Mtambue mtumishi wa Mungu wa kweli

Mtambue mtumishi wa Mungu wa kweli

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Habari waungwana,

Ni matumaini yangu kwamba hamjambo wote, na mnaendelea vyema kutimiza wajibu wenu. Napenda kuwambieni habari njema kwamba kwa siku hizi kumekuwa na watu wengi wanaohubiri ila wapo waongo na wapo wa kweli pia.

Mhubiri wa ukweli ni yule mwenye upendo na watu wote, mwenye hofu ya Mungu, asiyewasema watumishi wenzio vibaya, mara hoo fulani anatumia maji ya .... mara hooh fulani anatumia majini .. mara hooh .. flani ni free marson ,,, n.k.

Wa ukweli yote hayo humwachia Mungu kwani si vyema kuhukumiana. Ukiona kiongozi wako wa kiroho anawasema watumishi wengine vibaya ... mkimbie na MWOGOPE KAMA UKOMA!
 
ni kweli mkuu dini siku hizi imekua biashara unamponda m2 ili upate wateja katika bidhaa zako mteule kuwa macho siku za mwisho zakaribia
 
ni kweli mkuu dini siku hizi imekua biashara unamponda m2 ili upate wateja katika bidhaa zako mteule kuwa macho siku za mwisho zakaribia
Nimekusoma mkuu! tuwatambue kwa matendo yao!
 
Hakuna mtumishi wa Mungu kwa sababu hakuna Mungu.

Sema jingine.
 
Hakuna mtumishi wa Mungu kwa sababu hakuna Mungu.

Sema jingine.
Kwanza umenishtua! Hivi wewe ni mwanadamu / mtu au nini? Nikipata jibu nitajua ni kwa nini unasema hakuna Mungu.
 
Kumbe ukoma ni balaa kuliko hata ukimwi
Habari waungwana,
Ni matumaini yangu kwamba hamjambo wote, na mnaendelea vyema kutimiza wajibu wenu. Napenda kuwambieni habari njema kwamba kwa siku hizi kumekuwa na watu wengi wanaohubiri ila wapo waongo na wapo wa kweli pia.
Mhubiri wa ukweli ni yule mwenye upendo na watu wote, mwenye hofu ya Mungu, asiyewasema watumishi wenzio vibaya, mara hoo fulani anatumia maji ya .... mara hooh fulani anatumia majini .. mara hooh .. flani ni free marson ,,, n.k.
Wa ukweli yote hayo humwachia Mungu kwani si vyema kuhukumiana. Ukiona kiongozi wako wa kiroho anawasema watumishi wengine vibaya ... mkimbie na MWOGOPE KAMA UKOMA!
 
Mimi ni mtu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
Kama wewe ni mtu hakika hupaswi kumjua Mungu ... Sisi wana-Adam (Wana wa Adam) tunajua kwamba babu yetu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Hivyo Mungu yupo ndugu.
Naomba unijulishe nyie watu mlitokea wapi?
 
Kama wewe ni mtu hakika hupaswi kumjua Mungu ... Sisi wana-Adam (Wana wa Adam) tunajua kwamba babu yetu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Hivyo Mungu yupo ndugu.
Naomba unijulishe nyie watu mlitokea wapi?
Hujajibu swali nililokuuliza.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Nilianza kukuuliza swali hilo. Nijibu kwanza kabla ya kuniuliza maswali zaidi.
 
Hujajibu swali nililokuuliza.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Nilianza kukuuliza swali hilo. Nijibu kwanza kabla ya kuniuliza maswali zaidi.
Mungu yupo na huwa anajidhihirisha kwa wale wamwaminio katika Roho na kweli. Anaponya wagonjwa, anagawa riziki kwa waja wake.
Kikubwa zaidi ndiye Muumba wa kila kitu.
 
Mungu yupo na huwa anajidhihirisha kwa wale wamwaminio katika Roho na kweli. Anaponya wagonjwa, anagawa riziki kwa waja wake.
Kikubwa zaidi ndiye Muumba wa kila kitu.
Hujathibitisha. Umehubiri.

Sijaomba mahubiri. Nimetaka uthibitisho.
 
Hujathibitisha. Umehubiri.

Sijaomba mahubiri. Nimetaka uthibitisho.
Sina picha yake kwa sababu yeye ni Roho. Hivi ukiambiwa kwamba thibitisha kwamba furaha ipo utatibitisha vipi?
Furaha, upendo, chuki n.k huthibitika kihisia tu. Kama unakataa kwamba hakuna hisia, basi endelea kuamini hivyo. Na haya unayoyaandika ni kwa sababu milango yako ya ndani imefunguka vibaya.
 
Sahihi. Kwa sababu naamini unazungumzia watumishi wa kikristo, nadhani inabidi liangaliwe kwa upana wake. Mtumishi kwanza amjue Yesu na kumwamini. Hayo mengine yooote yanajirekebisha. Kwa sababu Yesu akishaingia ndani yake anamfanya kiumbe kipya, basi anakua na upendo, heshima, utii, na matendo yake yote kwa ujumla yanabadilika.

Kwa ambaye hamwamini Mungu, mara nyingi sio vizuri kudebate. Kwa sababu Roho huwapa ufahamu wa uwepo wa Mungu watu wote hapa duniani. Kwahiyo hata kama anapinga, ila ndani yake, nafsini mwake anakua hana uhakika. Ndio maana wengi wanakua wanapenda sana kudebate au kuargue na kudefend points zao.

Ila wewe kama mkristo kwa sababu una uhakika na Mungu wako, relax. Kama umemwambia mtu habari njema, umempa resources zote za kutambua uwepo wa Mungu, na bado anakataa. Unamwacha.
Hata mtume Paulo alisema hivyo.

Cha msingi usiache kuongea kuhusu Mungu, lakini usifikie hatua ya kubishana, inakua kama kupoteza wakati, while kuna wengine wengi wapo tayari kuskiliza.

Hii ndio hua inasababisha hata watumishi wengine kuhukumu watu, kusengenya, kwa sababu tu wamehubiri kuhusu Mungu watu wakampinga. Hapo wanafika mbali.

Pia unajua hapa duniani kuna choice nyingi sana. Ndio maana hata wanaopinga uwepo wa Mungu wanaishi na wanafanikiwa pengine kuliko wakristo. Hiyo ni neema ya Mungu. Lakini wote tunajua kua njia bora kabisa ni kumwamini na kumfuata yeye. Kama wanajua wanavyokosa, wanatakiwa wakubali wenyewe kumfuata Yesu na kuamini. Kuna tofauti kubwa sana.
 
Back
Top Bottom