Mtandao wa Habarileo kuzuia taafifa zake zisikopiwe hii imekaaje?

JacksonMichael

JF-Expert Member
Mar 22, 2012
339
61
Ngugu wanaJF,

Mtandao wa gazeti tajwa hapo juu limezuia habari zake zikikopiwe, hii imekaaje? mbona mitandano ya magazeti yote hapa nchini na sememu nyingi katika dunia hii hawana sheria za ajabu kama hizi? hali kama hii nimeiona katika mitandao inayouza vitabu na majarida ambayo kwa kuwa lengo lao ni uuzaji ni fine lakini kwa gazeti letu la kiserikali naona haijatulia.

Nafikili bado wananchi wanahaki ya kutumia taarifa zile cha msingi waacknowledge source ya habari na wasibadili contents husika. Wadau tujadili hili gazeti la ccm naona linatupeleka pasipo kwa ubinafsi huu.
 
Wadhaifu hao achana nao, source mbona kibao mkuu, kijarida hicho cha udaku...
 
ngugu wanajf,

mtandao wa gazeti tajwa hapo juu limezuia habari zake zikikopiwe, hii imekaaje? Mbona mitandano ya magazeti yote hapa nchini na sememu nyingi katika dunia hii hawana sheria za ajabu kama hizi? Hali kama hii nimeiona katika mitandao inayouza vitabu na majarida ambayo kwa kuwa lengo lao ni uuzaji ni fine lakini kwa gazeti letu la kiserikali naona haijatulia.

Nafikili bado wananchi wanahaki ya kutumia taarifa zile cha msingi waacknowledge source ya habari na wasibadili contents husika. Wadau tujadili hili gazeti la ccm naona linatupeleka pasipo kwa ubinafsi huu.

duhu. Mkuu kama umesoma education ni vigumu kujua
 
LAzima ulitaka kucopy ile ya viongozi wa dini na ningefurahi kama ungeicopy habari nzima ...
 
Wewe si ni kilaza mmoja wapo DHAIFU toka magamba!!

Ulikuwa hufahamu kuwa magazeti yote ya Serikali sasa hivi huruhusiwi kucopy??

BTW, habari zao ni za uzushi na dhaifu sana na zina dhima za kimasaburi bora wabaki nazo wenyewe!!
 
Kila kitu unaweza ku-copy Mkuu.
Kama ni hiyo stori ulikuwa unaitafuta hiyo hapo.....nilitaka kukuhakikishia kuwa wameweka hizo features but U can go around it.


Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ), Mansour Yussuf HimidWaziri asiyekuwa na Wizara Maalumu wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Mansour Yussuf Himid


SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
kutangaza kukaribisha maoni yote kuhusu Muungano, yakiwemo ya kuuvunja,
Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
(SMZ), Mansour Yussuf Himid ametangaza kuvutiwa na misimamo ya Jumuiya
ya Mihadhara ya Uamsho kuhusu Muungano.


Katika tamko hilo, ameweka wazi kuwa anapendezwa na misimamo hiyo
aliyoiita yenye malengo ya kutetea maslahi ya Wazanzibari katika
Muungano na kutaka Wazanzibari waachiwe wapumue bila kufafanua dhana
hiyo ya kuachiwa wapumue.


Waziri Mansour ambaye ni Mwakilishi Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM,
alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia Bajeti ya SMZ kwa mwaka wa
fedha 2012-2013 katika Baraza la Wawakilishi.


Mbali na kuwa mwakilishi kwa tiketi ya CCM, ambayo imeweka wazi kuwa
itatetea kuwepo kwa muundo wa Muungano wa serikali mbili, Mansour pia ni
mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho na Katibu wa Idara ya Uchumi na
Fedha ya Chama hicho, Zanzibar.


Pamoja na kutofafanua dhana ya Wazanzibari waachiwe wapumue, Mansour
alisema anakubaliana na mikakati na misimamo ya jumuiya hiyo yenye
malengo ya kuwepo kwa Muungano utakaokuwa na maslahi kwa upande wa
Zanzibar ingawa hakubaliani na vurugu zinazohamasishwa na viongozi hao.


“Mimi msimamo wangu unafahamika wazi wazi katika Muungano...ni kuwepo
Muungano wenye maslahi kwa wananchi wa Zanzibar. Ingawa sio mfuasi wa
Uamsho lakini nakubaliana na misimamo yao yenye malengo ya kuwepo kwa
Muungano utakaojali maslahi ya Wazanzibari na kutaka Wazanzibari
tuachiwe tupumuwe,” alisema.


Alisema wananchi wa Zanzibar wanataka Muungano, lakini kutokana na
muundo wa Muungano uliopo sasa wamekuwa na mawazo mbalimbali kwamba
umekuwa ukiwanyonya na kurudisha nyuma mipango ya maendeleo.


Alitoa mfano wa muundo uliopo sasa wa Muungano wa serikali mbili, ambao
ndio msimamo wa CCM, akasema wananchi mbali mbali wamekuwa hawaridhiki
nao huku ukiwa hauna tija kwa Wazanzibari.


Aonya Polisi Aidha Mansour alionya vitendo vya Dola kutumia nguvu kwa
watu wenye mawazo tofauti kuhusu Muungano ikiwemo wale wanaopinga
Muungano na kutaka uvunjike na kusema kufanya hivyo ni kwenda kinyume na
demokrasia na uhuru wa wananchi kutoa maoni yao na kujieleza.


Alisema kinachotakiwa kufanywa ni kuwashawishi watu ambao hawataki
Muungano kwa kuwaelimisha na kuwatajia mazuri yatakayopatikana katika
Muungano wa pande mbili na athari zitakazopatikana kama Muungano utavunjika.


“Naomba vyombo vya Dola viache kutumia nguvu kwa watu wanaoukataa
Muungano...tunachotakiwa kufanya ni kuwashawishi wale watu wanaokataa
Muungano kwa kujenga hoja ya faida za Muungano na athari kama
ukivunjika,” alisema Mansour.


Awali Mansour aliwataka wananchi mbalimbali wa Zanzibar kujitokeza kwa
wingi kutumia nafasi yao ya demokrasia kutoa maoni kuhusu muundo wa
Muungano wanaoona unafaa kwa sasa wakati wa kutoa maoni kuhusu Katiba
mpya ya Jamhuri ya Muungano.


Alisema hiyo ndiyo fursa muhimu na pekee iliyopo sasa ambayo kama
wananchi wataitumia vizuri, basi watatua matatizo mbalimbali yaliyomo
katika Katiba ikiwemo mambo ya Muungano.


“Hii ndiyo fursa muhimu na pekee iliyopo sasa kwa wananchi kutoa maoni
yao kuhusu muundo gani wa Muungano wanataka,” alisema.


Mwakilishi wa Magomeni, Salmin Awadh (CCM), alisema wakati umefika kwa
wananchi wa Zanzibar kutoa maoni yao kuhusu muundo wa Katiba ikiwemo
muundo wa Muungano.


“Wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kutoa maoni yao kuhusu muundo
wa Muungano pamoja na marekebisho ya Katiba...hiyo ndiyo fursa pekee ya
kikatiba iliyopo kwa sasa,” alisema.


Mjadala wa kujadili Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2012- 2013
umetawaliwa na mambo ya Muungano huku wajumbe wakitaka kujua haki za
Zanzibar zilizopo katika Muungano.


Muundo wa Muungano umekuwa ukiamsha mjadala mkubwa ambapo kwa Zanzibar,
CCM imekuwa ikitetea msimamo wa kuwa na muundo wa serikali mbili; wakati
CUF, ikisisitiza muundo wa serikali tatu.
 
Back
Top Bottom