Msukuma: Kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
RC+Makonda.jpg

Waziri wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi ameikosoa kampeni iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuwasaidia wanawake wenye watoto waliotelekezwa na waume zao na kusema kwamba ilipaswa kufanyika kwa faragha.

Kabudi ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga kuhoji uhalali wa kampeni hiyo.

Profesa Kabudi amesema shughuli hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika kwa faragha si kama inavyofanyika sasa.

Wakati Kabudi akisema hayo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha.


Chanzo: Mwananchi

 
Muwe mnaongelea public mambo hayo na sio kwenye hizo kamati.

Kabudi akiwasilisha bajeti yake ya wizara inatakiwa agusie jambo hilo na hali kadhalika mawaziri wengine.

Ila mtukufu yuko kimya wala halisemei jambo hili au ile kauli ya ZZK kuwa nchi inaongozwa na Washamba na Malimbukeni inapata legitimacy...????
 
Sio tu faragha bali imebagua waathirika wa kutelekezewa na kubambikiziwa watoto.
Kwani wapo wanawake wamewatelekeza watoto kwa ndugu, jamaa, marafiki, waume zao na wazazi wao kwa kisingizio cha kwenda kutafuta mijini.
Lakini pia wapo wanawake waliozaa watoto nje ya ndoa na kuwaaminisha waume zao kuwa ni watoto wao.
Hata hivyo kuna wanaume ambao wamediliki kuwadhulumu watoto wake zao na kuwaficha kwa wazazi wao bila ya mke kupata ruhusa ya kuwaona.
Vivyo hivyo kwa wadada wa kazi za majumbani kutelekezewa watoto/mimba kwa staili ile ile ya kutokuvuruga familia either kwa vijana wa kiume ndani ya nyumba, ndugu wa familia au baba.
Alichokifanya Mh. Makonda ni kama indicator ya Kubadili tabia na kuboresha pale alipoishia.
Binafsi nampongeza kwa jitihada zake za kutetea wananchi wake.
 
:eek: eek!

Just get back and check you moves. Namba saba anakaba, beki inajishambulia na midfieder sijui ni centre-half anazozana na kipa. Refa sijui yuko wapi, Kocha naye yu juu ya mzambarau anameza zambarau hata hazijaiva vizuri mazima mazima. Mengine kaweka mfukoni mashabiki wanasubiri ashuke, bahati mbaya akipaliwa sijui itakuwaje... Uwanja wa shule jamani mbigiri kibao na tunapenda mpira.
 
Huyu Baba alie telekezwa na mke wake pamoja na watoto, alimliliaonda kwa upendeleo kwa akina mama pekee
 

Attachments

  • VID-20180418-WA0012.mp4
    2 MB · Views: 56
Hivi punde
Haya CCM mseme ninyi sasa kuhusu Naibu Rais wenu. Wapinzani wameshamaliza. Ju.ha. anabaki ju.ha. hata ukimvisha suti. Fa fa fa form four ni ya kweli.
 
Aisee nimepita pale mida ya tisa nilitaka kulia kwa kuwaona wamama walivyojazana na watoto hasa vile vilio vya watoto. Hata kama ni kujitafutia umaarufu kwa gharama ya wengine kwa hili hapana aisee lazima mtu achume laana ya wale watoto
 
Back
Top Bottom