Mtanzania aacha kukalia uchumi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtanzania aacha kukalia uchumi

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MziziMkavu, Feb 26, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 491"]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mtanzania aacha kukalia uchumi[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD][​IMG][/TD]
  [TD]
  Andrew Mbogoma Ngiri, mtanzania mwenye wake watatu na watoto 34 ameamua kuacha kuukalia uchumi na kuutumia pale alipouza ng'ombe wake 250 na kujipatia mamilioni ya fedha yaliyomwezesha kujenga nyumba ya kisasa ya kulala wageni yenye vyumba 14.
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Ngiri anaishi katika Mtimbira Ulanga Morogoro. Hatua hiyo ni mkakati maalumu wa kupunguza mifugo (uchumi) aliyokuwa nayo hapo awali iliyofikia zaidi ya elfu moja na sasa kubakiwa na ng'ombe 700 ambapo pia anakusudia kupunguza tena ili kununua trekta kwa ajili ya shughuli za kilimo.

  Bwana huyo alifanya uamuzi huo baada ya kupata elimu iliyomtaka abadilike kutoka ufugaji wa kuhamahama na kuwa wa kisasa akiwa na mifugo michache zaidi yenye tija bila kuchafua mazingira. Kwa mujibu wa mfugaji huyo, elimu hiyo iliyotolewa na Ofisa wa Mifugo wa Wilaya ya Ulanga, Dk Frederick Sagamiko, imembadilisha kabisa.

  Mfugaji Andrew amenukuliwa na vyombo vya habari akisema "Mimi sijasoma na wala umri wangu siufahamu, lakini elimu niliyopata imezaa matunda kwangu na wenzangu wa kabila la Wasukuma, wameitikia mwito huu na sasa wamepunguza ng'ombe na wengine wapo kwenye mchakato wa kupunguza," Elimu anayokusudianhapa ni ile ya kujua namna ya kuutumia uchumi na kuwa mfugaji mwenye tija sio kujaza ming`ombe huku unahesabiwa masikini.

  Pia alisema kutokana na elimu aliyoipata, ameanza mkakati wa kutumia mifugo aliyonayo kuweza kuwasomesha watoto wake kuanzia elimu ya Msingi hadi Vyuo Vikuu, ili siku za usoni waweze kujitengemea wenyewe. [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3, align: center"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo.Mtanzania aacha kukalia uchumi

  Bravo umebadilisha biashara nakutakia kila la kheri inshallah.

  [​IMG]
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,125
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa watalamu wa Biashara huyo mzee hakuna alicho fanya na hapo sana sana alishauriwa na wanasiasa wanao fanya ziara huko kwamba uza ng'ombe wako.

  Mkuu na hili ndo Tatizo kubwa sana linalo tukabili watanzania wengi kwa sasa, na itafikia mahali tutaagiza ng'ombe wa kuchinja kutoka kenya na kwingineko tena kwa bei ya juu sana,

  Hapo nashindwa kuelewa lengo la huyo mgugaji lilikuwa lipi, kufuga na kuuza na kujenga gest?

  Moja ya Biashara ambazo zinaweza kututoa watanzania ni

  1. Ufugaji

  2. Kilimo

  3. Uvuvi

  4. Utalii kwa kiasi fulani

  6. Viwanda

  7. Madini kama yatasimamiwa vyema,

  Nchi zote zilizo endelea duniani zimeendelea kwa sababu ya vitu hivyo hapo juu mkuu,

  Mkuu najua kuna watu watanipinga sana hapa but biashara zifuatazo haziwezi kututoa watanzania kabisa, na mwenye nchi iliyotoka kwa hizi biashara atujuze,

  1. Kujenga gest

  2. Mabaa

  3. Uchuuzi wa bidhaa mbalimbali

  Na zingine nyingi, kwanza hizo biashara haziajiri watu wengi ukilinganisha na viwanda na vile vile kufanya biashara za Uchuuzi tunajenga uchumi wa china huku tukijidanganya uchumi wetu unakua, Uchumi wetu utakua vipi kwa kuuza bidhaa za china? Nenda china uone bidhaa wanazo uza wao,

  Na katika biashara zinazo vutia Investers wengi sana hizo za uchuuzi hazimo kabisa, na jaribu hata kutafuta watu wakufanya nao biashara halafu uwaambie unataka kufungua duka la kuuza sijui redio, hupati mtu labuda watanzani wenzetu ila kwa wawekezaji wa nje hupati mtu,

  Na hatujajiuliza kwa nini wawekezaji kutoka nje wengi wao wanakimbilia sekata za
  1. Viwanda
  2. Madini
  3.Kilimo
  4. Utalii
  5. Ufugaji

  HUYO MZEE ANGEFANYA HIVI

  1. Angeuza part ya ngome wake na kuwekeza katika ufugaji wa kisasa ikiwemo kununua alidh ya kutosha na kufungua Ranchi yake mwenyewe hapo angefuga kisasa na kuweza hata kuuza nje ng'ombe wake hao na angeweza hata kuwa na kiwanda chake cha ku process Nyama pamoja na mazao mengine yatokanayo na Ng,ombe,

  Ng'ombe 250 ni kitu gani? Nenda kwenye Runchi za huk zimbabwe uone kiasi cha ng'ome wanacho fuga huko au zile Runch za kule Argentina,

  MIMI SI MUUNGI MKONO HUYO MZEE NA NI SAWA NA KUUZA BUNDUKI HALAFU UNUNUE RUNGU


  1. A
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Wengine wanasubiri ng'ombe wao wafe kwa ukame na njaa.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Mkuu Komando nakubaliana na wewe kwa asilimia nyingi. Tatizo watendaji wetu ni wanasiasa zaidi, hata huyo afisa mifugo hajui ufugaji na tija zake ninini, anabaki kutekeleza matakwa ya wanasiasa. Ng'ombe mia saba kwa ufugaji wa kienyeji ni kazi kubwa sana kufikia idadi hiyo ya wanyama, hiyo inaonesha ni jinsi gani huyo mzee anakipaji cha ufugaji, na huo ulikuwa ni mtaji wake wa kujiwezesha kuwa mfugaji bora kwa kufuga kwa mfumo rasmi wa kitaalam; lakini kama bwana shamba anayetakiwa amshauri ufugaji bora anamshauri kupunguza idadi ya mifugo basi kuna matatizo hata kwenye mfumo wetu wa elimu. Tunatakiwa kuzalisha kwa wingi na kwa ubora madhubuti, mahitaji ya nyama yanaongezeka siku hadi siku, kama wafugaji wakipewa elimu stahiki basi wanaweza kabisa kuwa wafugaji wakubwa wenye mchango mkubwa kwa Taifa kuliko hizo Guest House za kizinzi wanazoshauriw akujenga. Bado hatuna wataalam.
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tatizo ni kwua serikali inalichukulia suala la kupunguza mifugo kisiasa zaidi. Mbali ya kumsikia rais Kikwete akilisema hili kwenye hotuba zake za kisiasa, sijasikia programu yoyote iliyoandaliwa na wizara husika kuhusiana na utekelezajiw a azma hiyo
   
 6. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mkuu KOMANDO na Amoeba, kweli mnena pointi kabisa. Tunahitaji ufugaji wenye tija, huku tukikabiliana na changamoto zake si kwa kuzikimbia kwa kupunguza idadi ya ng'ombe ila kwa kubadili mbinu za kufuga. Hii ya kuuza na kujenga Guest House ili uhamasishe uzinzi haiji akilini!!
  Anyway, labda Afisa Mifugo aliona hicho pekee ndicho kingeweza kumbadili huyu mfugaji na kuweza kumuokoa asipoteze uchumi wake wote siku moja. Pamoja na kutoweka siasa kila sehemu, tunahitaji kuumiza vichwa kwa kutatua matatizo yetu wenyewe siyo kuyakimbia kama ilivyosasa ambapo kila kitu tunakimbilia mgeni aje atusaidie.
   
 7. matwi

  matwi JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Sep 2, 2009
  Messages: 276
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tatizo letu tunaweka siasa katika kila kitu.yani maneno ni mengi kuliko vitendo.
  Huyu sio mfugaji wa kwanza kuuza mifugo na kujenga nyumba za kisasa,kuna wafugaji wengi tu waliojenga nyumba za biashara Morogoro mjini na bado wanaendelea na ufugaji.
  Tatizo linalowafanya wafugaji wengi kubaki na mifugo yao ni kukosa soko la uhakika na bei shahili.huwezi mwambia leo mfugaji auze ng'ombe wake kwa bei ya laki 3, wakati anajua akija mjini nyama kilo ni sh 6000.Bado akitaka kwenda uza nchi ya jirani anakutana na vikwazo vingi kiasi kwamba hata akienda uza hela yaishia kwenye makato ya ushuru.

  Cha muhimu ni serikali kuchukulia hili suala serious kwa kufufua viwanda vya usindikaji na kusambaza mizani kwa minada ya mifugo nchi nzima hii itasaidia kuongeza demand na wafugaji kuuza mifugo yao kwa bei stahiki.
   
Loading...