Mtangazaji mkongwe wa DW Kiswahili astaafu.

Mwendo Kasii

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
203
Reaction score
213
Mtangazaji nguli na mashuhuri katika tasnia ya habari Abdul Mtullya amestaafu utangazaji rasmi kutokana na ukomo wa umri wa kustaafu.

Aliajiriwa radio Tanzania mwaka 1972 na kufanya kazi hapo miaka sita na kisha kwenda ujerumani kujiunga na iliyokuwa ikijulikana kama Idhaa ya kiswahili ya redio Berlin kabla ujerumani haijaungana na kuwa nchi moja na kufanya kazi katika idhaa hiyo kwa takribani miaka 11. baada ya ujerumani kuungana(Cold War Period miaka hiyo ya ) ndipo alijiunga katika shirika la utangazaji la Ujerumani ( Dewtsche Welle) katika idhaa ya kiswahili( DW Kiswahili). Wengi tunakumbuka katika kipindi chake cah "Umeipata Hiyo?" katika idhaa ya DW. Amerejea tanzania kuendelea na shughuli zingine kama za uandishi wa vitabu.
upload_2016-9-10_17-7-29.jpeg

Timu ya Idhaa ya Kiswahili

Kutoka kushoto: Mohammed Khelef, Mohamed Dahman, Oummilkheir Hamidou, Elizabeth Shoo, Nyamiti Kayora, Abdul Mtullya, Nina Markgraf, Grace Kabogo, Daniel Gakuba, Amina Abubakar, Mohamed Abdul-Rahman, Zuhura Hussein, Batoul Kidadi, Saumu Mwasimba, Iddi Ssessanga, Samia Othman, Sudi Mnette, na Andrea Schmidt.

N.B: Saumu Mwasimba kwa sasa yupo BBC Swahili.
 
Sauti ya America na idhaa ya sauti ya ujerumani zipo sana taabani wanachokosea wanaondokewa na watangazaji wazuri wanaleta chini ya viwango.mnamkumbuka Jerome danford kazembe
 
Mtangazaji nguli na mashuhuri katika tasnia ya habari Abdul Mtullya amestaafu utangazaji rasmi kutokana na ukomo wa umri wa kustaafu.

Aliajiriwa radio Tanzania mwaka 1972 na kufanya kazi hapo miaka sita na kisha kwenda ujerumani kujiunga na iliyokuwa ikijulikana kama Idhaa ya kiswahili ya redio Berlin kabla ujerumani haijaungana na kuwa nchi moja na kufanya kazi katika idhaa hiyo kwa takribani miaka 11. baada ya ujerumani kuungana(Cold War Period miaka hiyo ya ) ndipo alijiunga katika shirika la utangazaji la Ujerumani ( Dewtsche Welle) katika idhaa ya kiswahili( DW Kiswahili). Wengi tunakumbuka katika kipindi chake cah "Umeipata Hiyo?" katika idhaa ya DW. Amerejea tanzania kuendelea na shughuli zingine kama za uandishi wa vitabu.
View attachment 397698
Timu ya Idhaa ya Kiswahili

Kutoka kushoto: Mohammed Khelef, Mohamed Dahman, Oummilkheir Hamidou, Elizabeth Shoo, Nyamiti Kayora, Abdul Mtullya, Nina Markgraf, Grace Kabogo, Daniel Gakuba, Amina Abubakar, Mohamed Abdul-Rahman, Zuhura Hussein, Batoul Kidadi, Saumu Mwasimba, Iddi Ssessanga, Samia Othman, Sudi Mnette, na Andrea Schmidt.

N.B: Saumu Mwasimba kwa sasa yupo BBC Swahili.
Binafsi nampenda sana oummilkheir basi akiwa anasoma taarifa utasikia mjiiini booooooorn..nimtakie Kila la heri bwana Abdul mtullya. Karibu nyumbani
 
Othman Miraji, Wsjir Sheikh, Oummilkheir na Abdul Mtullya ni miongoni mwa watangazaji wa DW Swahili waliokua wakinivutia sana, hapo sijaongelea Ramadhan Ali, huyu walikua maarufu kipindi cha michezo.
 
Karibu nyumbani mzee mtullya, huku tuko bize kufyatua watoto, we tafuta mwenzako muanze kufyatuana
 
Hongera kwa kupiga kazi kwa miaka mingi.

Vipindi vyako utotoni nilikuwa navipenda sana miaka hiyo hakuna radio za FM.
 
OUMMILKHEIR..navutiwa nae...hivi ni mwanamama au ni Mwanaume.. sauti yake tamu
 
ivi kwanini watangazaji wengi wa izi idhaa ni waislamu
Nijuavyo mimi:
Utamkaji wao wa maneno ya kiswahili ni fasaha sana kutokana na malezi ya madrasa. kwani wengi wao ni wa mikoa ya pwani ambako waarabu waliishi sana, na tujuavyo kuwa kiswahili kimekopa maneno mengi kutoka lugha ya kiarabu.
 
Back
Top Bottom