Mtaaiba kura lakini wananchi wamechoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaaiba kura lakini wananchi wamechoka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kamundu, Nov 2, 2010.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Tukiacha vyama na ushabiki ukweli ni kwamba wananchi wamechoka na mabadiliko ni lazima yatatokea. Kwa mfano Mkapa alikuwa anatishia vyombo vya habari lakini sasa hakuna siri tena kwasababu huwezi kuwazuia watu wakati wote watapata njia tu. Kikwete na huko Zanzibar wataiba kura lakini kama hawataleta maendeleo itafikia wakati kuiba haitawezekana kwani Watanzania wanabadilika haraka kuliko serikali. Je ni kwanini sehemu kama Lushoto kule juu hakuna maji wala umeme na ni sehemu nzuri ya wageni kutembelea na Kilimanjaro kuna lami mpaka vijijini kuzidi hata dar?? na wabunge ni wapinzani?. Je ni kwanini shule za sekondari zinafelisha watoto Div 4 na ziro kila mwaka lakini serikali haizifungi?. Je ni kwanini utoe rushwa kutoa vitu vyako bandarini wakati ni wewe mwenyewe umefanyia kazi mtaji au umekopa kuleta vitu vyako, na usiko toa rushwa wanapeleka vitu storage na gharama zinapanda? je ni kwanini tunakatiwa umeme wakati tunatumia luku ambayo unalipia umeme kabla hata ya kuutumia? je ni kwanini Bush ametoa $600m ya barabara lakini hatuwezi ku control trafic ya dar-es-salaam ya magari laki mbili tu? je ni kwanini nchi ndogo kama Tanzania kila kiongozi anamisafara ya mabenzi wakati watoto hawana madawati wala magari ya kuendea shule?, je ni kwanini Watoto wa shule wanategemea tution wakati serikali ingeweza kuwatumia wanavyuo kufundisha kama ilivyokuwa JKT?, je ni kwanini viongozi wa serikali ambao hawana biashara wananunua viwanja kwa milioni mia tatu?, je ni kwanini watu wanahonga mamilioni kuwa wabunge?, je nikwanini sumenti inagharama kuliko kenya? je ni kwanini Tanzania inamatatizo ya mikataba mfano ni sababu gani inayoifanya serikali itoe $170 kwa kampuni ya uongo kuleta genereta za umeme wakati wangeweza kupata genereta kwa kampuni inayotengeneza hizo genereta?. Tatizo ni ubinafsi na msiko kuwa waangalifu mtaacha wajukuu zenu kwenye vita vya matabaka na nchi itakuwa somalia huko baadae. Hivyo kwa watanzania ni kubadilika na kuleta maendeleo au vita huko mbele, viongozi wazee mnaweza msiwepo lakini wajukuu zenu mtawaachia vita, hata Ivory cost kulikuwa na matajiri, zimbabwe kulikuwa na matajiri, zaire kulikuwa na matajiri, liberia kuliwa na matajiri, angola kulikuwa na matajiri? lakini kwenye vita vya jaamii watu wote wanakimbia. CCM ni lazima muelewe Watanzania wanabadilika mapema sana, na ni watu wanaojipenda sana lakini Mtanzania akiamua kupigana huwezi kumzuia. Kikwete kama unapenda nchi na tunajua utaiba kura urudi lakini badilika na badilisha nchi watanzania si wajinga kama CCM mnavyofikiria.
   
Loading...