Mtandao wa Smile watuweke wazi kama wamefilisika ili tutafute namna nyingine kuwafikia ndugu zetu

Alfris

New Member
Aug 18, 2019
4
6
JF, tunaomba mtusaidie kuwauliza wamiliki wantandao wa Smile, kuna tatizo gani ambalo halitatuliki? Ni zaidi ya miezi mitatu sasa huduma hazipatikani kwa tuliopo nje ya Tanzania.

Tumewauliza mara kadhaa kwa email, wanadai kuna tatizo la kiufundi.
Siyo kawaida tatizo kudumu miezi.

Tunaomba watuweke wazi kama ni kufilisika, ili tutafute namna nyingine kuwafikia ndugu zetu waliopo mbali nasi.
 
Nilikuwa mteja wa Smile, wako hoi bin taabani. Nilijitoa baada ya kunitapeli elfu 65 halafu wakadai ni upgrade personal info.
Mitambo yao ikashindwa kuganya kazi.
 
Back
Top Bottom