Mtandao wa simu wa SMART ni watapeli wakubwa

Mtandao wa simu wa SMART ni watapeli wakubwa

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
5,093
Reaction score
11,948
Hii mitandao ya simu inayokuja sasa si ya kurukia. SMART siku ya kwanza tu kujiunga kwa sababu hawatumii scrach card ilibidi nimpe alieniunganisha elfu kumi anijazie muda wa maongezi, huyo jamaa akaweka elfu nane na akagoma kabisa kulipa elfu mbili mpaka nikanfikisha kwa bosi wake ndo akatuma hiyo fedha ikifuatiwa na kuondoka gafla sh elfu nane.

Leo nimeweka elfu tano kutaka kununua kifurushi ikashindikana kuwa salio halitoshi. Nilipowapigia wakaahidi kuwa anashughulikia na atanipigia, kumbe ndo nikawa nimentuma aendelee kuzifyeka na amefyeka karibu elfu mbili. Najaribu kuwapigia hawapokei simu.

Hivi huu ni mtandao wa kigogo gani?
 
hamia mitandao mingine. au kafungue kesi ya madai polisi.
 
Hii mitandao ya simu inayokuja sasa si ya kurukia. SMART siku ya kwanza tu kujiunga kwa sababu hawatumii scrach card ilibidi nimpe alieniunganisha elfu kumi anijazie muda wa maongezi ,huyo jamaa akaweka elfu nane na akagoma kabisa kulipa elfu mbili mpaka nikanfikisha kwa bosi wake ndo akatuma hiyo fedha ikifuatiwa na kuondoka gafla sh elfu nane. Leo nimeweka elfu tano kutaka kununua kifurushi ikashindikana kuwa salio halitoshi. Nilipowapigia wakahaidi kuwa anashugulikia na atanipigia, kumbe ndo nikawa nimentuma aendelee kuzifyeka na amefyeka karibu elfu mbili. Najaribu kuwapigia hawapokei simu. Hivi huu ni mtandao wa kigogo gani.

aga khan foundation
 
Hivi siwezi kubadilisha kile kidude cha smile nitumie mitandao ingine??
 
Hii mitandao ya simu inayokuja sasa si ya kurukia. SMART siku ya kwanza tu kujiunga kwa sababu hawatumii scrach card ilibidi nimpe alieniunganisha elfu kumi anijazie muda wa maongezi ,huyo jamaa akaweka elfu nane na akagoma kabisa kulipa elfu mbili mpaka nikanfikisha kwa bosi wake ndo akatuma hiyo fedha ikifuatiwa na kuondoka gafla sh elfu nane. Leo nimeweka elfu tano kutaka kununua kifurushi ikashindikana kuwa salio halitoshi. Nilipowapigia wakahaidi kuwa anashugulikia na atanipigia, kumbe ndo nikawa nimentuma aendelee kuzifyeka na amefyeka karibu elfu mbili. Najaribu kuwapigia hawapokei simu. Hivi huu ni mtandao wa kigogo gani.
Tumesikia upande mmoja(mtumiaji wa SMART),tungependa pia kusikia upande wa pili yaani SMART. Hii ni business lazima sisi watumiaji tupate taarifa kamili kabla ya kufanya maamuzi,
 
Tumesikia upande mmoja(mtumiaji wa SMART),tungependa pia kusikia upande wa pili yaani SMART. Hii ni business lazima sisi watumiaji tupate taarifa kamili kabla ya kufanya maamuzi,

Ni kweli hebu SMART jitokezeni mtwambie je, hayo ndiyo mmemfanyia mteja mwenzetu? inafahamika wazi kuwa mwenzako akinyolewa wewe tia maji, kwahiyo njooni mjibu tuhuma hapa, mkinyamaza tutaamini kuwa ninyi nanyi ni walewale!!! fanyeni fasta kabla hatujaanza kuwakimbia maana sisi kwetu kuhamahama mitandao imeshakuwa sehemu ya uhai wetu
 
Ni kweli niko tayari kutoa maelezo zaidu na namba za simu zao za binafsi ambazo huwa natumia kulalamika.
 
Hii Tanzania bwana!

Kila mtu anafanya analoona ni bora kwake kufanyika...

Mitandao ya simu inasumbua,

Raia wa nchi nyingine mpaka makomandoo nao wanakuja tu na kuishi bila bughudha wala kufuatiliwa,

Ajira watu wanapeana wao kwa wao kama vile wao tu ndiyo wamesoma na wana sifa,

Katiba imekuwa dili, mpaka sasa wameshalamba mamilioni ya TAS huku waalimu wakilamba chaki kila siku..!

Ukijitoa kuwa msamaria mwema na kuripoti uhalifu, basi wewe unakuwa sample...

(napita jamani...)
 
Kwa taarifa tu ni kuwa hakuna mtandao wenye gharama kubwa TANANIA NZIMA kama SMART.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom