Mtandao wa IKULU waendelea kuitangaza CCM!

Mtandao wa IKULU waendelea kuitangaza CCM!

..wiki chache zilizopita tulitoa tahadhari kuhusu taarifa za vikao na mikutano ya CCM kuwekwa ktk mtandao wa ikulu. ilikuwa faraja kubwa kuona kwamba wahusika walifanya marekebisho ya haraka kuondoa tatizo hilo.

..lakini kitu cha kushangaza ni kwamba wiki hii tena hali hiyo imejirudia tena. mtandao wa ikulu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Tovuti Rasmi ya Ikulu umeweka picha za vikao vya CCM pamoja na picha za mkutano wa kichama ambao unamhusisha mgombea Uraisi kupitia CCM Dr.Magufuli.

..mimi nadhani hii ni kasoro kwasababu taarifa za shughuli za vyama vya siasa hazipaswi kuwekwa ktk mtandao wa kiserikali ambao ni wetu wa-Tanzania wote.

..nawaomba wana-JF wenzangu ambao mnapenda haki na usawa hapa nchini muwatafute wahusika wa ikulu na tcra ili hali hii ya upendeleo wa waziwazi kwa CCM isitishwe.

..anwani za wahusika zinapatikana ktk mtandao wa ikulu nazo ni hizi hapa:

Ofisi ya Rais Ikulu,1Barabara ya Barack Obama,11400 Dar es salaam

Simu : 0222116898Simu : 0222116900/6

Nukushi: 0222113425/2116910/2117272

Barua pepe : ikulu@ikulu.go.tz

..anwani za ofisi ya katibu kiongozi ambazo ziko kwenye mtandao wa ikulu ni hizi hapa:

Ofisi ya Rais Ikulu,1 Barabara ya Barack Obama,11400 Dar es Salaam.

Simu : 0222116898

Simu : 02222116900/6

Barua pepe : Tovuti : chiefsecretary.go.tz


..anwani za tume ya taifa ya mawasiliano zinazopatikana kwenye mtandao ni hizi hapa:

The Director General

Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA)
Mawasiliano Towers
20 Sam Nujoma Road
P.O Box 474
14414 Dar Es Salaam
Tel: +255 22 2199760 - 8; +255 22 2412011 - 2
Mob: +255 784558270 - 1
Director General Direct Line +255 22 2199769
Fax: +255 22 2412009 / +255 22 2412010

E-Mail: dg@tcra.go.tz

NB:

..nadhani suala hili linapaswa kupelekwa hata kwenye ofisi za Tume ya Uchaguzi, pamoja na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa.








Kwani majadiliano ya ccm yanakusu nini? Kama hutaki kuyasoma nani anakulazmisha na yana madhara gani kwenye tovuti ya iku lu? Fahamu kwamba baba mwenye nyumba pia ni mwenyekiti wa ccm na anataka kusoma mambo ya nchi bila kuhama tovuti!
 
Nadhani kuna watu hawajaelewa hoja. Tovuti ya ikulu inatakiwa Mambo ya ikulu tu hasa shughuli za Rais. Ndo hoja ya mtoa hoja na ndivyo inavyotakiwa. Sasa ukisema inamhusu nini au kwamba Rais ni mwana ccm kwahiyo ni sawa kuweka habari za chama ni kukusa uelewa. Je kama wewe ni mkurugenzi wa ofisi ya umma habari za mtoto wako kuchagua kuingia kidato cha tano kiwekwe kwenye tovuti ya shirika la umma? Mtu kama hujaelewa hoja siyo Lazima utoe maoni na usiingize ushabiki au upenzi wa chama chako bali tuwe na upeo mpana wa kitaifa.
 
ila wadau mimi napingana kabisa na hili la barabara ya ikulu kupewa jina la Obama. nadhani angepewa hata barabara ya huko mburahati. nadhani barabara ya ikulu ingemfaa sana nyerere kama muasisi wa taifa hili au hata akina chief mkwawa, hasan makunganya, isike na wazalendo wengine walioliifia taifa hili. hivi hakuna uwezekano rais ajaye akabadilisha hilo jina? nauliza.

Jina hilo ni muhimu kwani tezi dume limetolewa ardhini kwake kwa heshima zote
 
Jina hilo ni muhimu kwani tezi dume limetolewa ardhini kwake kwa heshima zote
mkuu umeelewa swali langu? au na wewe nyumbu? swali ni hili, labda usome tena
quote_icon.png
By Abunuas

ila wadau mimi napingana kabisa na hili la barabara ya ikulu kupewa jina la Obama. nadhani angepewa hata barabara ya huko mburahati. nadhani barabara ya ikulu ingemfaa sana nyerere kama muasisi wa taifa hili au hata akina chief mkwawa, hasan makunganya, isike na wazalendo wengine walioliifia taifa hili. hivi hakuna uwezekano rais ajaye akabadilisha hilo jina? nauliza.
 
mkuu umeelewa swali langu? au na wewe nyumbu? swali ni hili, labda usome tena
quote_icon.png
By Abunuas

ila wadau mimi napingana kabisa na hili la barabara ya ikulu kupewa jina la Obama. nadhani angepewa hata barabara ya huko mburahati. nadhani barabara ya ikulu ingemfaa sana nyerere kama muasisi wa taifa hili au hata akina chief mkwawa, hasan makunganya, isike na wazalendo wengine walioliifia taifa hili. hivi hakuna uwezekano rais ajaye akabadilisha hilo jina? nauliza.


Mkuu, po nakubali mimi nyumbu nijuvyo mimi rais hhusiki na kutoa majina ya barabara. Sio kazi zake. Kuna watu wanaohusika na suala hilo na kwa hiyo uelekeze kwa watu hao hoja yako. Asilauiwe Rais wa jans, sasa na hata wa kesho.
 
Back
Top Bottom