Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,348
Kama kasi ya kuporomoka kwa Muziki wa Bendi (Rumba na Dansi) itaendelea katika awamu ijayo (awamu ya 5) hakuna shaka kwamba Bendi kongwe (Msondo Ngoma na Sikinde) zaweza kutoweka, kufutika na kusahaulika kabisa!
Bendi hizi ambazo umaarufu wake unakaribia ama kuwa sawa na umaarufu wa klabu kongwe za mpira wa miguu nchini-Simba na Yanga, zimeshindwa kusimama, kujizatiti na kujiendesha kibiashara! Kwa miaka nenda-rudi zimeendelea kubaki vilevile, mtindo (rhythm) uleule, uimbaji uleule, nyimbo zilezile, waimbaji walewale na mashabiki walewale!
Ni wakati mwafaka sasa kwa bendi hizi ambazo kusema ukweli ndizo 'nembo na alama' ya muziki wetu wa dansi na rumba nchini kuijitathmini na kujizatiti. Ziwekeze katika menejimenti na utafiti, ziwekeze katika vipaji vichanga, tungo mpya na mirindimo mipya itakayoendana na mabadiliko ya nyakati tulizomo hivi sasa.
Zinapaswa kuzaliwa upya.
Kutoka kwa Sampu Mussa Sampu