Mtambue rafiki mwenye dalili za uadui

Mtambue rafiki mwenye dalili za uadui

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,609
Ni vema tukafahamu kwamba katika maisha rafiki anaweza kuja kuwa adui au msaliti kwenye mambo mengi sana yakiwemo mambo ya kwenye mapenzi, biashara, kupata nafasi kazini, mahusiano na marafiki zenu au kwenye mikataba au tenda.

Kuna uwezekano mkubwa sana yule aliyeonekana kuwa karibu sana na wewe, yule aliyesimama kama rafiki mkubwa sana kwako na ambaye hukuwahi kuwaza kama siku moja anaweza kubadilika sasa anaweza kuwa adui mkubwa kuliko.

Yapo baadhi ya mazingira au dalili ambazo ni muhimu kila mmoja wetu akazifahamu na kuzikumbuka wakati wote ili kuweza kujua aina za watu wa jinsi hii. Dalili hizo ni kama vile;

Unaposikia au unapogundua kuwa rafiki yako anakusema vibaya kwa wengine wakati anapokuwa na wewe anajifanya malaika. Labda mmezoea kuongea mengi pamoja lakini baadaye unakuja kugundua yote hayo mliyokuwa mnaongea yeye anaongea kinyume akiwa na wengine na labda sio tu anaongea kinyume, yamkini anakupinga na hata kusema vibaya kuhusu wewe.

Anapokuja kwako anakuwa kama hajawahi kusema chochote kibaya kwako, anahisi haufahamu chochote na yamkini anakueleza ubaya wa hao wengine alioongea nao. Usifurahie habari hizi kutoka kwake, huyu ni ndumilakuwili mkubwa.

Unapohisi au unapogundua rafiki yako anakupinga au kukuonea wivu kwenye mambo fulani. Yamkini kuna mambo mnafanya kwenye ushirikiano wenu, tena mnafanya ukijua mnapendana, lakini kuna wakati unaona vijidalili vya kukuonyesha kuwa huyu unayedhania ni rafiki yako mara kwa mara hakubaliani na badhi ya vitu unavyoviwaza au kuvipendekeza na zaidi ya hapo kuna hali ya kukuonea wivu kwenye baadhi ya vitu kwenye maisha yako.

Upohisi au kugundua nia yake ya kutamani kupata zaidi yako. Inatokea kuna vitu mnavipanga au kuviongelea katika miradi au mikakati ya kimaisha, lakini katika hali zote mnazohusiana kwazo unakuja kugundua anapenyeza kwa wazi au kwa sirisiri kiu yake ya kupata zaidi yako, kiu yake ya kukushinda, kiu yake ya kukuongoza, kiu yake ya kuwa mbele zaidi yako.

Kwa mfano mnataka kufungua kampuni, labda lilikuwa wazo lako lakini yeye anafanya juu chini awe kiongozi, au mtu wa kusimamia fedha. Labda mnampango wa kukutana na watu fulani wa muhimu katika mikakati fulani, ghafla anakwambia ameshaonana nao na wameongea bila hata wewe kujua, ukimuuliza anakwambia alihisi wewe utakuwa umebanwa akaamua kufanya ili aje kukupa taarifa. Hali hii sio ya kutaka kukusaidia bali kukufunika. Nia yake hii niyauovu kabisa. Kuwa macho sana.


Unapohisi au kugundua kuwa ushauri anaokupa sio wa kukusaidia bali wa kukukwamisha huko mbeleni. Mara nyingine unaona wazi kuwa anakushauri, tena ushauri mzuri, ukidhani nia yake ni kuona unapenya kwenye maisha, hii ni kwasababu haujafungua macho yako vema, kila unapofuata ushauri wake mambo hayaendi.

Unakuja kugundua kuwa ushauri wake sio sana kukuwezesha kupenya bali kukutega au kukufunga kamba ili ukwame hapo mbeleni. Kibaya zaidi maranyingine anakushauri katika hali ambayo ukija kukwama hapo kesho yeye anachukua fursa uliyoikosa wewe.

Anakushauri kitu, kesho au keshokutwa biashara yako inashindwa na inakufa ghafla unaona mazingira ya yeye kuwachukua wateja wako au kulichukua soko lako.

Wakati haya yanapokuja kutokea yeye haumpati tena na ukimpata na kumuuliza anaweza kukwambia kuwa yeye hakuwa na nia mbaya. Fahamu kwamba huyu alikuwa adui tokea muda sana sema wewe hukuwa macho vya kutosha.




mwananchi
 
Ni kweli watu wa aina hii wapo kila kona huku kwetu!
[emoji15]
 
Nilikuwa na mmoja wa namna hiyo unaona mmeshibana kumbe kila mjadilianalo au kumwambia ye anaenda kueleza wengine tena kwa kufanya uonekane mbaya mbele za watu/jamii....

Kibaya zaidi ni nilipogundua kuwa hata wakati sina kazi na nimemaliza chuo ananisema vibaya kwa nilichosomea na anafurahia mimi kuwepo home tuuu sina mchongo wa maana ...
ila kipindi tunasoma nilimsaidia sana pamoja na kumpa kidogo kama pesa za matumizi kama mzazi wake akishindwa kumpa kwa kuwa mi nilikuwa na mkopo na yeye alisoma diploma ya ualimu hana mkopo.

Baada ya kumaliza na kupata kazi hapo ndipo nilipoona rangi zake halisi kwa kuwa alikuwa anafurahia mi kuwa chini sina ishu ya maana.....

Kweli hapo nilijisogeza pembeni na kufanya mambo yangu kivyangu na simwamini mtu yoyote.
 
Siku zote Rafiki anakuwa mmoja tu wengine waliobaki wanakuwa Washikaji tu., sasa ukiona una Marafiki zaidi ya Mmoja inabidi ujitathimini!
 
Hakuwahi kunisema vibaya,wala kunipa ushauri mbaya,hakuwahi kuonesha dalili yoyote ya kutaka kunizidi.....siku zote alikuwa mwema sana kwangu na kwa ndugu zangu lakini alichokuja kunifanyia sitakaa nikisahau,kwani kimekuwa donda ndugu moyoni mwangu! I trust nobody in this world.
 
Dawa yake ni kuwaepuka marafiki kwenye mambo yako ya kifamilia na kibiàshara maana huko ndiyo wanakowaharibia wanzao, shirikiana nao kwenye pombe kiasi, misiba na sherehe kidogo
 
Back
Top Bottom