Mtaji wa CCM umebakia kwa kina mama tu

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,818
30,382
Wakuu,

Hakuna atakayebisha kwamba upepo wa kisiasa Tanzania umebadilika kabisa, harufu ya mageuzi imetanda, CCM imepotenza nguzo muhimu karibia zote na imebakiza hii ya KINA MAMA.

Siku ambayo mama zetu watastukia kwamba CCM sasa hawana jipya basi ndiyo itakuwa mwisho wake, wengi tunajua mama zetu ni wagumu sana kubadili uelekeo kwa ghafla, ingawa wao ndiyo wanapata shida kubwa sana hasa vijijini - lakini ndiyo wanakuwa kwa kwanza kushabikia CCM na kuvaaa khanga za chagua kikwete ambazo wengi huzitunza vizuri sana na kuzivaa wakati wa mikutano ya CCM.

Nachowasikitika CCM ni kupoteza nguzo ya VIJANA, vijana wengi kama si wote wapo CDM, unapopoteza nguzo hii ujue chama chako kinaingia shimoni, na kibaya zaidi CCM imekosa watu makini wa kujaribu kurudisha imani ya wananchi hasa vijana na hii ni hatari kubwa sana kwao.

CCM wanapofikia mahala pa kusema ushindi ni ushindi tu - hata wa kura moja zaidi ni ushindi - yaani hapo ujue kwamba sasa chama kimekosa mvuto na kinakufa, Chama kinapoanza kuangukia wazee wastaafu wakaokoe jahazi kwenye kampeni ina maana hakina vijana makini wa kukisemea mbele ya jamii na wakakubalika.


Chama kila kinapoenda kwenye mikutano yake ya kampeni lazima kiende na muziki na maigizo kuvuta wananchi- hapa lazima ufikiri mara mbili kwamba hoja zao hazina ushawishi kwa walio wengi kwa sasa. ndugu zangu hadi leo hatujui ni kwa nini baadhi ya wana CCM walizuiwa kufika igunga - hii inaonyesha ndani ya CCM yale makundi sasa ndiyo yamekomaa.

Mwisho nawapongenza wana CDM kwa ushindi wa kishindo Igunga na tunawaomba wana igunga wote kwamba muda ukifika CDM itarudi kuwashukuru, kazi nzuri sana na CDM sasa imepata focal point katika ukanda huo, hii itasaidia kupeleka ujumbe wilaya zingine jirani kama Sikonge, Urambo kwa 6, Nzega na hapo Tabora Mjini kwa mzee wa Mi-Bastola.

Kina mama, mama zetu tunawaomba imeifikia muda sasa muwaambie CCM kwamba khanga basi, vitenge basi ila mnataka utatuzi wa kero zenu.
 

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,636
Yana Mwisho haya FUSO.
Wanawake ni Mama Zetu, Dada zetu, Mabinti zetu, ni wake zetu ni ndugu, jamaa na rafiki zetu.
Hapa tulipokwama tuko nao pamoja, mfumo mbovu wa elimu, rushwa, uzembe, ukosefu wa
usimamizi wa sheria, mfumo mbovu wa usimamizi wa afya, food insecurity, infllation, ukosefu wa ajira,
mfumo mbovu wa uchaguzi, yote haya wanayaona.

Vijana waigunga sasa wamebaki wanalia, Machozi yao hayawezi kutoka bure, yatatiririka na kufika
kwenye matiti ya wamama wao, hapo ndio watakaposhtuka. sijui CCM watawaambia nini?
 

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
Fuso nadhani na wa kina mama just a time tu watakuwa upande wa mageuzi, coz wakina dada most of them wapo upande wa mageuzi bado mama zetu tu kubadilika, siku iyo itakuwa ni kilio na kusaga meno kwa c.c.m
 

Komeo

JF-Expert Member
May 3, 2011
2,497
1,169
Tena hao wamama waliobakia ccm ni wazee. Ukiona kijana mwanamama amevaa sare zao ujue analipwa mshiko kwa aina fulani ili mkono wake uende kinywani.
 

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,957
4,620
Watu wote hawawezi kubadilika kwa mkupuo. Ni lazma lianze kundi moja moja hadi makundi yote yatakuwa na msimamo mmoja.
Bado siku chache tu akina mama hasa wale wa mikoa ya pwani na wao wataona ukweli.
 

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
281
c.c.m kwisha habari yake, jana walikuwa na mkutano eneo la pugu kajiungeni sheli (ukonga) wanampokea Dr. kafumu kwa ushindi na kurejea nyumbani pugu, watu walikuwa wachache hata hamsini hawafiki, wengi ni wakina mama isitoshe most of them ni viongozi wa shina,matawi na kata. c.c.m aibu tupu Dr kafumu hata wakazi wa pugu awajajitokeza pamoja na kutangaza sana ujio wake.
Kama nadanganya nipo tayari kukosolewa wakuu. Magamba kazi kwenu.
 

peri

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,581
1,162
kama cdm inataka kufanikiwa haina budi kwanza kujichimbia mizizi kwenye kundi lenye idadi kubwa ya wapiga kura.
wawe wazee, vijana au kinamama.
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,818
30,382
c.c.m kwisha habari yake, jana walikuwa na mkutano eneo la pugu kajiungeni sheli (ukonga) wanampokea Dr. kafumu kwa ushindi na kurejea nyumbani pugu, watu walikuwa wachache hata hamsini hawafiki, wengi ni wakina mama isitoshe most of them ni viongozi wa shina,matawi na kata. c.c.m aibu tupu Dr kafumu hata wakazi wa pugu awajajitokeza pamoja na kutangaza sana ujio wake.
Kama nadanganya nipo tayari kukosolewa wakuu. Magamba kazi kwenu.
na ndiyo maana kila mikutano yao wasipowakodi ze-komedy au TOT bendi basi wenyeviti wa mashina ndiyo watakuwa wasikilizaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Top Bottom