Mswada wa sheria ya kuwabana watengeneza filamu (movies), wapelekwa Bungeni kwa hati ya dharura.

Fresh sana,2015 walipiga push up sana wakina JB,RICHIE,STEVE NYERERE etc.

Kwanza ningependekeza ipitishwe sheria kwa hati ya dharura hizo DVD/VCD za bongo movies makasha yao yasiwe na picha zozote zile yawe plain tu,ukiweka picha kwenye kasha linakua kosa la uhujumu uchumi(hakuna dhamana ni ndani tu).
Naunga mkono hoja yako.
 
Walianza watumishi wa Umma wakafuatia wafanyabiashara na baadae wakulima sasa ni wakati wa wasanii kuisoma tarakimu kwa uwazi na ukweli.
 
Hapo watakuja wale wazee wa "maadili ya kitanzania" watahariri maudhui yote ya filamu na kuifanya ionekane kama igizo la kilokole.

Kwa mujibu wa "maadili ya kitanzania", hata mwanamke kuvaa kipedo ni "jinai ya kimaadili". Anatozwa faini.

Akijikwatua na kimini chake uchwara, ni "uhalifu wa kimaadili". Anawajibishwa.

Najaribu kufikiri namna ambavyo series za hollywood zinavyotengenezwa, ingekuwa ni hapa Tanzania, nadhani tungejenga jela kubwa ambalo lingejaa watovu wa "maadili ya kitanzania".

Huwa nauliza, hayo "maadili ya kitanzania" yameandikwa kwenye msahafu gani nikausome!??? Maana anaweza kuibuka mwanasiasa mmoja mbabaishaji akaaminisha watu millioni hamsini kuwa mawazo yake ndio "maadili ya kitanzania".
Na wewe ndo wajinga walewale,wewe ulichoona Hollywood na kukifurahia unaamini hayo ndo maadili na sisi wote tuamini hivyo km unavyofikiri wewe. Hivi Bollywood nako si kunatengenezwa filamu!?? Ulishawaona wahindi wanavaa km wasanii wenu wa bongo movie!?? Tatizo mnapenda kujifungia ndani ya box. Kule Nigeria kuna kabila linaitwa HAUSA ulishaona movie zao!?? Wanaigiza sana movie na tamthilia za mapenzi lkn kwa nidhamu ya hali ya juu sana. Hata matamshi tu ya lugha ni kitu muhimu sana. Kumbuka hizo movie zinaangaliwa na rika zote,wewe unaona sahihi tu yanayofanyika na bongo movie hata ukiwa unatizama na wanao!?? Bunge wamefanya kitu muhimu sana.
 
Kama ulichosema ni kweli basi muswada huu ni wa kudidimiza maendeleo ya tasnia ya filamu na riwaya. Kama ni uhakiki, ni bora ufanyike tu kwenye ile product ya mwisho inayotakiwa kwenda sokoni, siyo kumchokonoa kuku na utumbo wake ukitegema kweli baadaye utakubali nyama yake iliwe.
Shida yenu huwa hamfatilii mambo... maana haya yanayosemwa kwenye muswada mbona yanafanyika kila leo? hakuna msanii anatoa movie bila kupeleka kwanza kuhaririwa na kupitiwa na bodi ya filamu....kwa taarifa tuu na wanalipia...
Nafikiri muswada una zaidi ya haya....... lakini kama ni hili wala sio jipya
 
Kwa mujibu wa mswada wa sheria unaopelekwa Bungeni tarehe 27/6, (MSWAADA WA SHERIA NAMBA 3 WA 2019), kama utapitishwa kuwa sheria, watengenezaji au wazalishaji wa movies wanatakiwa kupeleka picha zote walizopiga kabla ya kuhariri katika bodi ya filam.

Bodi itatakiwa kupitia picha hizo ghafi, na kisha kupitia pia filam ilivyohaririwa ndipo itatoa kibali cha filam hiyo kwenda public.

Atakaye kiuka utaratibu huo au kuficha taarifa hizo atalipishwa faini ya hadi 5% ya gharama za kutengeneza filam hiyo.

Mswaada huu unapelekwa Bungeni chini hati ya dharura.
Safi sana 2015 walijifanya makada kwelikweli ngoja wanyoooke hao masanii sie tupo na movies za nje hili halituhusu linawahusu ccm
 
Bongo movie iko hoi halafu wanaleta sheria ambazo zitaiua kabisa,Ilitakiwa waje na incentives kubwa ili industry iamke kama enzi za marehem kanumba
 
wewe ulichoona Hollywood na kukifurahia unaamini hayo ndo maadili na sisi wote tuamini hivyo km unavyofikiri wewe. Hivi Bollywood nako si kunatengenezwa filamu!?? Ulishawaona wahindi wanavaa km wasanii wenu wa bongo movie!?? Tatizo mnapenda kujifungia ndani ya box. Kule Nigeria kuna kabila linaitwa HAUSA ulishaona movie zao!?? Wanaigiza sana movie na tamthilia za mapenzi lkn kwa nidhamu ya hali ya juu sana. Hata matamshi tu ya lugha ni kitu muhimu sana. Kumbuka hizo movie zinaangaliwa na rika zote,wewe unaona sahihi tu yanayofanyika na bongo movie hata ukiwa unatizama na wanao!?? Bunge wamefanya kitu muhimu sana.
Nonsense, crap, rubbish, trash, spatatura, TAKATAKA!
 
Ni kama ndugu Mwigulu alivyotaka Bungeni eti tai yake iwe vazi la Taifa?
Hahaha. Hicho nacho ni kioja cha aina yake!

Wameshindwa kujadili "issues" za kulikwamua taifa toka tope zito la umasikini badala yake wamegeuka kwenye mabendera sare sare! Very small issues! Na ni waziri.

Si ajabu alisisitiza kuwa kuvaa tai ya bendera ni "maadili ya kitanzania" , na akataka kila mtu aamini hilo!
 
Atakaye kiuka utaratibu huo au kuficha taarifa hizo atalipishwa faini ya hadi 5% ya gharama za kutengeneza filam hiyo.
Kwani wangesema kwa kila filamu itakayotengenezwa itozwe kodi ya 5% ya gharama za utengenezaji kungekuwa na ubaya gani? (Jokes)
===
Utaratibu huu unaowekwa na sheria unaweza kuwa na nia njema lakini kama mpango wa makusudi hautawekwa kwa ajili ya kuepusha ucheleweshaji wa matokeo ya ukaguzi kuna hatari kubwa ya kuzamisha sekta ya filamu nchi. Tukumbuke utengenezaji na utoaji filamu ni project na inatabia zote za kuitwa mradi ikiwemo ya muda uliopangwa kwa ajili ya kutengeneza na kutoa kwa umma filamu husika.
 
Shida yenu huwa hamfatilii mambo... maana haya yanayosemwa kwenye muswada mbona yanafanyika kila leo? hakuna msanii anatoa movie bila kupeleka kwanza kuhaririwa na kupitiwa na bodi ya filamu....kwa taarifa tuu na wanalipia...
Nafikiri muswada una zaidi ya haya....... lakini kama ni hili wala sio jipya
Ungenimabia mimi shida yangu siyo kugeneralize kuwa shida yetu;halafu nadhani wewe hukuuelewa muswada huo. Kwa kawaid script ya movie huwa inahakikiwa kabla shooting haijaanza, na lile toleo la kwanza la movie pia linahakikiwa kabla ya kuingiza movie sokoni.

Katika kuandaa movie, kila scene kwenye script huwa inashutiwa mara kadhaa kutoa clips nyingi sana kabla ya kuanza kuziunganisha kwenye storyline. Mhariri wa movie atachagua ni clips zipi za kutumia katika kila scene kuziacha zile ambazo hazikutoka vizuri. Sasa muswada huu unataka clips zote zipitiwe hata zila ambazo mtayarishaji hazitumii kiwenye movie yenyewe. Ni upuuzi!! Kumwambia mtayarishaji apeleke clips zote za katikaiti na undue burden kwa mtayarishaji, kwani wakati mwinginine huwa wanazifuta clips hizo huko huko kwenye location ili kurudia shooting inapoonekana kuwa hazikutoka vizuri; lakini muswada utawazuia kufanya hivyo sasa.
 
Kwa mujibu wa mswada wa sheria unaopelekwa Bungeni tarehe 27/6, (MSWAADA WA SHERIA NAMBA 3 WA 2019), kama utapitishwa kuwa sheria, watengenezaji au wazalishaji wa movies wanatakiwa kupeleka picha zote walizopiga kabla ya kuhariri katika bodi ya filam.

Bodi itatakiwa kupitia picha hizo ghafi, na kisha kupitia pia filam ilivyohaririwa ndipo itatoa kibali cha filam hiyo kwenda public.

Atakaye kiuka utaratibu huo au kuficha taarifa hizo atalipishwa faini ya hadi 5% ya gharama za kutengeneza filam hiyo.

Mswaada huu unapelekwa Bungeni chini hati ya dharura.
Dikteta kazini , Lissu alishasema kwamba mkinyamaza mtakiona , nadhani sasa tunaelewana
 
Safi sana --

Back
Top Bottom