Wanajamii Habari ya mwenzetu kuwa ndani ni ukweli na imethibitishwa na ndugu na jamaa zake wa karibu ikiwa ni pamoja na rafiki yake wa kike (mzazi mwenzie) ambaye anaishi eneo/ nyumba moja na Mtuhumiwa,ndugu hawa wanaishi Columbia,Maryland........Jina la ndugu yetu huyo litatajwa hapa baadaye kwa idhini ya Kaka yake.
Ni jambo kubwa na linalosikitisha,ikiwa kama Jamii iliyostaarabika inabidi tusaidiane katika kuelimishana na kuelekezana baadhi ya mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa sheria,ni vyema ikumbukwe kuwa hatuko nyumbani...kwa maana hiyo ni vyema kuishi kwa kufuata na kutii taratibu za sheria.Tofauti ya hivyo tutakuwa tunajenga sifa mbaya na kuharibu jina Tanzania.....Tuna watoto na Wajukuu huko,tusiwaharibie maisha kwa sababu tu Baba/Mama zao tulishindwa kuishi katika misingi ya HAKI na USTAARABU.
Nimepata mshtuko mkubwa baada ya kuambiwa kuwa Watanzania nasi tumekuwepo kwenye macho ya sheria baada ya miaka ya karibu kuzidi kuonekana ktk vyombo vya sheria haswa kwa uvunjaji wa taratibu za maisha,ama kwa uizi,ubakaji,Ugomvi,Fujo (kelele),kutolipa pango, kuchinja mifugo hadharani au kulewa kupita kiasi.Kwa maana hiyo inabidi tuangalie upya tabia zetu ili kujenga Jamii yenye Heshima.
Ndugu yetu tunayemzungumzia, amepata matatizo kwa masuala yanayohusu "Ununuzi na uuzaji wa nyumba",matatizo hayo sio ya kwake tu,kuna ripoti kuwa kuna Watanzania wengine katika majimbo ya Arizona,Illinois,Minnesota na Texas ama wanaangaliwa au wamekwishaitwa kwenye vyombo vya dola kujibu mashitaka ya "Ujanja wa biashara za nyumba".Na baadhi ya ndugu hao ama wamekimbilia Canada au kurudi nyumbani kwa kuogopa mkono wa Serikali.......Pamoja na mashtaka hayo,ndugu yetu huyo wa Maryland ana mashtaka mengine karibu 40 yaliyosomwa kwake kwenye mahakama ya Rockville,MD.
Tuendelee kuelimishana na kuelekezana namna ya kuishi kwa kujali sheria....Lakini bado kwa umoja wetu nafikiri inapaswa kuangalia namna ya kumsaidia mwenzetu!!
Jana tu ulipoanzisha hii thread nilijua kuwa jamaa ni mwizi....sina sympathy na hawa "mabingwa" wanaotaka fweza za fasta fasta ktk nchi za watu, ufisadi huko huko bongo hii ni nchi ya sheria, ukizivunja basi sooo ni lako mwenyewe!
Uki-google jina la hiyo kampuni yake unapata haya hapo chini:
MAMBO JAMBO, USA.
New entartainment company.
Established in 2001.
Based in arusha, tanzania.
We have recording studio in dar-es salaam, tanzania.
We have a radio station in arusha, tanzania (. Mj FM 93.0)
Our main office for entartainment and general supply is in Washington DC.
We supply everything all over the world includes food, electronics, building materials, etc Construction Materials Stocks ,Entertainment Projects ,Network Communications ,Truck & Parts ,
Business Type Distributor/Wholesaler
Products/Services Entartainment products, food, electronics, building materials
Our Markets Worldwide
No. of Employees 11 - 50 People
Mr. (nimefuta jina)
Address 8821 Goose Landing Cirlce, Columbia, Maryland, Tanzania
Zip Code 21045
Telephone +001 410 997-0992
Mobile 4109080923
Fax +001 410 997-0992
Website Mambo Jambo (Usa),
Mambo Jambo (Usa)
Address hiyo imepinda,
"8821 Goose Landing Cirlce, Columbia, Maryland, Tanzania." Toka lini??? Entertainment company gani ipo 'ivo?? Waajiliwa kati ya 11-50, hai-make sense (kwanini isiwe ni 11 au 50 badala ya huo uzushi wa 11-50??)...na maswali mengine kibao!!!
Watu waende shule, ukiwa na elimu hata ya community college hapa USA opportunities ni kibao wajameni! Hizi story wengine tumezichoka, mchango nitatoa kwa mtu mwenye issues na INS/ICE (noma yenyewe pia iwe ya kueleweka)....
Hata 'ivo pole mingi kwa huyo
starring na familia yake, ndio ukubwa!!