza siku bila kumtaja Lowasa, inaonyesha huko hakupo salama kama Lowasa yupo nje ya chama chenu.
 
Baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kutoa onyo kwa Mbunge Nassari kuhusu ushahidi anaoutoa kuhusu wateule wa Rais kuwanunua madiwani Arusha, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, (CUF) Julius Mtatiro ameitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na na siyo kumtishia mbunge huyo.

Mtatiro%2012.jpg

Mtatiro ametumia ukurasa wake wa Facebook, kwa kusema kwamba alitegemea TAKUKURU ingempongeza sana Nassari kwa kazi aliyofanya lakini kinyume chake wanamtisha na kumshtaki kwa kauli yake aliyoitoa jana kuwa ataendelea kutoa series ya matukio hayo yanayohusisha rushwa.

Mtatiro ameendelea kusema kwamba TAKUKURU ni chombo cha wananchi, siyo watawala na Nassari ni kiongozi na ni mwananchi, ana haki zote za kuikosoa na kuishinikiza taasisi ya kiuchunguzi ichukue hatua stahiki.

"TAKUKURU siyo mahakama na kwa kweli haina kinga dhidi ya "kulaumiwa na kushinikizwa na umma". TAKUKURU ijibu mashinikizo haya kwa kuchukua hatua, aidha kuwafikisha mahakamani wale watoa rushwa au kuwasafisha. Na iache kumtisha Nassari" ameandika Mtatiro

Aidha Mtatiro amehoji kwamba "Kwani Nassari akiendelea kutoa hizo video za ziada anafanya kosa gani kisheria. Kama ni kosa kwa nini wale watuhumiwa (watoa rushwa na wapokeaji) hawajampeleka mahakamani"?

Pamoja na hayo Mtatiro amesema kutokana na kauli za Mkurugenzi wa TAKUKURU haitabaki salama kwa kauli na mienendo ya namna hiyo ikiendelea kutolewa.
Huyu kateuliwa na mwenyekiti wa ccm, unategemea atachukua hatua.? Tulishasema ccm ileile wote wahalifu hakuna mkweli
 
Back
Top Bottom