Mtaji wa TZS 80,000

Mtaji wa TZS 80,000

Neema Massawe

Member
Joined
Aug 13, 2014
Posts
44
Reaction score
9
Mtaji wa TZS 80,000


Kwa mtaji wa TZS 80,000 tu utaweza kuigeuza simu yako kuwa mtambo wa kutengeneza pesa zaidi ya TZS 1,000,000 kwa mwezi na kupata huduma za bure za mawasiliano.


Kwa habari zaidi piga 0658977330 au ni sms nikupatie maelezo.


Kama upo Dar basi tembelea ofisi yetu iliyopo Makumbusho Bus Terminal & Shopping Complex, Ghorofa ya kwanza (Juu ya Uchumi Supermarket)
 
weka mambo yote hapa hadharani bana...sasa wote tukikupigia simu hicho kimeo chako kitaishiwa chaji!!
 
Haya mambo ndio yale yale, unashindwa hata kuweka hints tu hapa
 
Ukitaka hints tembelea ofisini kwetu. Tupo Makumbusho Bus Terminal & Shopping Complex, Ghorofa ya Kwanza (Juu ya Uchumi Supermarket).
 
Kwa mtaji wa TZS 80,000 tu utaweza kuigeuza simu yako kuwa mtambo wa kutengeneza pesa zaidi ya TZS 1,000,000 kwa mwezi na kupata huduma za bure za mawasiliano.

Kwa habari zaidi piga 0658977330.

Matapeli kazini!

Wana jf kuweni makini sana.
 
Hakuna kampuni inayotangaza matangazo yake kijinga hivi, acheni utapeli mwisho mnafikia kuwa ma Escrow, unadhani hao walianzaje?
 
Matapeli kazini!

Wana jf kuweni makini sana.

Wanaotaka habari kuhusu fursa hii mmewekewa namba ya simu. Kama hamuwezi kupiga basi tutumie hata sms tukupigie ili tukuelezee kuhusu hii fursa.

Hii ni biashara mpya kabisa ya mtandao kwenye mawasiliano ya simu hapa Tanzania na kampuni ilioanzisha mtandao huu ni kampuni ya Kitanzania.

Tayari Watanzania wapatao laki mbili na zaidi wameshachangamkia fursa hii mpaka sasa.
 
Haya maelezo kuhusu hii fursa haya hapa:

Ni kwamba Zantel wameipatia tenda kampuni ya Kitanzania kuuza airtime zake kwa njia ya mtandao. Kujiunga unalipia TZS 76,500 ambapo unapata kifurushi chenye vocha ya TZS 10,000, laini ya Zantel, kitabu cha maelezo ya biashara na kadi ya kujiunga.

Ukishajiunga unapata reference number yako ya kuunganisha watu wengine. Malipo yanafanyika kwenye kampuni na kujiunga unajiunga kwenye simu yako.

Baada ya kujiunga, kila mtu utakayemualika utapata TZS 10,000 atakapojiunga na mtandao huu. Mtu aliyemuingiza akiingiza mtu mwingine utapata TZS 4,000. Huyu wa kizazi cha pili akiingiza mtu wa kizazi cha tatu utapata TZS 2,000. Unapata TZS 2,000 kwa watu wanaojiunga kuanzia kizazi cha tatu mpaka cha tisa. Kizazi cha kumi unapata TZS 4,000.

Ukiacha haya malipo ya kujiunga, kuna malipo ya mwezi. Unatakiwa ununue mda usiopungua TZS 10,000 kwa mwezi ili upate malipo ya mtandao kwa mwezi husika kwenye mtandao wako kwa vizazi 10 kwenda chini. Unapata 1% ya malipo ya manunuzi ya airtime ya watu wa kizazi cha kwanza na cha 10. Vizazi vilivyobaki unapata 0.5%.

Ukishaingiza watu 5 basi unapata fursa ya kuwa Dealer wa Zantel kwa kugawa lines za Zantel bure kwa kuwasajili watu na utalipwa 20% ya hela watakazonunua airtime kwa mara ya kwanza mara baada ya kujisajili. Malipo haya ya 20% utayapata kwa kipindi cha miezi mitatu. Baada ya hapo utakuwa unalipwa 10%.

Vilevile kuna malipo mengine kama ya Kiwanja, Gari la Kifahari, Nyumba ya Kifahari na mda si mrefu itaongezwa na bima ya afya pia. Malipo haya yatategemea na idadi ya watu waliopo kwenye mtandao wako.

Vilevile kuna huduma ambapo unalipia TZS 1,500 na kupata fursa ya kupiga Zantel kwenda Zantel bure pamoja na kupewa mda wa bure kwa simu nyingine pia.

Huu mtandao bado mpya hivyo kuna fursa nyingi sasa hivi kwa watakaowahi kuuchangamkia na kujenga mtandao wao. Hii kitu watu wanaichangamkia sana. Watakaokuja baadaye watapata shida ya kutafuta watu kwani wengi watakuwa wameshajiunga tayari.

Kwa wale watakaotaka kuunganishwa na fursa hii basi karibuni ofisini kwetu kama nilivyoelezea kwenye post ya kwanza hapo juu kama mko Dar. Mlioko nje ya Dar tuwasiliane kwa namba hii 0658977330 ili tupange mikakati ya kukuwezesha kujiunga huko huko uliko.
 
Leo kuna promotion hivyo kwa watakaojiunga leo basi watapata simu ya bure ya Zantel kwa hela hiyo hiyo ya TZS 76,500
 
Mhh hilo jina ndio limenistua. Hasa ukitia maanani tarehe za kwenda mlimani kuhesabiwa zimekaribia. Isije ikageuka nauli.
 
Mtaji wa TZS 80,000


Kwa mtaji wa TZS 80,000 tu utaweza kuigeuza simu yako kuwa mtambo wa kutengeneza pesa zaidi ya TZS 1,000,000 kwa mwezi na kupata huduma za bure za mawasiliano.


Kwa habari zaidi piga 0658977330 au ni sms nikupatie maelezo.


Kama upo Dar basi tembelea ofisi yetu iliyopo Makumbusho Bus Terminal & Shopping Complex, Ghorofa ya kwanza (Juu ya Uchumi Supermarket)

yaan wewe mtu kupata hints tu hadi aje offisini....duuuuh
 
Mhh hilo jina ndio limenistua. Hasa ukitia maanani tarehe za kwenda mlimani kuhesabiwa zimekaribia. Isije ikageuka nauli.

Hahaha watu wanajifanya kutengeneza fursa kumbe wanatumia janja kugeuza wenzao kuwa fursa kwao. Utanielewa tu!
 
Nimeulizwa in pm swali la msingi kwamba nini tofauti ya mtandao huu na mitandao mingine? Nimeona nianike majibu yangu hapa ili kila mtu ayaone:

Kuna tofauti nyingi sana.

Kwanza mtandao huu umejikita katika kutoa huduma ya mawasiliano ambayo kila mtu hapa Tanzania anaihitaji kwa shughuli zake za biashara hata mama ntilie, makuli na watu wa kawaida huko vijijini tofauti na mitandao mingine ambayo bidhaa zake ni za anasa au kusadikika.

Pili mtandao huu ni mpya tofauti na mitandao mingi mingine hivyo una fursa kubwa ya kupata watu wa kujiunga nayo kwani wengi bado hawajajiunga na hii fursa.

Tatu mtandao huu ni kampuni ya Kitanzania iliyosajiliwa hapa nyumbani hivyo italipa kodi na kulipatia taifa mapato.

Nne ni vizuri kuwa na utamaduni wa kupigia debe ubunifu unaotokea nyumbani na kuunga mkono kuliko kushabikia vitu vya nje tu kwani kama msemo wa kiswahili usemavyo, zimwi likujualo halikuli likakwisha.

Tano kampuni ya Zantel ni kampuni kubwa hapa Tanzania yenye kufanya biashara ya uhakika. Kwa sababu hiyo, haitaruhusu kampuni ya kitapeli ifanye biashara yake kupitia bidhaa za Zantel. Hivyo mtandao huu ni wa uhakika. Mara tu mtu akishajiunga chini yako basi utamuona palepale kwenye ofisi yako ya mtandaoni pamoja na mapato ulioingiza kupitia kwake.

Sita kampuni nyingi za kimtandao zinatumia hela za watu wanaolipa mwisho kulipia watu waliojiunga mwanzoni. Kwa maana nyingine hakuna uzalishaji ambao unafanywa na mtandao ili kuingiza kipato cha kugawana bali hela za wanachama ndio zinazotumiwa kutengenezea mapato ya kugawana. Kilichofanyika kwenye deal hii ya Zantel ni kwamba Zantel itaondoa gharama za matangazo kujitangaza ambazo ni kubwa mno hasa kwa makampuni ya simu kama tunavyoshuhudia mabango yao, kwenye magazeti, mitandaoni, n.k. Hivyo badala ya Zantel kumwaga pesa kwa ajili ya kujitangaza na kushindana kibiashara, hela hizo zinaingizwa katika mapato ya wana mtandao ambao wao wanasambaza biashara hii kwa njia ya mdomo kuwaambia ndugu na jamaa zao kuhusu fursa hii ya mtandao.
 
This's another form of network marketing alias Ponzi Scheme!
 
Back
Top Bottom