Mtanzania mfanyabiashara afariki ghafla nchini China

Mtanzania mfanyabiashara afariki ghafla nchini China

Zakamwamoba

Senior Member
Joined
Jul 28, 2016
Posts
175
Reaction score
609

Picha ya Marehemu enzi za uhai wake

Simanzi na majonzi vimetawala kwa Watanzania waishio nchi China baada ya kuondokewa na Mtanzania mwenzao ndugu HAMIS RUHABAYE.

Hamis ambae alikuwa Mfanyabiashara katika mji wa Guanzhou kwa muda mrefu na alikuwa anaishi pamoja na familia yake amefariki Dunia leo Jumatano Januari 17,2018.

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Bw. Abraham ( Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Kitanzania wanaoshi China) Amesema Marehemu alifariki ghafla kutokana Matatizo ya Moyo.

Bw. Abraham amesema tayari wamekaa na wameafikiana kwamba Bajeti inayohitajika kwa ajili ya kusafirisha Mwili, Familia na Mizigo mbalimbali hadi Tanzania ni 20,000 USD.

Watanzania waliopo nchini humo kwa pamoja wameanza kuchangishana ili kupata kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la usafirishaji.


MTILAH BLOG
http://www.mtilah.com/2018/01/mfanyabiashara-mtanzania-afariki-ghafla.html
 
Kama mtu alikuwa anaishi na familia yake huko Chiña, kwa nini asizikwe huko?
Kwanini usingeandika tu kuliko ku quote uzi mrefu alafu una comment pumba!! Kwani maziko si wanakubaliana familia wewe unahusika vp[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huwa napenda na nafurahi mno nikikutana na post ya Mtu wa JamiiForums anayejua ' Kufikiri ' kama Wewe Mkuu. Umesema kitu sahihi kabisa na nakuunga mkono kwa 100%.
Huyo mtu ana mamaake ana baabaake ana kakazake ana dadazake ana wajomba mashangazi wakumrehem unahisi wote watakuwa china!? Unajua china utamaduni wao wa kuzika!!? Wewe ukiwa na mkewako kikazi india ukifa utaprnda uzikiwe india!? Ni mtazamo tu usijenge chuki! [emoji109] [emoji109] nothng personally
 
Back
Top Bottom