Katika safari zangu nikitumia usafiri wa umma nimechukua wasaa kuongea mawili matatu na madereva na pia wahudumu katika magari haya.
Kilicho wazi ni kuwa watumishi hawa wenye kubeba roho zetu safarini wanakabiliwa na msongo mkubwa wa mawazo hasa kuhusiana na faini tokea katika makosa bambikizi lukuki tokea kwa askari wa usalama barabarani.
Si waendesha mabasi makubwa si waendesha mabasi madogo, barabarani kumekuwa hakufai kuwa ndipo sehemu ya kufanyia kazi. Barabarani Dar zakusanywa hadi bilioni 2 kwa wiki Moja peke yake.
Yanayosemekana ni makosa, ni discretion tu ya polisi mmoja mmoja katika maelfu ya waliopo barabarani kwa dereva anayetoka Dar hadi Mwanza anaopaswa kukabiliana nao. Kwa utaratibu uliopo sasa hivi, dereva hana pa kukata rufaa. Kwa kila shitaka, anachopaswa kufanya ni kulipa tu. Jamani, utaratibu gani huu usiokuwa na nafasi ya rufaa?
Si kwa madereva wa mabasi tu hali ni hivyo hivyo hata kwa wale wa magari ya mizigo na hata magari ya watu binafsi.
Baadhi ya watu hasa waendesha magari mapya kwenda nchi jirani wamelazimika kusafiri usiku kukwepa adha bambikizi za askari hawa. Hii ni bila kujali kabisa risks zote za usiku.
Baadhi yetu tumelazimika kuyaacha magari yetu majumbani si kwa kupenda bali adha za hawa jamaa tunaosikia wamepewa malengo ya idadi ya makosa kwa askari kwa siku.
Faini za kufikia 200,000/= kwa dereva kwa siku zinamwacha vipi dereva na amani ya roho kufanya kazi yake kwa ufanisi?
Je inafahamika kuwa faini hizi zina athari gani ya Moja kwa Moja kwenye mishahara yao wanayopata kwa mwezi? Je ni nani baina yetu anayepata mshahara kwa mwezi kwa mwezi anaweza kushangilia kwa kupunguziwa mshahara bila ya utaratibu na kila leo na hata kwa 5,000/= tu?
Barabara zenyewe ni tatizo kubwa tu kwani ni mbovu mno, polisi kama mbwa mwitu wameweka hadi viti vya kukalia kusubiria magari ili kuyatoza faini.
Utaratibu huu ni mbovu sana unaua morali ya kazi, kuleta msongo wa mawazo na matokeo yake ni kuweka maisha yetu rehani katika hizi ajali za kila leo.
Shirikisheni wadau wakiwamo wana saikolojia. Chanzo cha ajali kwa kiwango kikubwa tu ni hizi faini ambazo aghalabu hasara zake ni kubwa mno labda kuliko hata faida mnayodhania kupatikana.