Ambuje Akunnungu
Member
- Apr 12, 2019
- 19
- 16
Ndugu, ukipitia vizuri mtaala wa elimu ya sekondari, mapitio ya 2007, utagundua kuwa siku za masomo kwa mwanafunzi wa sekondari kwa mwaka ni 194. Ambapo siku hizo zimegawangwa katika mihula miwili ya masomo, ambapo ktk mihula hiyo kuna mapumziko ya mafupi ya likizo na weekend.
Ninachokifahamu ni kuwa walipanga siku hizo za masomo ambao ni taasisi ya elimu (TIE) walifanya utafiti wakaona zitatoa mapumziko ya kutosha ya akili ya mwanafunzi na kumpa muda mwalimu wa kujiandaa kwa kujisomea vitabu vya kutosha na kujiongezea uelewa kwa ujumla. Ndio maana wahadhiri vyuo vikuu hupewa kinachoitwa sabbatical leave ili wanoe bongo zao.
Kinachoonekana sasa kwenye halmashauri nyingi viongozi hawataki kuamini tafiti hizo za kitaalamu kabisa, ni rahisi kukuta walimu wakiambiwa hakuna kufunga shule kwa madarasa ya mitihani.
Hoja ni jee hizi siku kama zilivyopendekezwa na TIE zimepitwa na wakati? Walimu waendelee kufanya Kazi wakisubiri likizo zao za mwaka kama wafanyavyo wahasibu, manesi, n.k?
Je wanafunzi nao waendelee kupiga kazi bila kupumzika mwaka mzima??