Naomba msaada wa-kiushauri kwa mtaalam wa kutumia camera
1. Ni kamera ya megapixel ngapi inayoweza kuchukuwa picha yenye ubora kwa umbali wa mita 50?
2. Ni aina gani iliyo bora?
3. Ni bei gani na naweza kuipata wapi hapa tz?
Mchango wenu wandugu.
kaka mi si mtaalamu sana wa camera nina idea ndogo tu ya simu ila kwa sababu hujajibiwa tunaweza kushare mawazo.
1.unataka kuzoom umbali wa mita 50 au unataka camera iwe inacover eneo la mita 50?
kama ni kuzoom hapa itabidi uangalie lens. kitu cha karibu kinachonijia akilini ni telephoto lens itabidi iwe na lens kama hii
lakini weakness ya hii ni kwamba utaona kitu cha mbali ila utasacrifice details za pembeni.
kama ni kucover eneo la mita 50 kiupana itabidi uangalie focal length inakua in terms ya mm jinsi ikiwa ndogo ndio jinsi inavyocover eneo kubwa na kama ni lens ya fish eye basi itacover eneo hadi nyuzi 180 ina maana details zote za mbele utaziona. pia unatakiwa uangalie aperture inatakiwa iwe wide nayo.
2.kitu unachokitaka ni kikubwa na kampuni zenye uwezo wa kutengeneza vitu bora kama hivyo huwa hawababaishi ukipata kati ya kampuni hizi sio mbaya. nikon, canon, samsung, sony na panasonic wote sawa.
3. bei utaenda kutafuta mwenyewe madukani
kukupa tu guide hizi ni camera za 24mm ambazo zina wide angle utakazopiga picha kubwa za umbali huo.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.