Msomi my foot, if not just another fisadi in the making. Jamani msomi gani tena huyu, what lecturer can stoop so low - strike me pink, yaani udiwani kwa tiketi ya.... just look at him, yeah take a good good look !
Hivi kwa nini sisi tunapenda kulirusha rusha sana hili neno "msomi"
Utakuta kuna wengine wanajiita eti "learned" brother au sister (hasa waliosomea sheria). Mimi hili neno "msomi" halinipendezi hata kidogo. Limekaa kimajigambo majigambo. Eti "msomi"....yaani tunapenda visifa vya kijinga jinga tu visivyo na mbele wala nyuma.
Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali - kuna ma PhD. holders kibao lakini hata siku moja huwezi kusikia wakijitambulisha kwa kutumia academic qualifications zao. Kwa mfano Newt Gingrich...jamaa ana Ph.D. lakini kama hujui historia yake huwezi hata kujua kama anayo.
Haya, huyo Gordon Brown hata siku moja sijawahi kuona akitumia Dr.Gordon Brown.....lakini sisi lazima tuweke hizo herufi mbele ya majina yetu. Lazima watu wajue kuwa una u-dokta au ujinga ujinga mwingine. Tuko wa ajabu sana sisi.
Eti "learned" brother or sister...what fak is that?
Hupendi kulinganisha lakini unalinganisha! Kwani kila kitu lazima tuwaige Waamerika/Wazungu et al? Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari....
Sipendi kujilinganisha sana na Marekani lakini ukiangalia congress ya Marekani, chemba zote mbili za House na Senate, zimejaa watu waliobobea ktk fani mbalimbali
Hupendi kulinganisha lakini unalinganisha! Kwani kila kitu lazima tuwaige Waamerika/Wazungu et al? Mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari.
Naamini mimi ni msomi. Kwa kufahamu hilo nimekumbuka njia rahisi ambayo Msomi kama mimi hutumia kuwasiliana na wasomi wenzangu ni kupitia machapisho (publications).
Ajabu nimeiona baada ya kutafuta jina la Ally Zawadi ktk google. Jina hili linapatikana kwenye facebook tu!
Huuu ndo usomi?
Hii ni ngumu saana kusubstantiate km wao wanataka kujiita au wanaitwa!!!Mkuu Nyani thank you because hata mimi kitu hicho kina niboa sana. Halafu sasa una kuta "wasomi" wetu wengi wana degree feki.. Tunapenda sifa mno. Siku hizi hata wenye honorary degrees kama Karume wna taka kuitwa "dokta" wakati neyrere aliyekuwa na degree kibao za heshima hata siku moja haku kubali kutambulishwa hivyo. I think ni mchanganyiko wa sifa na watu kujua kwamba wakijitambulisha hivyo wata weza kujikweza zaidi kwa wapiga kura.
Aisee.... Hawa wasomi wa kwenye.... sijui mjengwa blog... michuzi blog... etc si walewale 'wasomi' wetu?! Watu kama hawa hata ukikamata watano watano kila siku na kunyonga hawataisha! Wasitutibue nyongo....
Siku hizi hata mainjinia wameamka yakhe.. Mtu hakubali kuitwa jina bila ya kutanguliza title ya 'injinia' so and so. Na akistaafu anataka aitwe 'injinia mstaafu' kama mmoja niliyesoma amechukuwa fomu ya ubunge leo.
Ninakuongezea na senkisi ya mdomo na kiii bodiMsiwasahau akina Dk. Manyaunyau, Prof. Vulata, Dr. Remmy Ongala......yaani shaghalabhagala tu.