Mtanzania ang’ara tuzo ya utalii Afrika

Mtanzania ang’ara tuzo ya utalii Afrika

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi, ameingia katika orodha ya wanawake 100 bora barani Afrika wanaojishughulisha na utalii.

MKURUGENZI%20Mtendaji%20wa%20Bodi%20ya%20Utalii%20Tanzania%20%28TTB%29%2C%20Devota%20Mdachi%2C.jpg

MKURUGENZI Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi.
​

Mbali na Mdachi, wanawake wengine wawili katika ukanda huu waliongia katika orodha hiyo ni Zainab Ansell, mmiliki wa kampuni ya Zara Tanzania Adventures na raia wa Kenya, Charity Githinji, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tandaza Africa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusu uzo hiyo, wanawake hao walisema mbali na kuitangaza Tanzania kimataifa, pia inaonyesha ni namna gani wanawake wanavyochangamkia fursa za kiuchumi, ikizingatiwa kuwa utalii ni miongoni mwa sekta zinazoliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

“Akwaaba ni taasisi kubwa ya utalii duniani na tamasha lake linaingia katika matamasha manne makubwa duniani likiwamo la Indaba la Afrika Kusini na ITB Berlin la Ujerumani. Hivyo kupata tuzo hii ni heshima kwangu, lakini pia bendera ya Tanzania imepeperushwa vyema,” alisema Mdachi.

Akizungumzia safari yake katika sekta ya utalii, alisema alianza kama ofisa habari wa TTB mwaka 1993, akiwa mwanamke wa kwanza kushika cheo hicho nchini na kutokana na mapenzi yake katika utalii, alipanda vyeo huku akiendelea kuweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini kushika vyeo hivyo hadi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo ambayo pia imeshikwa kwa mara ya kwanza na mwanamke.

“Hakuna kinachoshindikana ikiwa utafanya kazi kwa dhati. Nawaasa wanawake wenzangu kuingia katika sekta hii ya utalii kwa sababu kuna fursa nyingi vile vile inakupa fursa ya kuyajua maeneo yenye vivutio duniani,” alisema Mdachi.

Tuzo hiyo iitwayo ‘Top 100 African Women in Tourism’ hutolewa kila mwaka na waandaaji wa tamasha kubwa la utalii Akwaaba African Travel Market ambalo lilifanyika Lagos, Nigeria Septemba 11, mwaka huu.

Kwa upande wake, Ansell akizungumzia tuzo aliyopata, alisema haikuwa kazi rahisi kuwa sehemu ya wanawake 100 wanaofanya vizuri katika utalii barani Afrika kwa sababu waandaaji waliangalia vigezo vingi ikiwamo ufanisi katika kazi na ubunifu.

“Utalii unahitaji kujituma na kukutana na watu mara kwa mara. Wanawake wasilale waanzishe kampuni za utalii kwa sababu kuna mambo mengi ambayo hayajaguswa katika sekta hii. Hata utalii wa utamaduni unawezekana kwa kupika vyakula vya asili au upande wa mavazi,” alisema.

Naye Githinji ambaye mbali na kuwa raia wa Kenya ana kampuni ya utalii inayofanya kazi nchini, alisema licha ya ugumu uliopo katika sekta hiyo, bado anaamini hakukosea kuchagua kuingia kwenye biashara ya utalii.


CHANZO: Nipashe
 
Back
Top Bottom