Mtatiro ampinga Waziri Mkuu Majaliwa

assadsyria3

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
6,903
4,051
TUSIUE DEMOKRASIA KWA KISINGIZIO CHA
“HAPA KAZI TU”!
Na. Mtatiro J, “Darubini ya Mtatiro” Gazeti la
Mwananchi, Jumapili 27 Disemba 2015
Tamko la Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Tanzania
mhe. Kasimu Majaliwa alilolitoa wilayani
Ruangwa wakati anaongea na vyombo vya
usalama wa ndani wa nchi kwamba, wagombea
walioshindwa uchaguzi hawaruhusiwi kupita na
kuwashukuru wananchi ni lazima ipingwe na kila
mtu. Hii ni kauli hatari sana kutolewa na mtu wa
hadhi ya Waziri Mkuu, ambaye hajamaliza hata
mwezi mmoja madarakani.
Kauli hii ya Waziri Mkuu siyo yake peke yake,
aliitoa kwa niaba ya serikali yake na kusisitiza
kuwa “tumeshakubaliana ndani ya serikali”.
Nimekosa maelezo mazuri ya kushangazwa na
kauli hiyo lakini itoshe kusema kuwa mtu yeyote
anayefuatilia siasa za Tanzania huku akijifunza
kutoka katika siasa za nchi za wenzetu anajua
kuwa hiyo ni kauli ya kupuuzwa na kudharauliwa
kwa sababu inapingana na misingi ya kikatiba na
kisheria ambayo nchi yetu imejiwekea.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
imeshatoa haki mbalimbali na za msingi ambazo
hata Rais hana uwezo wa kuzipokonya, ni haki za
kikatiba.
Ibara ya 18.-(1) ya Katiba yetu inaeleza wazi
kuwa “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu
yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje
mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa
habari na dhana zozote kupitia chombo chochote
bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru
wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati”. Ibara hii
inatoa uhuru kwa wananchi bila kujali vyeo wala
kada, kutoa maoni na mawazo yao, kwenda
mahali kwa ajili ya kupokea taarifa au kutoa
taarifa, bila kujali mipaka ya nchi. Je Waziri Mkuu
na serikali wameamua kukifuta kipengele hiki?
Ibara ya 18 (2) ya katiba ya Tanzania inaendelee
kusisitiza kuwa “Kila raia anayo haki ya kupewa
taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali
nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa
maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya
masuala muhimu kwa jamii.” Waziri Mkuu na
serikali wanapopiga marufuku wagombea
walioshindwa katika uchaguzi kukutana na
wananchi na kuongea nao kwa maana ya
kuwashukuru, je wanatekeleza matakwa ya
kikatiba ya ibara hii kutaka watu wapewe taarifa?
Ibara ya 20.-(1) ya katiba ya Tanzania imeeleza
wazi kuwa “Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya
kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine
kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na
kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga
na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa
madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au
maslahi yake au maslahi mengineyo”. Ibara hii ina
maana kwamba kila mtu bila kujali ni mgombea,
alikuwa mgombea au hakuwa mgombea anayo
haki ya kukutana na watu wengine bila kuathiri
amani ya nchi? Hivi mgombea gani ambaye
akienda kukutana na wananchi kwa hiyari
(wananchi watakaotaka) atakuwa ameharibu au
kuhatarisha amani na usalama wa nchi? Je,
tamko la Waziri Mkuu na serikali limekanyaga
kipengele hiki cha katiba kwa kiasi gani?
Ushahidi mwingine wa wazi uko kwenye Ibara ya
21.-(1) ya katiba ya Tanzania, inasomeka “Bila
ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya
67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana
na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au
kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za
utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli
za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa
kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi
kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”.
Ibara hii inasisitiza kwamba kila mwananchi
(mgombea, asiyekuwa mgombea, aliyeshinda
uchaguzi, asiyeshinda uchaguzi n.k.) anayo haki
ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi.
Na ushiriki wa utawala wan chi unahusisha njia
zote muhimu, kuwa mtendaji, kuwa mfuatiliaji na
anayehoji ili serikali itende, kuchukua hatua za
kushauri n.k. Najiuliza, kabla Majaliwa hajatoa
tamko lile la “kidikteta” hakuwa amesoma katiba
hii?
Huwenda tutamlaumu Waziri Mkuu wetu bure na
serikali yake. Huwenda hakuwa ameisoma katiba
ambayo aliahidi kuilinda, huwenda hajui
alichokisema na madhara yake. Lakini kama
ameshaikanyaga katiba, kwani hajui kuna sheria
iliyoanzisha chama chake na ndiyo maana akawa
mbunge kupitia chama hicho ambacho imefuzu
vigezo vya kutoa Waziri Mkuu kwenye serikali ya
sasa? Kasimu Majaliwa hajawahi kuisoma Sheria
namba 258 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992
kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002?
(The Political Parties Act of 1992 as revised in
2002)?
Kifungu cha 11 cha sheria hii kimeeleza wazi
kuwa kila chama cha siasa chenye usajili wa
muda na wa kudumu kina haki zote za kufanya
mikutano katika eneo lolote la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania baada ya kutoa taarifa
za mkutano huo kwa Ofisa wa Polisi anayehusika
na eneo hilo. Kila chama cha siasa kinapaswa na
kinabanwa na sheria kuvisaidia vyombo vya dola
kutunza amani katika eneo hilo n.k. Mbona sheria
ziko wazi kiasi hiki? Ni sheria ipi inayompa
mamlaka Waziri Mkuu au serikali “ku-suspend”
au kufuta haki za kikatiba na za kisheria za
wananchi, vyama vya siasa n.k.?
Kama hakuna sheria inayompa mamlaka hayo
Waziri Mkuu na serikali kutoa amri ya namna hii
sisi wananchi ambao tunaamini kuwa Waziri
Mkuu na serikali nzima waliapa kuilinda na
kuitetea katiba ya Tanzania na sheria zake
tueleweje? Je, Waziri Mkuu anatufundisha nini?
Kwamba tuige nini kutoka kwake? Dharau kwa
katiba! Kuipuuza sheria? Kwamba wananchi wa
Tanzania wanapata mfano gani kutoka kwa
kiongozi wao mkuu, anawafundisha wananchi
wafanye nini? Yeye anafanya nini?
Matamko ya namna hii ya kimakusudi na yenye
lengo la kujinufaisha kisiasa kwa chama kimoja
ndiyo huwa yameleta vurugu na cmachafuko
katika nchi nyingi za Afrika. Amani ya Tanzania
haitalindwa kwa kuvunja katiba na kuondoa haki
za kiraia, amani itadumu ikiwa haki za kiraia
zinaheshimiwa na serikali. Amani itadumu ikiwa
serikali na viongozi wake ndiyo wanakuwa mstari
wa mbele katika kulinda na kutetea katiba ya
Tanzania.
Majaliwa na serikali ya CCM wajitathmini upya,
kauli mbiu ya hapa kazi tu ina maana ya
kuhamasisha kila mtanzania achape kazi, kauli
hiyo haina maana ya kuwapora watanzania haki
zao za msingi.
Tukutane Jumapili ijayo kwenye darubini nyingine.
TUWASILIANE: juliusmtatiro@yahoo.com,
 
Kuna sifa iliyojijengea kwa muda mfupi inaweza kutoweka kwa kukiuka misingi ya kidemokrasia iliyojengeka hapa Tanzania.
 
Demokrasia tz bado kwa kweli wapinzani wanajitahd mno ktk mazingira ya Tz ambapo mpinzani kufa km A.Mawazo siyo shida.
 
Lazima tukubali uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa wananchi kuijenga nchi yao chini ya rais walieyemchagu, waziri mkuu yuko sahihi kupiga marufuku kwasababu wenye nia ya kuwashukuru wananchi watakuja kudai kufanya maandamano na mambo mengine ya kisiasa ambayo hayana tija kwa sas, wananchi waachwe wafanye kazi za maendeleo kwa sasa
 
Kweli ndege wafafanao huruka kwa pamoja. Huyu jamaa na mteuzi wake akili zinafanana; Hakuna mwenye mawazo mbadala. Tutaona!
 
Lazima tukubali uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa wananchi kuijenga nchi yao chini ya rais walieyemchagu, waziri mkuu yuko sahihi kupiga marufuku kwasababu wenye nia ya kuwashukuru wananchi watakuja kudai kufanya maandamano na mambo mengine ya kisiasa ambayo hayana tija kwa sas, wananchi waachwe wafanye kazi za maendeleo kwa sasa
Hata kushukuru wananchi nayo ni KAZI!
 
Kwani kuna lipi la ajabu? Nani asiyejua kulitokea nini baada ya kupiga kura na kura kuhesabiwa na kubandikwa vituoni nchi nzima? Mwananchi yeyote mwenye uwezo wa kufuatilia alikuwa na haki ya kujumlisha matokeo ya vituo vyote nchi nzima na kujua nani mshindi kuanzia diwani, mbunge na rais. Kwa upande wa rais hakuna mtu anayeruhusiwa kutangaza (sio kujumlisha) matokeo zaidi ya mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.
Kwa aliyeshinda/shindwa sioni kosa lolote la kwenda kwa wananchi kutoa pole na shukrani kwa kufanya kampeni kwa amani hatimaye mshindi akapatikana. CCM wasiwe na wasiwasi wowote wachape kazi walete mababadiliko kwa wananchi ndicho kila mtu anangojea!
 
:…@@::::@?@::::::::::::::::……:…"_--……::"::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::: said:
[FONT=Book Daudi:: , post Antiqua]kama hujui maana ya siasa za vyama vingi kaa kimya.[/FONT]

Maana ya siasa za vyama vingi ni kushukuru ukishindwa? kushukuru???
 
Lazima tukubali uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa wananchi kuijenga nchi yao chini ya rais walieyemchagu, waziri mkuu yuko sahihi kupiga marufuku kwasababu wenye nia ya kuwashukuru wananchi watakuja kudai kufanya maandamano na mambo mengine ya kisiasa ambayo hayana tija kwa sas, wananchi waachwe wafanye kazi za maendeleo kwa sasa

Unabwabwaja hujui hata kilichoandikwa. Hivi kumbe watu wanapiga kelele kila siku kuwa katiba ya nchi imebeba mambo mengi sana ikiwemo haki za msingi za ushiriki katika mambo muhimu yanayohusu wananchi wewe hujawahi kujaribu hata kufungua akili yako kujua ni mambo gani hayo. Huwezi kuzuia kufanyika mikutano ya kisiasa kisa et uchaguzi umeisha. Hapa naona tunafutiana agenda za kuandamwa siku zijazo. Kumbukeni matamko yanayotolewa kijingajinga namna hii yaliwafanya wengine watoe machozi kama watoto baada ya kubanwa bungeni.
 
TUSIUE DEMOKRASIA KWA KISINGIZIO CHA
“HAPA KAZI TU”!
Na. Mtatiro J, “Darubini ya Mtatiro” Gazeti la
Mwananchi, Jumapili 27 Disemba 2015
Tamko la Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Tanzania
mhe. Kasimu Majaliwa alilolitoa wilayani
Ruangwa wakati anaongea na vyombo vya
usalama wa ndani wa nchi kwamba, wagombea
walioshindwa uchaguzi hawaruhusiwi kupita na
kuwashukuru wananchi ni lazima ipingwe na kila
mtu. Hii ni kauli hatari sana kutolewa na mtu wa
hadhi ya Waziri Mkuu, ambaye hajamaliza hata
mwezi mmoja madarakani.
Kauli hii ya Waziri Mkuu siyo yake peke yake,
aliitoa kwa niaba ya serikali yake na kusisitiza
kuwa “tumeshakubaliana ndani ya serikali”.
Nimekosa maelezo mazuri ya kushangazwa na
kauli hiyo lakini itoshe kusema kuwa mtu yeyote
anayefuatilia siasa za Tanzania huku akijifunza
kutoka katika siasa za nchi za wenzetu anajua
kuwa hiyo ni kauli ya kupuuzwa na kudharauliwa
kwa sababu inapingana na misingi ya kikatiba na
kisheria ambayo nchi yetu imejiwekea.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
imeshatoa haki mbalimbali na za msingi ambazo
hata Rais hana uwezo wa kuzipokonya, ni haki za
kikatiba.
Ibara ya 18.-(1) ya Katiba yetu inaeleza wazi
kuwa “Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu
yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje
mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa
habari na dhana zozote kupitia chombo chochote
bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru
wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati”. Ibara hii
inatoa uhuru kwa wananchi bila kujali vyeo wala
kada, kutoa maoni na mawazo yao, kwenda
mahali kwa ajili ya kupokea taarifa au kutoa
taarifa, bila kujali mipaka ya nchi. Je Waziri Mkuu
na serikali wameamua kukifuta kipengele hiki?
Ibara ya 18 (2) ya katiba ya Tanzania inaendelee
kusisitiza kuwa “Kila raia anayo haki ya kupewa
taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali
nchini na duniani kote ambayo ni muhimu kwa
maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya
masuala muhimu kwa jamii.” Waziri Mkuu na
serikali wanapopiga marufuku wagombea
walioshindwa katika uchaguzi kukutana na
wananchi na kuongea nao kwa maana ya
kuwashukuru, je wanatekeleza matakwa ya
kikatiba ya ibara hii kutaka watu wapewe taarifa?
Ibara ya 20.-(1) ya katiba ya Tanzania imeeleza
wazi kuwa “Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya
kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine
kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na
kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo
hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga
na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa
madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au
maslahi yake au maslahi mengineyo”. Ibara hii ina
maana kwamba kila mtu bila kujali ni mgombea,
alikuwa mgombea au hakuwa mgombea anayo
haki ya kukutana na watu wengine bila kuathiri
amani ya nchi? Hivi mgombea gani ambaye
akienda kukutana na wananchi kwa hiyari
(wananchi watakaotaka) atakuwa ameharibu au
kuhatarisha amani na usalama wa nchi? Je,
tamko la Waziri Mkuu na serikali limekanyaga
kipengele hiki cha katiba kwa kiasi gani?
Ushahidi mwingine wa wazi uko kwenye Ibara ya
21.-(1) ya katiba ya Tanzania, inasomeka “Bila
ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya
67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana
na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au
kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za
utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya
Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli
za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa
kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi
kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu
uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”.
Ibara hii inasisitiza kwamba kila mwananchi
(mgombea, asiyekuwa mgombea, aliyeshinda
uchaguzi, asiyeshinda uchaguzi n.k.) anayo haki
ya kushiriki katika shughuli za utawala wan chi.
Na ushiriki wa utawala wan chi unahusisha njia
zote muhimu, kuwa mtendaji, kuwa mfuatiliaji na
anayehoji ili serikali itende, kuchukua hatua za
kushauri n.k. Najiuliza, kabla Majaliwa hajatoa
tamko lile la “kidikteta” hakuwa amesoma katiba
hii?
Huwenda tutamlaumu Waziri Mkuu wetu bure na
serikali yake. Huwenda hakuwa ameisoma katiba
ambayo aliahidi kuilinda, huwenda hajui
alichokisema na madhara yake. Lakini kama
ameshaikanyaga katiba, kwani hajui kuna sheria
iliyoanzisha chama chake na ndiyo maana akawa
mbunge kupitia chama hicho ambacho imefuzu
vigezo vya kutoa Waziri Mkuu kwenye serikali ya
sasa? Kasimu Majaliwa hajawahi kuisoma Sheria
namba 258 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992
kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002?
(The Political Parties Act of 1992 as revised in
2002)?
Kifungu cha 11 cha sheria hii kimeeleza wazi
kuwa kila chama cha siasa chenye usajili wa
muda na wa kudumu kina haki zote za kufanya
mikutano katika eneo lolote la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania baada ya kutoa taarifa
za mkutano huo kwa Ofisa wa Polisi anayehusika
na eneo hilo. Kila chama cha siasa kinapaswa na
kinabanwa na sheria kuvisaidia vyombo vya dola
kutunza amani katika eneo hilo n.k. Mbona sheria
ziko wazi kiasi hiki? Ni sheria ipi inayompa
mamlaka Waziri Mkuu au serikali “ku-suspend”
au kufuta haki za kikatiba na za kisheria za
wananchi, vyama vya siasa n.k.?
Kama hakuna sheria inayompa mamlaka hayo
Waziri Mkuu na serikali kutoa amri ya namna hii
sisi wananchi ambao tunaamini kuwa Waziri
Mkuu na serikali nzima waliapa kuilinda na
kuitetea katiba ya Tanzania na sheria zake
tueleweje? Je, Waziri Mkuu anatufundisha nini?
Kwamba tuige nini kutoka kwake? Dharau kwa
katiba! Kuipuuza sheria? Kwamba wananchi wa
Tanzania wanapata mfano gani kutoka kwa
kiongozi wao mkuu, anawafundisha wananchi
wafanye nini? Yeye anafanya nini?
Matamko ya namna hii ya kimakusudi na yenye
lengo la kujinufaisha kisiasa kwa chama kimoja
ndiyo huwa yameleta vurugu na cmachafuko
katika nchi nyingi za Afrika. Amani ya Tanzania
haitalindwa kwa kuvunja katiba na kuondoa haki
za kiraia, amani itadumu ikiwa haki za kiraia
zinaheshimiwa na serikali. Amani itadumu ikiwa
serikali na viongozi wake ndiyo wanakuwa mstari
wa mbele katika kulinda na kutetea katiba ya
Tanzania.
Majaliwa na serikali ya CCM wajitathmini upya,
kauli mbiu ya hapa kazi tu ina maana ya
kuhamasisha kila mtanzania achape kazi, kauli
hiyo haina maana ya kuwapora watanzania haki
zao za msingi.
Tukutane Jumapili ijayo kwenye darubini nyingine.
TUWASILIANE: juliusmtatiro@yahoo.com,
Wekeni DEMOKRASIA Kwenye vyama vyenu kwanza kabla hamjazungumzia neno hilo.Hata ya Kubumbabumba kama ya CCM inatosha...............Vinginevyo mwogopeni Mungu
 
Mtatiro yuko sahii Majaliwa atafakari mara mia, hivi vyama ni kwa mujibu wa katiba iliyopo sio aliyetunga yeye.
 
Back
Top Bottom