RAYAN THE DON
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 679
- 1,220
Habari za mchana wakubwa kwa wadogo. Ni matumaini yangu kwamba hamjambo wote humu ndani na manaendelea vyema katika utafutaji wa ridhiki.
Wakuu bila kupoteza muda naombeni ushauri katika hili jambo kwa sababu najiona kabisa kupotea katika uso wa Dunia.
Wakuu kama nitakuwa nakosea mtanirekebisha kwani humu kuna wazazi, kaka, dada na wadogo zangu ambao kwa namna moja au nyingine mlishawahi kuyapitia haya ninayoyapitia kwa sasa.
Ni kwamba tangu mwaka 2011 mpaka 2015 nilikuwa nasoma chuo fulani hapa mjini Dar es salaam. Baada ya kumaliza chuo sikuona umhimu wa kurudi nyumbani kwani niliona tayari nimekuwa mtu mzima hivyo ni bora niendelee na maisha ya utafutaji hapa mjini.
Katika mahangaiko yangu Mungu alisaidia nikafungua duka la vipodozi 2016, nikaanzisha uwakala wa M- PESA, TIGO PESA, CRDB & NMB na biashara ya kukopesha watu kwa riba. Kiukweli maisha yalikuwa mazuri sana. Pia kwa wakati nilifanikiwa kununua viwanja 3 mkoani Dar es salaam na shamba moja na kujenga nyumba huku Kigamboni.
Hata wazazi wangu waliponitembelea walifurahi sana kuona kijana wao nimepiga hatua hiyo. Pia nilikuwa nawatunza vizuri sana. Ila baadae mambo yalienda kombo ambapo ni mwanzoni mwa 2019.
Mambo yalivyoenda kombo sikuwahi kuwaambia kwani sikutaka wajue hali iliyonipata na maisha niliyopitia tangu nilipoanguka katika maisha ya utafutaji.
Sasa wakuu kuna rafiki yangu ambaye tunatoka sehemu moja na tulisoma nae mpaka High School ndipo tukatengana kwa sababu tulipata nafasi katika vyuo tofauti.
Huyu rafiki yangu inaonekana kwa sasa maisha yanamuendea vizuri kwani amejenga sana na amenunua gari moja.
Kila wazazi wangu wanapokutana na huyu jamaa unakuta wananipigia simu na kunilaumu sana kuwa ni kwanini siendi kujenga nyumbani ili nipate hata nyumba ya kufikia.
Kadhalika, huongea maneno ya ajabu ajabu sana kuwa nimeacha kuwatunza na hawajui kama nitawatunza tena siku wakizeeka. Kibaya zaidi huwa wananilinganisha na jamaa kuwa mnalingana ila yeye amefanya mambo makubwa huku ila wewe hatuoni unachokifanya.unakuta wanahoji kwamba huko Dar es salaam bado sijapata pesa yaani wanaona kama bado nacheza.
Wakuu kumbuka kwamba wao hawajui maisha ninayoyapitia tena ili niweze kusimama kama nilivyokuwa mwanzoni. Kwa sababu ukiwa umefika hatua fulani na ukaanguka huwa inauma sana na inachukua muda kidogo kurudi kama mwanzoni.
Kitu ambacho kinaniumiza sana ni pale ambapo wananipigia simu kunieleza mafanikio ya rafiki yangu, kunilaumu sana, kunidharau kwa namna moja au nyingine.
Hili jambo limekuwa likiniumiza sana wakuu. Mpaka linanipa msongo wa mawazo kwani nimeishahudhuria hospitalini kama mara tano na kuambiwa kuwa siumwi chichote ila nina msongo wa mawazo.
Kutokana na hali hiyo ya dharau, masimango, uringanisho usio na tija nimeamua nisiwasiliane nao kabisa katika maisha yangu kwani najiona kabisa kuendelea kuwasiliana nao hali yangu itazidi kuwa mbaya sana. Nimeamua kufanya hivyo ili nizidi kulinda afya ya akili yangu(mental health) na amani ya moyo wangu(peace of mind) kwani kuna wakati huwa nawaza vibaya ila nikikumbuka kwamba maisha yatakaa vizuri muda wowote unakuta naghairisha uamuzi wowote mbaya.
Kutokana na hayo nimesajiri namba mpya ili nisipatikane kwa namna moja au nyingine kwani nimechoka sana kusikia maneno yao ambayo hayana msaada katika kunijenga bali kuniumiza moyo wangu.
Pia jambo la kunilazimisha kwenda kujenga nyumbani kwake(kwetu) naona halipo sawa kwani pale ni nyumbani kwake na siyo kwangu. Nasema hivyo kwa sababu mimi ni mwanaume nami nahitaji kuwa na kwangu na siyo kujenga kwake. Je kwa uamuzi huu nakosea wakuu?
Karibuni kwa michango yenu wakuu.