Mtambo wa CathLab waleta mapinduzi ya tiba ya kiharusi nchini

Mtambo wa CathLab waleta mapinduzi ya tiba ya kiharusi nchini

Taasisi ya Mifupa-MOI

Senior Member
Joined
Apr 15, 2025
Posts
118
Reaction score
214
Kwa muda mrefu, tiba ya kiharusi hapa nchini ilikuwa changamoto kubwa kutokana na ukosefu wa teknolojia ya kisasa ya kuchunguza na kutibu mishipa ya damu ya ubongo kwa haraka na kwa ufasaha.

Hali hiyo ilisababisha wagonjwa wengi kupoteza maisha au kubaki na ulemavu wa kudumu. Ujio wa mtambo wa kisasa wa Cathlab uliopo MOI umeleta mageuzi makubwa katika huduma za kibobezi na kuanza zama mpya za matibabu ya kiharusi nchini.

Akizungumzia mapinduzi hayo, leo Alhamis Januari 22, 2026 Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema mtambo huo umeongeza kwa kiwango kikubwa uwezo wa hospitali kuokoa maisha ya wagonjwa katika Taasisi hiyo na kuongeza ufanisi wa huduma kwani mtambo huo unawasaidia wataalam kujua tatizo lilipo tofauti na hapo nyuma walikuwa wakifanya upasuaji kwa kubahatisha.

"Miaka ya hivi karibuni tulikuwa hatuna namna ya kujua ni sehemu hasa ambazo zimepata matatizo... Lakini katika taasisi yetu (MOI), tuna wataalam ambao wamesoma na kubobea katika kutekeleza majukumu yao ya kutumia vifaa hivi vya kisasa mashine inayoitwa Cath Lab (Angio Suite)" amesema Dkt. Mpoki

Aidha, Dkt. Mpoki ametoa rai kwa Watanzania na watu wote wenye dalili za kiharusi kuwahi katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kuchunguzwa ili kama kuna maeneo ya kurekebishwa yarekebishwe kabla ya kupata ulemavu wa kudumu.

Kwa upande wake, mtaalam kutoka Pennsylvania nchini Marekani, Prof. David Sacks amesema wameshirikiana na wataalam wa MOI katika kubadilishana uzoefu katika matumizi ya mtambo wa CathLab (Angio Suite) kwa kutumia mbinu za Kisasa kubaini kwa usahihi sehemu yenye tatizo kwenye mishipa ya damu ya ubongo.

Ameongeza kuwa ushirikiano huo umeongeza ufanisi wa uchunguzi na matibabu, kupunguza hatari ya ulemavu na vifo vitokanavyo na kiharusi, pamoja na kuwezesha wataalam wa ndani kufanya tiba hizo kwa viwango vya kimataifa.

Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano huo wa kitaalamu utaendelea ili kuhakikisha wagonjwa wengi zaidi wanapata huduma bora na za kisasa hapa nchini bila kulazimika kwenda nje ya nchi.
IMG-20260122-WA0088.jpg
IMG-20260122-WA0091.jpg
IMG-20260122-WA0089.jpg
 
Hii ni kwa mujibu wa Chatgpt.
Bei ya mashine zinazotumika katika angio suite, kama vile angiography machines au fluoroscopy systems, pia inatofautiana kulingana na chapa, vipengele, teknolojia inayotumika, na uwezo wa mashine hiyo. Hizi ni mashine za gharama kubwa ambazo zinahitaji matengenezo ya juu na huduma maalum.
Hapa ni makadirio ya bei kwa baadhi ya mashine muhimu zinazotumika katika angio suite:
1. Angiography System
Angiography system ni kifaa kinachotumika kuchukua picha za mishipa ya damu (angiogram) kwa kutumia x-rays na fluoroscopy.
Bei:
Mashine za angiography za kiwango cha chini (basic systems) zinaweza kugharimu $100,000 - $300,000 (karibu 100,000,000 - 300,000,000 TZS).
Mashine za angiography za kiwango cha juu (advanced systems), zenye teknolojia ya kisasa ya imaging (digital subtraction angiography - DSA), zinaweza kugharimu hadi $500,000 - $1,000,000 (karibu 500,000,000 - 1,000,000,000 TZS).
2. C-arm Fluoroscopy Machine
C-arm ni kifaa kinachotumika kuchukua picha za x-ray wakati wa matibabu kama angioplasty, stent placement, au upasuaji wa misuli na mifupa. C-arm ni kifaa kinachotumika kwa uchunguzi na pia kwa matibabu ya mishipa ya damu.
Bei:
Bei za C-arm fluoroscopy zinaweza kuwa $50,000 - $250,000 (karibu 50,000,000 - 250,000,000 TZS), kulingana na chapa na uwezo wa mashine hiyo.
Mashine zenye teknolojia za kisasa kama 3D C-arm zinaweza kugharimu hadi $500,000 (karibu 500,000,000 TZS).
3. CT Angiography (CTA) Systems
CT Angiography hutumika kuchunguza mishipa ya damu kwa kutumia picha za tomography ya kompyuta (CT scans). Inahusisha mashine ya CT skani ya hali ya juu ambayo ina uwezo wa kufanya angiography.
Bei:
CT scanner ya kiwango cha chini inaweza kugharimu $150,000 - $500,000 (karibu 150,000,000 - 500,000,000 TZS).
Mashine za CT skani za kisasa, kama zile zenye dual-source au 64-slice, zinaweza kugharimu $500,000 - $2,000,000 (karibu 500,000,000 - 2,000,000,000 TZS).
4. Endovenous Laser Therapy (EVLT) Systems
Kwa matibabu ya varicose veins, mashine za laser zinazotumika kwa EVLT ni za gharama kubwa.
Bei:
Mashine za Endovenous Laser zinaweza kugharimu $50,000 - $200,000 (karibu 50,000,000 - 200,000,000 TZS).
Vitu vya ziada
Vifaa vya kutunza na kudhibiti (kwa mfano, vifaa vya upasuaji na vifaa vya picha): Bei za vifaa hivi pia huongezeka kwa gharama, kulingana na mfumo wa kudhibiti na huduma.
Matengenezo na huduma: Gharama za matengenezo ya mashine hizi ni muhimu sana. Hospitali au kliniki lazima ziwe na mkataba wa matengenezo na kampuni za teknolojia, na hii inaweza kugharimu $10,000 - $50,000 kwa mwaka kulingana na mashine.
Hivyo, ukizingatia gharama za kununua, matengenezo, na vifaa vya ziada, mashine hizi ni za gharama kubwa, na hospitali au kliniki zinazotaka kuanzisha angio suite lazima ziwekeze kiasi kikubwa cha fedha.
Ikiwa unahitaji kujua zaidi kuhusu uuzaji wa mashine hizi au una maswali kuhusu jinsi ya kupata hizi mashine kwa biashara yako au hospitali, niambie!
 
Vyakula bora vya kuzuia kiharusi na kuishi kwa afya – ushauri wa mtaalamu Prof Elaine Rush

View: https://m.youtube.com/watch?v=3gWDwVYQAgs
taarifa wazi na za kuaminika kuhusu kiharusi na shambulio la muda mfupi la kukosa damu kwenye ubongo (TIA), ikijumuisha sababu za hatari na njia za kujikinga, pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaotambulika wa huduma ya kiharusi
 
2026
Perth, Australia

Kiharusi na kinga yake – ushauri wa mtaalamu Prof Graeme Hankey mtaakamu wa neurololia


View: https://m.youtube.com/watch?v=3ewrIxClepw

Video hii inatoa taarifa wazi na za kuaminika kuhusu kiharusi na shambulio la muda mfupi la kukosa damu kwenye ubongo (TIA), ikijumuisha sababu za hatari na njia za kujikinga, pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaotambulika wa huduma ya kiharusi.

SELI ZA UBONGO NA KIHARUSI


View: https://m.youtube.com/watch?v=wICFx6ZW8d8
 
2026
Athari za kisaikolojia na kiakili baada ya kiharusi Prof Suzanne Barker Collo mwanaSaikolojia wa mishipa ya neva


View: https://m.youtube.com/watch?v=PeFTDUD75WA
Video hii inatoa taarifa wazi na za kuaminika kuhusu kiharusi na shambulio la muda mfupi la kukosa damu kwenye ubongo (TIA), ikijumuisha sababu za hatari na njia za kujikinga, pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaotambulika wa huduma ya kiharusi
 
2026

Athari za kiharusi kwenye uwezo wa mwili na shughuli za kila siku

View: https://m.youtube.com/watch?v=L7dPzcv--Gk
Katika video hii, utaona na kusikia maelekezo ya hatua kwa hatua yanayotegemea ushahidi na mbinu bora kuhusu jinsi ya kuishi na kiharusi na kusaidia kupona — ikiwa ni pamoja na jinsi kupona kunavyoweza kuwa, changamoto za kawaida, na mikakati ya kusaidia maisha ya kila siku.
 
2026

HISIA BAADA YA KIHARUSI KUTOKEA

View: https://m.youtube.com/watch?v=Zt4xpxW_4j0
Katika video hii, utaona na kusikia maelekezo ya hatua kwa hatua yanayotegemea ushahidi na mbinu bora kuhusu jinsi ya kuishi na kiharusi na kusaidia kupona — ikiwa ni pamoja na jinsi kupona kunavyoweza kuwa, changamoto za kawaida, na mikakati ya kusaidia maisha ya kila siku.
 
2026
MPITO WANGU Kurudi nyumbani baada ya kiharusi kutoka hospitalini uzoefu binafsi


View: https://m.youtube.com/watch?v=xw5BX3wQ9rk
Katika video hii, utaona na kusikia maelekezo ya hatua kwa hatua yanayotegemea ushahidi na mbinu bora kuhusu jinsi ya kuishi na kiharusi na kusaidia kupona — ikiwa ni pamoja na jinsi kupona kunavyoweza kuwa, changamoto za kawaida, na mikakati ya kusaidia maisha ya kila siku.
 
2026
Uzoefu binafsi wa mchakato wa urekebishaji na kupona baada ya kupata kiharusi


View: https://m.youtube.com/watch?v=tEBIw1qtkcU
Katika video hii, utaona na kusikia maelekezo ya hatua kwa hatua yanayotegemea ushahidi na mbinu bora kuhusu jinsi ya kuishi na kiharusi na kusaidia kupona — ikiwa ni pamoja na jinsi kupona kunavyoweza kuwa, changamoto za kawaida, na mikakati ya kusaidia maisha ya kila siku.
 
2026
Jinsi ya kuzuia vidonda vya presha (mbinyo mwilini) kwa mtu mwenye kiharusi anayeshinda amelala kitandani kwa muda mrefu

View: https://m.youtube.com/watch?v=CC3-Olgx5c8
Video hii inaonyesha mbinu bora za uuguzi na utunzaji kwa mtu aliye na kiharusi kikali, kulingana na ushahidi wa kitaalamu. Inazingatia faraja, heshima, usalama, na kuzuia matatizo nyumbani au katika mazingira ya huduma.
 
2026

Mambo yanayohusiana na umri kuhusu kiharusi Dkt Geoff Green


View: https://m.youtube.com/watch?v=_fwNVj5c6d8
Utaalamu wa huduma ya watu wazee yaani Gerentorojia, udaktari wa wazee na magonjwa yao ikiwemo kiharusi ambacho huwapata watu wa kundi la rika la wazee
.
Video hii inatoa taarifa wazi na za kuaminika kuhusu kiharusi na shambulio la muda mfupi la kukosa damu kwenye ubongo (TIA), ikijumuisha sababu za hatari na njia za kujikinga, pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaotambulika wa huduma ya kiharusi.
 
2026

Mazoezi ya mwili na kuzuia kiharusi Prof Ralph Maddison

View: https://m.youtube.com/watch?v=j2u7Jdbax7c
Video hii inatoa taarifa wazi na za kuaminika kuhusu kiharusi na shambulio la muda mfupi la kukosa damu kwenye ubongo (TIA), ikijumuisha sababu za hatari na njia za kujikinga, pamoja na ushauri kutoka kwa wataalamu wanaotambulika wa huduma ya kiharusi.
 
Back
Top Bottom