Mtakatifu na kinyume chake

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Wakuu nimewaletea uzi huu baada ya kubaini kuna UTATA wa maana ya neno MTAKATIFU na ni yupi anaye stahili kuitwa na kinyume chake ni nin.

Kwanza MTAKATIFU ni neno la kiswahili linalotokana na neno TAKATA( safi,isiochafuka, nadhifu,bila dhambi,bila uwonevu, bila dhulma, bila nijasi)basi kwa sehemu kama hiyo inaitwa "PATAKATIFU.
NA kama ni mtu anaitwa MTAKATIFU.
na mtu yoyote yule anaye anyemwona mweziwe ametakata, msafi na hana dhambi, anaweza akamwita MTAKATIFU, na kinyume cha MTAKATIFU na kwa vile utakatifu unatokana na KUTAKATA (usafi) ni MCHAFU au"MCHAFUKOGE
 

Kipala

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
3,606
1,500
Kwa maana ya kietomolojia ni sawa kabisa unachosema. Lakini jinsi ilivyo mara nyingi neno "mtakatifu" limepata maana ya pekee na mara nyingi katika matumizi yake ni maana hii ya pekee yaani ya kidini inayotumiwa.
 

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Mkuu itabidi turudi nyuma, zamani kabla ya dini hazijaingia kwenye jamii ZETU za kiswahili neno hilo lilikuepo na lilikua likitumika, kwahivo sio kila mtu akilitumia anamaanisha kidini, uzito wa neno MTAKATIFU upo kiasili zaidi, ambaye ni KUTAKATA au MTAKATA
 

Safari Safi

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
2,695
2,000
Neno hilo hata lingebaki kutumika kidini tu, Bado lina utata, Kwa sababu Utakatifu, si tendo, utakatifu siyo tukio, utakatifu ni ' Nia ovu'
Wagalatia 5:16-22.
kwa mantiki hiyo hakuna kigezo cha kumtambua mtakatifu
 

MPHINGU

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
519
1,000
Mkuu imani ya binadamu ni yamakisio au yahisia, ndio maana binadamu anaweza kuamini kitu, anatoa ushuhuda na kuapa, lakini kwa mungu sio sahihi.
na wewe kwa kusema, hakuna kigezo cha kumjua MTAKATIFU, mbona sisi binadamu tunawajua watakatifu wengi tu Akina Francisco, Albano, Peter, Joseph na wengineo
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom