Mtanzania aaga dunia huko Rwanda

Mtanzania aaga dunia huko Rwanda

papa anayevutia

Senior Member
Joined
Sep 5, 2012
Posts
153
Reaction score
52
Ndugu wanajukwaa..naleta habari za masikitiko za kifo cha Mtanzania mwenzetu aliyefariki kwa ajali ya maji hapa Rwanda.Kifo kimemkuta leo mida ya saa nne katika ziwa Kivu- mjini Gisenyi/Rubavu karibu na mpaka wa Goma/Kongo.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina Nasib Athuman(23),Mkazi wa Kinondoni(mchaga);alikuwa katika safari ya masafa marefu kutoka DSM kuelekea Goma-Kongo.Leo asubuhi walifika Gisenyi.Huku taratibu za kuvuka mipaka zikiendelea kijana huyo alikuwa na watanzania wenzake akiwemo kaka yake waliyekuwa pamoja katika roli hilo la mizigo; baada ya kuchezacheza mpira kijana huyo aliamua kwenda kuogelea ziwani(lipo eneo hilo).
Hivyo kijana alielekea eneo moja karibu na hotel ya serena..alijirusha majini(diving)..basi alivyo-dive hakuweza kutokea tena hadi vijana walipoamua kufuatilia na kumkuta chini kabisa akiwa ameshakata roho.Maiti ya kijana huyo imehifadhiwa katika hospitali ya serikali-Gisenyi.Tunasubiri kesho(siku ya kazi) ili kwa kushirikiana na mamlaka husika tutoe taarifa ubalozi wa Tanzania-Kigali kuona taratibu za kusafirisha mwili hapo kesho..Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.Amina

CHANZO CHA HABARI: mimi mwenyewe nipo eneo la tukio
 
Inna lillahi wa Inna ilaihi rajiun.
Poleni sana mungu amuweke mahala Pema peponi.
Vingenevyo:
Humu watu wakianza kuandika au kutoa taarifa za vilio, nafasi ya kubadilishana hoja itakuwa haipo kabisa.
Labda kwa kuwa Huyu mtanzania ni mchaga nini ndo maana taarifa yake inatolewa.?
 
poleni sana ila isije ikawa kuna hujuma zimefanywa na huyo dikteta maana mpaka sasa hatupo kwenye uhusiano mzuri
 
RIP Kijana Nasib Athumani(mchagga)
Lakini MODS mada nyingi zinaondolewa hapa, je hii ni siasa?
Maintain your standards!
 
Ndugu wanajukwaa..naleta habari za masikitiko za kifo cha Mtanzania mwenzetu aliyefariki kwa ajali ya maji hapa Rwanda.Kifo kimemkuta leo mida ya saa nne katika ziwa Kivu- mjini Gisenyi/Rubavu karibu na mpaka wa Goma/Kongo.

Kijana huyo aliyejulikana kwa jina Nasib Athuman(23),Mkazi wa Kinondoni(mchaga);alikuwa katika safari ya masafa marefu kutoka DSM kuelekea Goma-Kongo.Leo asubuhi walifika Gisenyi.Huku taratibu za kuvuka mipaka zikiendelea kijana huyo alikuwa na watanzania wenzake akiwemo kaka yake waliyekuwa pamoja katika roli hilo la mizigo; baada ya kuchezacheza mpira kijana huyo aliamua kwenda kuogelea ziwani(lipo eneo hilo).
Hivyo kijana alielekea eneo moja karibu na hotel ya serena..alijirusha majini(diving)..basi alivyo-dive hakuweza kutokea tena hadi vijana walipoamua kufuatilia na kumkuta chini kabisa akiwa ameshakata roho.Maiti ya kijana huyo imehifadhiwa katika hospitali ya serikali-Gisenyi.Tunasubiri kesho(siku ya kazi) ili kwa kushirikiana na mamlaka husika tutoe taarifa ubalozi wa Tanzania-Kigali kuona taratibu za kusafirisha mwili hapo kesho..Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe.Amina

CHANZO CHA HABARI: mimi mwenyewe nipo eneo la tukio

jina siyo geni,wanafanya kazi P trucks?
 
Heading haina faida ni kujaribu kuweka hisia...kumbe kaamua kujivika mwenyewe ...Mchagga na kuogelea wapi na wapi?
 
Naam @ Haki sawa yawezekana kwa mtazamo wako..nilitaka kuuamsha ubalozi wetu ambao huwa haujui ni nini huwa kinaendelea kwa watz wanaokuwa wanahitaji msaada.si ajabu wakapigiwa simu kesho wakala kona
 
Janja ya wanyarwanda ya kutaka kuwaonesha watanzania kuwa eti wana huruma na sisi!
 
Inna lillahi wa Inna ilaihi rajiun.
Poleni sana mungu amuweke mahala Pema peponi.
Vingenevyo:
Humu watu wakianza kuandika au kutoa taarifa za vilio, nafasi ya kubadilishana hoja itakuwa haipo kabisa.
Labda kwa kuwa Huyu mtanzania ni mchaga nini ndo maana taarifa yake inatolewa.?
Hahahha ..kaka sio sababu ya uchagga..ni mazingira tu..lengo ni ubalozi pale kigali ushtuke kidogo..maana una tabia ya kulalalala..kumbuka huyu ni konda tu..na maiti yabidi isafirshwe..so msaada wa ubalozi unahitajika
 
Jamani post zingine! Mi nilidhani kauwawa kumbe kajiachia mwenyewe kwenye maji?! Poleni
 
Back
Top Bottom