Mtaji wa 46M faida 540,000, pia mtaji wa 45M faida 576,000

Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni zakuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukar unaiuza kwa miezi2 nafaida yake ni 540000 wakati huo gharama zamanunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton32 sawa namifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidgo tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji
Ndugu biashara ni somo ambalo watanzania wengi hawakufaulu Kuna nyuzi nyingi sana za kuomba mawazo ya biashara gani mtu afanye na anaeomba ana mtaji mkubwa tuu lakini ushauri uliomo inabidi tufikirie kuoa mchaga tuu huenda ukapata wazo zuri la biashara.

1. Jingalie kama wewe ni mtu wa biashara maana biashara unahitaji kujituma kujinyima na ukauzu vinginevyo utarudi kuwa omba omba, zipo biashara unaweka pesa hata 10m lakini profit yake kwa mwezi ni zaidi ya 3m.

Ila Kuna hizi biashara unaweka 20m upate faida 300k kama huna pesa ukafanya inaitwa biashara kichaa ila kama pesa unayo na unafanya hii inaitwa biashara ya kitajiri yaan unainvest Ili pesa Yako isipotee yaan izunguke lakin kimaisha ushafanya Kila kitu na bank kuko vizuri Hizi wanaofanikiwa ni matajiri sababu wanakuwa na target za mauzo kwa kiwango flan hivyo faida anayopata kwenye mauzo sio kitu yeye anasubiri robo mwaka apate incentive yake Bado anakuwa anasaidiwa transport ila kwa mtu ambae hajui anaiga anaumia anaishia kusema lazima kuloga ndio ufanikiwe.

2. Kama wewe sio mtu wa biashara basi tafuta mtu alie kwenye biashara Jenga urafiki nae wa kibiashara kubaliana nae muwekeze pamoja uwe unapata gawio zuri au mfanye awe meneja wako we Mpe Target atakupambania hapo akipata Zaidi usitamani na akikosa usisikilize stori zake, jali pesa Yako.

Tajiri anaspend to invest, maskini ana invest kuspend
 
Hiyo pesa ingiza kwenye Mazao utakuja kunishukuru. Yaani 46M inakuletea laki Tano halafu unapata usingizi?
Kweli wenye michongo hawana pesa na wenye mitaji hawana michongo.

Hiyo pesa unapaswa kuwa imeidabo ndani ya miezi sita na kwa mwaka Uwe na 100M. Ingiza chaka Acha kukaa mjini na pesa yote hiyo inazeeka tu.
 
Habari wakuu mnaionaje hizi baishara ni zakuendelea kufanya kweli tandam ya gari ya sukari inabeba mifuko 600 ya sukar unaiuza kwa miezi2 nafaida yake ni 540000 wakati huo gharama zamanunuzi 46m faida kwa Kila mfuko jumla jumla ni tsh 900.

Wakati huo huo mtaji wa gari ya ngano 45m hapo gari ya ton32 sawa namifuko 1280 kwa Kila mfuko ukiuza jumla faida ni tsh 450 sawa jumla ya 576000 kwa mifuko yote ambayo unaiuza kwa miezi 2.

Je, wakuu hii biashara inanichanganya sana mtaji mkuwa faida kidgo tupeane fursa za hela ili tubadilishe biashara tupate faida anagalau inayoendana na mtaji
Tafuta biashara nyingine hiyo ni risk kubwa sana yaani faida ni asilimia 1.3 ya mtaji then unaipata ndani ya miezi miwili are you serious?
 
Huwa mnalalamika situation ya biashara na hamtoi details hasa juu ya location. Unakuta mtu analalamika kitimoto hailipi unajikunja kumuelekeza kumbe jamaa yupo Unguja.

Nina kifremu naambiwa jirani kwenye godown hapa kabla sijapanga aliuza unga wa jumla alikuwa anauza sana watu wanapishana semi zinatoka Iringa uko zinajaza. Jamaa akafirisika eti watu wanajiuliza ilikuwaje, simply ni kwamba alikuwa anafanya biashara ya sifa kama wewe. Siku ukiagiza canter mvua imenyesha, likatumbukia mtoni likamwaga unga lazima uchanganyikiwe. Hasara moja inakula faida ya siku nyingi sana.

Yani kwenye inventory ya milioni 40 unapata laki tano??? Biashara yangu ndogo sana ila nikitumia 5M huwa napata laki tano, yani unafanya 10 times ya hela yangu na unateseka zaidi yangu ila faida tunalingana.

Nishawahi fanya research ya vyakula vya jumla kama mchele na unga, au mahindi. Kitu kikubwa kule ni uchawi, ila sio faida. Nimekaa sana Tandika nasoma wafanyabiashara na madalali nikajihakikishia ni biashara kichaa. Eti mtu ulete tani 20 za mchele upate faida milioni moja, si wehu huo. Alafu hasara ikija sasa, milioni tatu nne kawaida.

Unakuwa mfanyabiashara unaishi kwa hasira mtu akikukanyaga unampiga. Sura imekakamaa hela unazo ila hupendezi mawazo tu.
Ushauri wako ni upi niingie ktk biashara zipi
 
Hiyo pesa ingiza kwenye Mazao itakuja kunishukuru. Yaani 46M inakuletea laki Tano alafu unapata usingizi?
Kweli wenye michongo hawana pesa na wenye mitaji hawana michongo.
Hiyo pesa unapaswa kuwa imeidabo ndani ya miezi sita na kwa mwaka Uwe na 100M. Ingiza chaka Acha kukaa mjini na pesa yote hiyo inazeeka tu.
Chaka kama wapi nikapige Moshe gani
 
Location nzega...ila nawaza vitu pia kuagiza labda kuuzia mtandaoni
Mtandaoni kwa Nzega sijui. Ila kwa retail ya vinywaji vikali na pombe ukiwa supplier wa eneo lako hela na mzunguko unapata. Sifa kuu ya Watanzania ni uvivu, umbea, ulevi na pombe.

Makampuni ya mitandao, wauza simu, wamiliki wa clubs na bar, wamiliki wa kampuni za pombe, wenye mahoteli na lodges wote wametumia udhaifu huo.

Mambo mengine yanategemea ukoje, elimu, umri, muda, ukali na ukorofi, akili, etc
 
Back
Top Bottom