Mtambue mtu uliye na mahusiano naye

Nyalotsi

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Posts
6,989
Reaction score
5,068
Kuna personality aina mbili ambazo binadamu tubaweza kuwa nazo. Unaweza kuwa introvert au extrovert (nimekosa neno la kiswahili).
Introvert ni watu ambao mambo yao mengi wanapenda kuyafanya kimya kimya, sio waongeaji, mara chache sana katika hali ya kawaida watajumuika na makundi ya watu. Muda mwingi wanapenda kuangalia tamthilia na movies wakiwa wametulia. Unaweza ukawa umetoka naye kimtoko lakini mwenzako muda mwingi yupo kimya au hata maongezi yake ni ya mkato mkato. Kwenye kuwasiliana unaweza kumtumia msg yenye maelezo mengi lakini yeye anakujibu neno moja tu 'poa'. Ukweli ni kwamba anaboreka na maongezi marefu. Anapenda kutulia peke yake.

Extrovert ni watu ambao wanapenda kufanya mambo yao wazi wazi. Wanapenda kujichanganya sana na Furaha yao ni kuona wanafurahia na watu wengine. Wanapenda kwenda 'out' na watu hata kwa gharama zao. Hata kuangalia muvi atapenda sehemu yenye watu wengi, hata kama ni nyumbani hawezi kuangalia peke yake. Atapenda muda mwingi muwe mnawasiliana ili ajisikie yuko karibu na watu. Wapenzi wa mpira wa miguu wengi wapo kundi hili. Ndio maana mtu ataondoka kwake na kuacha kila kitu na kwenda banda la video kuliko na watu wengi.

Introvert ni vigumu kujua matatizo yanayowakabili na wanapatwa sana na msongo wa mawazo na sonona. Pia huwa ni wepesi wa kujitoa uhai wanapozidiwa. Kama ni mpenzi wako utajikuta tu mnakuwa na ugomvi ambao sababu yake huijui kwani mambo mengi hayasemi.

Extrovert ni wepesi wa kuwajua matatizo yanayowakabili kwani wao kila kitu anawashirikisha marafiki zake na watu wanaomzunguka. Ila ni wepesi wa kutoa siri za ndani kwa watu wasiohusika. Na kukupa makavu ukimkosea ni kitu cha kawaida kwake.

Unapokuwa na uhusiano wa karibu na mtu inabidi umtambue yupo kundi lipi na yeye umuelezee ni nini unapendelea ili kuzoeana naye, msiwe na mifarakano ya mara kwa mara. Hii itapunguza malalamiko ya hisia zako kutojaliwa na mtu wako wa karibu kwani utaona Kama anakunyanyasa.

Jumapili njema wandugu na Mungu awabariki.
===============================================================================================================
 
Ambiverts??? Ipoje hiyo mkuu

hawa Ambiverts huwa na tabia za kati, wao huonesha tabia zile zipatikanazo kwa introvert na extrovert. hivyo tuwaite wao ni wastani wa hao Introvert na Extrovert, rejea sifa za Introvert na Extrovert kwa mkuu Nyalotsi kisha utamwelewa huyu Ambiverts vizuri.
 
Nashukuru kwa elim uliyonipa leo,umesaidia kumtambua mpenzi wangu! gd sunday tooo
 
Kumbe ndivyo tulivyo,santeee kwa darsa
Nalog off
 
Ambiverts??? Ipoje hiyo mkuu

^^
Pamoja na majibu mazuri ya segere na maelezo ya mleta mada,, tukumbuke kuwa uanishaji wa makundi hayo MSONDANI (Extrovert) na MMNDANI (Introvert) ulifanywa na mwanasaikolojia Carl Jung kwa kutazama Haiba (personality)
Kutokana na mageuzi makubwa ya ulimwengu wa saikolojia, walikuja wanasaikolojia wengine wengi wakiwemo akina Hockenburg, Phillip, n.k waliofanyia utafiti nadharia ya Carl Jung wakaongeza kundi la AMBIVERTS ambao huchukua 50% ya extroverts na 50% ya introverts.
Ni watu wanaoweza kuendana na mtu yeyote na mara nyingi ni wazuri wa kubadilika sawa na mazingira.
^^
 
Last edited by a moderator:
Eti eee nimejitambua sasa
Jpili njema nawe pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…