Mtanda fuatilia kwa karibu mradi wa jengo la uwanja wa ndege la kimataifa Mwanza, limesimama tena

tripof

JF-Expert Member
Apr 2, 2024
280
355
Wananchi wa Mwanza tumekuwa tukifuatilia kwa karibu ujenzi wa jengo la abiria la uwanja wa ndege la Mwanza linalotarajiwa kuufanya uwanja huu kuwa wa kimataifa.

Aliyekuwa RC wa Mwanza Makalla alijitahidi sana kuurejesha kwenye uhai lakini kampuni ya Mzawa haionekani kufanya chochote hadi sasa site kulikoni? kimya kabisa.

Aidha, kuna ahadi ya kujenga njia 4 barabara za Kenyata na Nyerere kuingia/kutoka jijini ahadi ya muda mrefu tunataka kuona vitendo na matokeo, wizara ya uchukuzi na pia ujenzi si jui wanatuonaje kanda hii.

Tunaangalia utakavyoisaidia Mwanza na Kanda ya Ziwa kukamilisha miradi. Tunakutakia kazi njema na uongozi uliotukuka kwenye mkoa huu ili uache alama
 
Waziri Mbarawa na ile kampuni ya ujenzi ya Rostam wote ni wahuni sana...ok ila mwaka huu watajenga huo uwanja na hizo barabara siunajua tunaenda kwenye uchaguzi.
 
Wananchi wa Mwanza tumekuwa tukifuatilia kwa karibu ujenzi wa jengo la abiria la uwanja wa ndege la Mwanza linalotarajiwa kuufanya uwanja huu kuwa wa kimataifa.

Aliyekuwa RC wa Mwanza Makalla alijitahidi sana kuurejesha kwenye uhai lakini kampuni ya Mzawa haionekani kufanya chochote hadi sasa site kulikoni? kimya kabisa.

Aidha, kuna ahadi ya kujenga njia 4 barabara za Kenyata na Nyerere kuingia/kutoka jijini ahadi ya muda mrefu tunataka kuona vitendo na matokeo, wizara ya uchukuzi na pia ujenzi si jui wanatuonaje kanda hii.

Tunaangalia utakavyoisaidia Mwanza na Kanda ya Ziwa kukamilisha miradi. Tunakutakia kazi njema na uongozi uliotukuka kwenye mkoa huu ili uache alama
Mwanza haina sababu nzuri ya kuwa na international airport.
 
Sababu nzuri ni zipi mkuu 'fazili'?
Itakuwa vizuri sana ukitueleza hilo, na mjadala mpana tutauanzisha hapa kuhusu hizo hoja zako.

Haitoshi kusema tu "Mwanza haina sababu nzuri ya kuwa na international airport," na kuishia hapo!

Sababu unazoziona wewe kuwa "nzuri" zinaweza kuwa mbovu kabisa kwa wengine. Pengine hata hujui maana ya "International Airport" huijui!
 
Mimi ninazo sababu za Mwanza kuwa na international airport km ifuatavyo:
1. ni jiji la pili Tanzania kiuchumi kwa Dar
2. jiji hili liko kimkakati "strategic" kwenye ukanda wa nchi za Maziwa Makuu,Kenya,Uganda,Rwanda, Burundi,DRC, kibiashara.Wageni kutoka nchi hizo wana option ya kusafiri kwa gari tu kuifikia Mwanza,hii husababisha usumbufu na haiendani na protokali za EAC
3.Ni mwisho na kituo kikuu cha SGR, ina Bandari kubwa kavu na Majini kanda ya ziwa Makuu ndani ya ziwa viktoria
4.Hakuna uwanja wa ndege kimataifa kanda ya ziwa na magharibi,mazao ya samaki na nyama husafirishwa kupitia kenya na uganda na hivyo kunufaisha nchi hizo kiuchumi kwa mgongo wa Tanzania
5 Kiutalii Iko karibu na mbuga za Serengeti, Burigi Chatto na Rumanyika, uwepo wa uwanja wa ndege wa kimataifa utanufaisha nchi yetu kimapato.
6.uchumi wa kanda ya ziwa ni mkubwa abiria 400,000 kwa mwaka, kuna madini,kilimo,uvuvi,mifugoetc husafirishwa kupitia Nairobi au JNIA gharama kubwa za uzalishaji ns usafirishaji kwa mwekezaji
7.Uwanja huu unatumika na abiria wengi ni namba nne kwa JNIA,KIA na ZNZ airprt.ATCL inapeleka ndege mara 4- 5 inahudumia abiria wengi kuliko jiji lingine ukiacha dar nchini. Umbali na viwanja vya JNIA na KIA ki logistic kunaifanya Mwanza ihitaji uwanja wa kimataifa,idadi ya watu nk
8. Angalau kuna miundo mbinu inayokubalika ya kuanziana ICAO na IATA Km Rada,control tower ya kisasa na barabara njia 4 kuingia uwanjani upungufu mkubwa uiopo ni jengo la abiria na mizigo, upanuzi wa njia ya kurukia ndege na taxi parking,hotel etc
9.Ilani ya uchaguzi ya ccm 2020 inaitaka serikali kujenga uwanja wenye hadhi ya kimataifa Mwanza. Ni kipaumbele cha kitaifa
jesababu hizi zote unazionaje hazitoshi kuufanya uwe wa kimataifa.
 
Wakipitia Arusha ndio kila kitu kwanza wanaanza na:
My Kilimanjaro, then
Arusha national park
Tarangire
Manyara
Ngorongoro halafu ndio
Serengeti
Arusha pamekaa kistratejia zaidi
AHaa. Kumbe unasukumwa na maslahi na siyo sababu za sifa za kuwa na uwanja wa kimataifa wa ndege?
Ni mtalii gani anakuja Tanzania na lengo la kutembelea maeneo hayo pekee uliyoyataja wewe? Unataka vivutio viwe sehemu moja tu ya nchi; kwa nini?

Inajulikana toka zamani, maslahi ya watu wenye mawazo kama yako ndio miaka yote wamekuwa wakiukwamisha huu uwanja wa Mwanza usipewe hadhi inayoistahili. Huu ni ubinafsi usiohitajika ndani ya nchi hii. Maendeleo ya nchi ni kwa watu wote, siyo eneo fulani pekee.
 
Wananchi wa Mwanza tumekuwa tukifuatilia kwa karibu ujenzi wa jengo la abiria la uwanja wa ndege la Mwanza linalotarajiwa kuufanya uwanja huu kuwa wa kimataifa.

Aliyekuwa RC wa Mwanza Makalla alijitahidi sana kuurejesha kwenye uhai lakini kampuni ya Mzawa haionekani kufanya chochote hadi sasa site kulikoni? kimya kabisa.

Aidha, kuna ahadi ya kujenga njia 4 barabara za Kenyata na Nyerere kuingia/kutoka jijini ahadi ya muda mrefu tunataka kuona vitendo na matokeo, wizara ya uchukuzi na pia ujenzi si jui wanatuonaje kanda hii.

Tunaangalia utakavyoisaidia Mwanza na Kanda ya Ziwa kukamilisha miradi. Tunakutakia kazi njema na uongozi uliotukuka kwenye mkoa huu ili uache alama
Umeangalia mkataba wa ujenzi inasemaje? Au umekimbilia kwa Mtanda bila kusema kama kuna sehemu ametajwa ndani ya mkataba? Watu kama nyie ndo wanasababisha kuaribika kwa kazi.
 
AHaa. Kumbe unasukumwa na maslahi na siyo sababu za sifa za kuwa na uwanja wa kimataifa wa ndege?
Ni mtalii gani anakuja Tanzania na lengo la kutembelea maeneo hayo pekee uliyoyataja wewe? Unataka vivutio viwe sehemu moja tu ya nchi; kwa nini?
Inajulikana toka zamani, maslahi ya watu wenye mawazo kama yako ndio miaka yote wamekuwa wakiukwamisha huu uwanja wa Mwanza usipewe hadhi inayoistahili. Huu ni ubinafsi usiohitajika ndani ya nchi hii. Maendeleo ya nchi ni kwa watu wote, siyo eneo fulani pekee.
Sawa ila lazima uangalie ukaribu na vivutio hivyo na vipo vingi sehemu gani. Huwezi kujenga tourist hub Kigoma ambapo vivutio vya utalii ni vichache ukaacha kujenga hub hiyo mahali kama Arusha ambapo vivitio hivyo vimelundikana. Mwanza ukiacha Ziwa Victoria kuna national parks ngapi ukilinganishwa na ukanda wa Kaskazini? Kilimanjaro national park, Mkomazi np, Arusha np, Tarangire np, Manyara np, Ngorongoro np, na nyingine nyingi. Kwanini kuanza kuvunja nguvu hii kwa kuanzisha circuits nyingine pengine zitazoongeza gharama tu kwa serikali na watalii?
 
Utalii sio kuangalia wanyama pekee lazima tubadilike tuendane na wakati leo hii Dubai wanatengeneza mbuga zao zenye wanyama kama ambao wapo kwetu na ukweli ni kwamba wametoka kwetu kwahiyo itafika muda watalii wengi wataishia Dubai badała ya kują nchini kwetu kutolana na mikakati wenzetu waliyojiwekea huko mbeleni.

Utalii upo wa aina nyingi ingawa sisi tumekomaa na wanyama tu miaka nenda rudi wakati mila na tamaduni za baadhi ya jamii zetu ni utalii tosha pia fukwe na majengo ya kale, miamba na mapango, vyakula nk. Mpaka hapo hujaona umuhimu wa kuwa na uwanja wa ndege Wenye hadhi ya kimataifa kwa ukanda ule?
 
Utalii sio kuangalia wanyama pekee lazima tubadilike tuendane na wakati leo hii Dubai wanatengeneza mbuga zao zenye wanyama kama ambao wapo kwetu na ukweli ni kwamba wametoka kwetu kwahiyo itafika muda watalii wengi wataishia Dubai badała ya kują nchini kwetu kutolana na mikakati wenzetu waliyojiwekea huko mbeleni. Utalii upo wa aina nyingi ingawa sisi tumekomaa na wanyama tu miaka nenda rudi wakati mila na tamaduni za baadhi ya jamii zetu ni utalii tosha pia fukwe na majengo ya kale, miamba na mapango, vyakula nk. Mpaka hapo hujaona umuhimu wa kuwa na uwanja wa ndege Wenye hadhi ya kimataifa kwa ukanda ule?
Mkuu achana nae, unamuelewesha mtu aliyejiandaa kutokukuelewa. Muache akae na akili zake mgando.
 
Sawa ila lazima uangalie ukaribu na vivutio hivyo na vipo vingi sehemu gani. Huwezi kujenga tourist hub Kigoma ambapo vivutio vya utalii ni vichache ukaacha kujenga hub hiyo mahali kama Arusha ambapo vivitio hivyo vimelundikana. Mwanza ukiacha Ziwa Victoria kuna national parks ngapi ukilinganishwa na ukanda wa Kaskazini? Kilimanjaro national park, Mkomazi np, Arusha np, Tarangire np, Manyara np, Ngorongoro np, na nyingine nyingi. Kwanini kuanza kuvunja nguvu hii kwa kuanzisha circuits nyingine pengine zitazoongeza gharama tu kwa serikali na watalii?
International Airport hazijengwi kwa sababu ya Tourism peke yake. Kuna mambo mengi muhimu, pengine muhimu zaidi ya hilo swala moja tu la utalii.
Hili la utalii ndilo wewe limekupofusha akili kabisa?

Dar es Salaam ilivyo sasa, ungetamani isiwe na international airport kwa vile haipo kwenye eneo la vivutio vya utalii?
 
Mkuu achana nae, unamuelewesha mtu aliyejiandaa kutokukuelewa. Muache akae na akili zake mgando.
Lile wazo la Magu Kutengeneza mbuga nyingine tofauti na tulizozizoea lilikuwa sahihi sana sema wabongo tunachukua muda mrefu kuelewa vitu tunaishia kwenye kuponda bila kuwaza kwa usahihi na kufikiria kwa mapana zaidi. Fikiria Waarabu wameona wachukue wanyama huku kwetu wakatengeneze mbuga sisi tupo tu na zile zile za kale hata hatuwazi vizuri kuongeza vivutio zaidi vya utalii.
 
Mwanza haina sababu nzuri ya kuwa na international airport.
Ukiangalia majimbo ya nchi jirania ambayo yako mipakani na nchi yetu karibu na mwanza.. hapa naongelea Entebbe kwa Uganda na Kisumu kwa Kenya yote na hizo International Airports licha ya kuzidiwa uchumi na mwanza yetu.

Leo hii mtu akiwa na safari yoyote ya kibiashara pale Entebbe haitaji kufika kwanza Kampala kisha ndio aende Entebbe...mtu akiwa anahitaji kufika kisumu sio lazima afikie Nairobi, kama ilivyo kwa Tanzania ambapo mtu kutoka nje akiwa n business trip yoyote pale Mwanza inamlazimu afikie Dar kisha ndio atafute tena usafiri wa kumfikisha Mwanza.

Hii inaonesha ni jinsi gani sisi bado tuko nyuma kwenye suala zima la usafiri wa anga.... hivyo basi kuna kila sababu uwanja ulipo mwanza uwe upgraded na kuwa wa kimataifa.

Wewe kama hauoni sababu ya mwaza kuwa na international airport basi ni kwa sababu ya ujinga uliokujaa au zile chuki za kikanda ambazo mimi huwa naona ni za kitoto sana.
 
Back
Top Bottom