Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Taarifa rasmi ninayoleta kwenu ni kwamba ule mtandao wa vijana ambao walijikusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya nchi hususan kwenye vyuo wakimuunga mkono aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa umevunjika rasmi.
Taarifa za kuvunjika kwa mtandao huo ambazo nimezipata hivi punde kutoka kwa mmoja wa viongozi wa umoja huo zimekuja baada ya kukatika kwa mawasiliano baina ya Edward Lowassa na viongozi wa mtandao huo. Kwamba, tangu Novemba 2015, hakuna mawasiliano yoyote baina ya pande mbili hizo.
Pia kiongozi huyo amenidokeza kuwa, 4u Movement walikuwa wanakabiliwa na matatizo makubwa ya kifedha na kwamba tangu Septemba 2015, hali ya kifedha ilikuwa ngumu sana. Mathalan, amesema kuwa viongozi wa umoja huo walikuwa wanalipwa posho ya wastani wa shilingi 650,000 kwa mwezi.
Hata hivyo, anasema kuwa hawajalipwa posho hiyo kwa zaidi ya miezi minne sasa. Pia anasema kuwa waliahidiwa kulipiwa kodi ya ofisi kuanzia mwezi Januari 2016 baada ya kodi yao kwisha Desemba 2015.
Hata hivyo, mpaka leo amesema kuwa hawajapata fedha hizo na hawana uhakika wa kuzipata na kwamba wenye majengo wameamua kusitisha mikataba yao na hivyo kuwaamuru kuondoa vifaaa vyao ili wawapangishe wateja wengine.

Last edited by a moderator: