Naona wachangiaji hapo juu hawajanielewa vizuri. Sikusema ni elimu ipi kwani hiyo ndio michango inayotakikana hapa, Pia, huu uzi ni kutoa wazo tu watu tujadili ni vipi such an undertaking inaweza kufanyiwa kazi.
Kwa mchango wa polytechnic, ndio, level hii ya elimu haipo kabisa nchini, licha ya vyuo vya ualimu, hamna elimu mbadala kwa wananfunzi wa level baada ya sekondari. Ndio kuna VETA lakini bado idadi ya wanafunzi wanaohitaji elimu ya kati ni kubwa mno na VETA centres ni chache na labda courses zao hazitoshelezi mahitaji say, ujasiriamali. lakini pia tukumbuke, polytechnic sio catchment ya mbumbumbu... Unahitaji elimu ya awali pia uwe umepitia na kiwango cha kufaulu pia uwe nacho. Kwa hiyo idea kama hii inajaribu ku'pinpoint capital ambayo jumuiya inaweza kukusanya kwa investments kama hii. Tukifanikisha mradi kama huu, imagine spinoff effect inaweza kuwaunganisha watu zaidi kufanya shughuli zingine nyingi. Kwa nini nimesema capital in Billions of TSH? Kwa sababu, hapa JF watu wengi wameomba ideas kuendeleza/kuanzisha biashara in terms of millions, mijadala ya ufisadi tunaongelea sana, na humo tuna'debate investments ambazo zinawekezwa na wageni katika sectors nyingi nchini which are in terms of billions, na sote tunauliza, sisi wenyewe hatuwezi? Simu, TRL, Bia, Bandari nk
Education sector according to some figures on vijana.fm inaonyesha,
in 2010, Tanzania imetumia zaidi ya 2000 Billion, (2 Trillion) TSH katika sector hii, matokeo????
Nadhani swali la elimu ipi, ni kuangalia huo mchango wa capital incase hiyo idadi ya stakeholders 2500 inapatikana, je 12.5Billions, zinaweza kujenga a mix of education levels ngapi? 10 Primary, 5 Secondary, 1 University/Polytechnic ili kuwa na end to end education system.
LAT: Ndio Education ni wimbo kwangu lakini lengo ni hii chorus iwe inafahamika na wengi, labda album yake itaisaidia jamii..