Msuya amshukia Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msuya amshukia Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Apr 6, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  KADA wa (CCM) David Msuya Mkazi wa Kibaha mkoani Pwani amemshukia Katibu Mkuu wa CCM Yusufu Makamba akidai ameshindwa kukiongozi chama hicho na kumtaka ajiuzulu.

  MwanaCCM huyo amesema Makamba ndiye chanzo cha kuibuka kwa migogoro na malumbano ndani ya chama hicho.

  Msuya pia amewataka vigogo wa CCM, Umoja wa vijana (UV-CCM) na wanachama wote kuacha kulumbana kwenye vyombo vya habari akisema kufanya hivyo ni kukiua chama.

  Kauli ya Musuya imekuja huku chama hicho kikiwa kwenye mvutano kati ya baadhi ya vigogo wa CCM na UV-CCM.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Msuya alisema kitendo cha katibu mkuu kuacha malumbano hayo yaendelee ni hatari kwa chama na ni ishara tosha kuwa ameshindwa kazi yake, hivyo anasitahili kujiuzulu.

  “Hebu tutazame wakati wa uongozi wa Benjamin Mkapa na katibu wake Phillip Mangula chama kilikuwaje, Katibu Mkuu aliwajibika na hivyo alionyesha kuimudu nafasi yake ndio maana hata chama hakikuyumba ”alisema Msuya.

  “Katibu wetu wa sasa ndio chanzo cha malumbano yanashika kasi ndani ya chama kwa sasa, yeye amekaa kimya, baada ya kutokea malumbano ilimpasa kuwaita wote wanaolumbana nje ya utaratibu kwenye kamati ya maadili na kuwaonya”alisema Msuya.

  Msuya alisema kitendo cha kuacha malumbano hayo kuendelea ni hatari kwa chama sababu kunaweza kutoa mwanya hata kwa baadhi ya wanachama kukihama na watu waliotaka kujiunga kuendelea kukikimbia.

  Alisema kwa sasa CCM pamoja na jumuiya zake si wakati w a kuendeleza malumbano na badala yake ni wakati wa kufikiri wapi walikiuka hata kusababisha kupoteza majimbo mengi kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

  Alisema kwa sasa viongozi walipaswa kukaa chini kupitia na kutafiti wapi walikotoka na wanakokwenda wakiweka malengo zaidi kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Katika hatua nyingine Msuya aliwataka makatibu wa chama hicho ngazi zote kuandaa na mikutano ya hadhara kuwezesha wananchi kukutana na viongozi ili kujadili chama chao.
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2011
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  mm nilidhani Msuya yule aliekuwa WAziri mkuu, kumbe huyu kidagaa, kama alivyomuita Dr slaaa yule ambaye sasa Mbunge wa NCCR, ah nimekumbuka yeye alimuiata sisimizi
   
Loading...