Msuva, Gaucho yawakuta 'mazito' Morocco, waonya

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,988
1,175
KLABU ya Waydad Casablanca ya Morocco imepewa siku 45 kukamilisha malipo ya Dola za Marekani 700,000 (sawa na Sh. bilioni 1.6) kwa aliyekuwa mchezaji wao, Simon Msuva baada ya nyota huyo kushinda kesi aliyofungua dhidi ya klabu hiyo.

Akizuñgumza jijini Dar es Salaam jana, Yasmin Razack, msimamizi wa mchezaji huyo alisema kiasi hicho kinatakiwa kulipwa mara moja na tangu hukumu hiyo itolewe, Wydad inaruhusiwa kukata rufani ndani ya siku 10.

Yasmin alisema Msuva amepitia wakati ngumu alipokuwa Morocco kwa kuwa hakuwa na usimamizi mzuri na kudai mchezaji anapofika nchini humo huwa ananyang’anywa hati ya kusafiria ili asipate msaada wowote ule.

Alisema Msuva alinyimwa haki zake mbalimbali huku akipewa makaratasi mengi ya kusaini ambayo yalikuwa yameandikwa lugha ya Kifaransa ambayo hakuifahamu lakini akilazimishwa kusaini haraka.

Aliwataka wachezaji wasikubali kusaini mkataba wowote bila kuwa na wanasheria binafsi ambaye atamtafuta kwa ajili ya kumsaidia hapo baadaye na kuongeza mateso aliyoyapitia Msuva yamekuwa fundisho.

Alisema mpaka Msuva amefanikiwa kushinda kesi yake amepata tabu hivyo Watanzania wanapaswa kufahamu Waarabu hawana utu.

Msuva alisema ameshukuru kushinda kesi hiyo na amewataka wachezaji wenzake kupata wasimamizi wazuri pindi wanapokuwa wanasaini mikataba na timu yoyote.

"Kwa mateso niliyoyapitia angekuwa mtu mwingine nisingeweza kuitumikia Timu ya Taifa lakini ninashukuru TFF pamoja na makocha wangu walikuwa wananishauri nitulize akili hatimaye nimefanikiwa na sitaki kulipwa pesa nusu nusu," alisema Msuva.

Aliongeza hali ilikuwa mbaya zaidi pale Rais wa klabu hiyo iliyomsajili kukata mawasiliano naye na kukataa kuonana naye hata pale alipomfuata nyumbani kwake.

"Kilichonikuta walinipa makaratasi mengi ya kusaini ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha ya Kifaransa, nilisaini sikujua kile ambacho kitanikuta, sitaki kuwasikia Waarabu, nimeteseka mno," Msuva alisema.
Aliishukuru serikali pamoja na Watanzania kwa sapoti waliyompa kipindi chote alichokuwa kwenye matatizo hayo.

Wakati huo huo, Yasmin alisema mchezaji mwingine wa Tanzania, Mwanahamisi Omary 'Gaucho' naye ameamua kurejea nyumbani kufuatia klabu yake ya Shabab Atlas ya Morroco kutomtendea haki.

Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Tunzo, ambaye anamsimamia Gaucho alisema nyota huyo wa zamani wa Simba Queens ameisamehe klabu hiyo pesa zote anazozidai na hataki kurejea Morocco kuitumikia.

"Mwanahamisi amesema licha ya mateso aliyoyapitia amesamehe kila kitu, ameamua kurudi nyumbani, hataki kuendelea tena na Waarabu," Yasmin alisema

Source: Nipashe
 
Msuva ni popoma,utasaini vipi makaratasi yameandikwa kiarabu sijui kifaransa bila kujua maana yake.
Mbona hata nyinyi ni mapopoma tu! Mkiulizwa bilioni 20 ziko wapi, mnaishia tu kutoa mapovu! Leo hii mnaingia mkataba na M-Bet halafu t-shirt za wachezaji zimetolewa nembo ya sportpesa, na kuandikwa juu M-Bet!

Mkataba ni kiasi gani, na utadumu kwa miaka mingapi! Hamjui! Yaani Mo na Barbara wanawageuza tu kama chapati!
 
Simba sio mali yangu
 
Nyani mpuuzi katika ubora wako,unabweka tu kama umbwa
Mbona hata nyinyi ni mapopoma tu! Mkiulizwa bilioni 20 ziko wapi, mnaishia tu kutoa mapovu! Leo hii mnaingia mkataba na M-Bet halafu t-shirt za wachezaji zimetolewa nembo ya sportpesa, na kuandikwa juu M-Bet!

Mkataba ni kiasi gani, na utadumu kwa miaka mingapi! Hamjui! Yaani Mo na Barbara wanawageuza tu kama chapati!
 
Mbona hata nyinyi ni mapopoma tu! Mkiulizwa bilioni 20 ziko wapi, mnaishia tu kutoa mapovu! Leo hii mnaingia mkataba na M-Bet halafu t-shirt za wachezaji zimetolewa nembo ya sportpesa, na kuandikwa juu M-Bet!

Mkataba ni kiasi gani, na utadumu kwa miaka mingapi! Hamjui! Yaani Mo na Barbara wanawageuza tu kama chapati!
Ungesema 'sisi' ni mapopoma ningekuelewa maana uto iliyowahi kukodishwa na Manji na iliyopo hivi sasa utofauti wake na unaowazomea ni nini?
 
Hii ni habari ya upande mmoja..

Wabongo tatizo elimu ndogo, mtu anasaini mkataba bila kutumia mwanasheria halafu analalamika umeandikwa kwa kifaransa, sasa ulitaka wakuandikie kwa kiswahili wakati ndio official language ya nchi ya Morocco?

Wewe Msuva ulitakiwa kutumia Agent kwenye kunegotiate benefits zako hapo Wydad. Matokeo yake kifaransa hujui ila ukaenda wewe mwenyewe, makaratasi ya kusaini umepewa huelewi kitu.

Mbona wacongo wengi wanacheza Morocco hatujasikia huo upuuzi unaosema?

Kipaji bila elimu ni bure kabisa. Uache kuchafua Waarabu kwa ujinga wako mwenyewe, idiot.

Wabongo elimu muhimu kwenye kila kitu la sivyo mtalizwa sana kwa ujinga wenu. Leo nimesoma thread humu kuna dada wa miaka 23 "kaliza" watu wazima ambao hata kuagiza bidhaa China hawawezi wanataka waagiziwe, yaani ni ujinga ujinga tu hii nchi..
 
Msuva kabla ya kucheza Waydad alicheza Difaa ljadid miaka yote hiyo hakujifunza lugha na pia hakujifunza kuwa na wanasheria wanaopitia mikataba yake?
 
Mbona hata nyinyi ni mapopoma tu! Mkiulizwa bilioni 20 ziko wapi, mnaishia tu kutoa mapovu! Leo hii mnaingia mkataba na M-Bet halafu t-shirt za wachezaji zimetolewa nembo ya sportpesa, na kuandikwa juu M-Bet!

Mkataba ni kiasi gani, na utadumu kwa miaka mingapi! Hamjui! Yaani Mo na Barbara wanawageuza tu kama chapati!
Eti nawee uko Mtumba, Dodoma mji wa Serikali.
Wallah kazi ipo hapa.
 
Hii ni habari ya upande mmoja..
Wabongo tatizo elimu ndogo, mtu anasaini mkataba bila kutumia mwanasheria halafu analalamika umeandikwa kwa kifaransa, sasa ulitaka wakuandikie kwa kiswahili wakati ndio official language ya nchi ya Morocco
Umemalizaaaaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom