Miss Halima
Senior Member
- Aug 4, 2026
- 198
- 441
Kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Mabula Msanga, mwenye umri wa miaka 23, amejiunga rasmi na klabu ya JS Kabylie ya Algeria.
Mabula, anayesifika kama kiungo mkabaji, amejiunga na klabu hiyo kwa uhamisho huru baada ya kumaliza mkataba wake na Şamaxı FK ya Azerbaijan.
JS Kabylie imethibitisha usajili wake Agosti 31, 2026, Usajili huo unakuwa hatua nyingine muhimu katika safari ya Mabula ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa Tanzania wanaocheza nje ya nchi.
Kiungo huyo wa Taifa Stars sasa anatarajiwa kuanza ukurasa mpya katika soka la Algeria, huku akipewa jukumu la kuongeza nguvu na uimara katika eneo la kiungo la JS Kabylie.