Mtanzania afungwa jela London kwa kosa la kupost maiti facebook

Imetokea huko Westminster, Uingereza ambapo Mtanzania aliyejulikana kwa majina ya Omega Mwaikambo (43), alipohukumiwa jela miezi mitatu kwa kusambaza picha za wafu wa ajali ya moto iliyotokea kwenye Jengo la Grenfell, tarehe 14/6/2017.

Wakati wenzetu wakiheshimu picha za wafu, na picha za matukio yasiyopendeza, huku kwetu ni tofauti kabisa. Mtu anaenda msibani anapiga picha ya mfu bila hata ya idhini ya ndugu wa marehemu kisha anaisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Watu walioathirika na magonjwa kama vile cancer, au mengine ya kutisha, picha zao zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kila siku. Halafu wasambazaji, walivyo majuha, unakuta wanatoa wito kwa wasomaji waandike AMEN, na wachangiaji kwa ujuha wao mara mbili badala ya kukemea tabia hiyo nao wanachangia kwa kuandika AMEN.

Ebu, tujiulize, hivi utajisikiaje siku moja ukikuta mtu kaweka picha ya marehemu ambaye ni dada yako, kaka yako, au mke wako, mume wako, ama mtoto wako aliyepoteza maisha kwa ajali ya moto, na picha hiyo ikimuonesha marehemu akiwa kaungua kama mshikaki?

http://www.telegraph.co.uk/…/man-jailed-sharing-photo-dead…/
View attachment 525886

Mijitu mingine haina akili sijui hawajisikiagi vibaya kupost picha za watu ambao wamepatwa na majanga.
 
Inapokuja suala la uhuru wa habari mitandaoni huwa kuna mipaka yake, huko Uingereza kuna mtanzania amefungwa jela kwa kupiga picha maiti za wahanga wa moto halafu akarusha kwenye Facebook, hapa Tanzania ingefanyika hivyo leo humu kwenye mitandao kila lawama na matusi yangekuwapo dhidi ya serikali mbali na hayo
mawakili maarufu wangejitokeza kukataa rufaa. Hapa Tanzania inapotokea ajali kitu cha kwanza badala ya kuokoa ama kusitiri mwili wa marehemu mtu anaanza kupiga picha na kutawanya kwenye mitandao ya kijamii.
Serikali ichukue hatua kama hii ya Uingereza ili tabia hii ikome.
 
c312c689fd8638cd4bc9475ece2ce0c4.jpg
Ona hili jinga limepost tena!! Mods kwa nini msimban for ever?
 
mmmnh sad kwa kweli,inabidi kujifunza maadili ya ugenini kwanza kabla hujatulia ,lol kosa lake sio kubwa kiihivyo,lol(msije mkanikamata na mimi,lol)
 
Back
Top Bottom