msuba wavutwa mbele ya Kituo cha Polisi Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msuba wavutwa mbele ya Kituo cha Polisi Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 7, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  UVUTAJI wa bangi na madawa mengine yanayodaiwa kuwa ni ya kulevya, ni vitu vya kawaida katika viwanja vya Mwembe Yanga, tena karibu kabisa na kituo cha Polisi kilichoko katika viwanja hivyo.
  Hali hiyo imewafanya wananchi wanaoishi karibu na viwanja hivyo na wale wanaopita katika eneo hilo kupaza sauti na kuwalaumu waziwazi viongozi wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke.

  “Hivi hawa polisi wanafurahishwa na harufu hii ya bangi katika eneo hili? Tena kibaya zaidi ni kwamba hawa wote wanaovuta ni vibaka”, amelalamika mmoja wa wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo, Zacharia Mwandiko.

  Mwananchi huyo amesema kuwa inashangaza kuona kuwa pamoja na kwamba viwanja hivyo hutumika katika shughuli mbalimbali za kitaifa, na kuwepo kwa kituo cha polisi katika viwanja hivyo, lakini uvutaji wa bangi umekithiri katika viwanja hivyo kuanzia mchana hadi usiku.

  Mkazi mwingine ambaye hakupenda kutaja jina lake amesema kuwa licha ya uvutaji wa bangi na madawa mengine ya kulevya eneo hilo pia ni makutano ya vitendo vya uhalifu, na kushangaa kuona kwanini polisi wanapita na kuwaona watu hao bila kuwahoji na ikibidi kuwachukulia hatua.

  Amesema kuwa harufu hiyo ya bangi sio tu inawakera watu wanaoishi karibu na eneo hilo, bali hata wapita njia kwasababu imekuwa ikivutwa kwa wingi na makundi ya vijana mbalimbali.

  “Sisi wakazi wa Temeke tunawajua wavuta bangi hawa, lakini hatuwezi kuwachukulia hatua. Hiyo ni kazi ya polisi ambao wanatakiwa kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria. Sasa kama wanawatazama na kufurahishwa na hii harufu ya bangi unaweza kuona ni namna gani jeshi letu linavyoyumba katika kufanya maamuzi yanayosaidia wananchi”, amesema mwananchi huyo.

  Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Temeke, David Misime hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, ingawa uchunguzi umebaini kuwepo kwa tatizo hilo kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo.


  5581562.jpg
   
 2. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mwananyamala kwa Kopa bange linapigwa nje ya kituo,polisi na raia wanakula kwa pamoja hiyo kitu. Bangi connecting people
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,348
  Likes Received: 1,143
  Trophy Points: 280
  after that mnadanganywa kuwa Tz no nchi huru yenye demokrasia ya kweli.
  Kiranja vipi huko, umenusurika kwenye kamata kamata ya kusaka wauaji wa Tegeta?
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  tegeta imekuwaje tena nimecheki kwa michuzi mbona pamechafuka sana kuna nn huko?
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Apr 8, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kuna mauaji yaliyotokea jana!
   
 6. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #6
  Apr 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  watu wangapi wamefariki?aisee duh
   
Loading...