Msisikitike, kuna njia ingine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msisikitike, kuna njia ingine

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by uporoto01, Nov 18, 2011.

 1. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Miaka kadhaa iliyopita Kibaki alitaka kufanya hichi anachokifanya sasa Jakaya ya kuandika katiba anayoitaka yeye sasa baadae kutakiwa kuwa na kura ya maoni kuikubali au kukataa njia hii.Wapenda mageuzi wa kweli wakajipanga na kupita nchi nzima kuipinga na kuwashawishi watu waikatae kwa kupiga 'NO' walijulikana kama orange,na upande wa Kibaki wa 'YES' ulijulikana kama ndizi.
  Upande wa 'NO' au Orange ulishinda na hivyo kumlazimisha Kibaki kutumia njia ya kuwashirikisha Wakenya wote katika kuandika na kupitisha Katiba hii nzuri waliyoipata sasa.
  Kwahiyo ni kujipanga tu wakati wa kura ya maoni kuhamasisha wananchi kuikataa Katiba hii,inawezekana kila mmoja akishiriki kikamilifu.
   
 2. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi binafsi kwa maoni yangu naona njia hii ni sahihi zaidi kuliko maandamano ambayo hayana athari ya moja kwa moja kubadili maamuzi haya. Tujipange kuikataa kwenye kura ya maoni na hata ukiongea na watu wengi hawajaafiki uburuzwaji uliotokea.Vote 'NO' to The State House Constitution.
   
 3. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo hamsemi kweli,mnadanganya watu sijui kwa faida ya nani? kenya walikataa katiba siyo mswada wa maandalizi ya katiba.chadema wanakataa mswada wa ,maandalizi ya katiba na kwa hakili zenu ndogo mnadhani nyinyi ndo wananchi wanawapenda kuliko ccm na cuf? kama tunapima uwakilishi ndo wingin wa watu wanaopenda chama,chadema wamepata wapi takwimu kwamba wao ndo wanapendwa kuliko ccm wenye RAIS NA WABUNGE WENGI?,njoni mikoan chadema mpoteze muda kama IGUNGA,LAKINI MJUE KATIBA ITAANDIKWA NA WATANZANIA WATAIKUBALI.
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wewe ndio muongo Kenya walikataa mchakato wa Kibaki katiba ilikuwa bado.
   
 5. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu uporoto kuna kitu nataka ujue,tukikosea step tukakubali kura ipigwe tumekwisha lazima watashinda,hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindanna na ccm tunapoongea mambo ya kura,ni wazoefu wa kuchakachua,hilo siafiki hata kidogo
   
 6. King2

  King2 JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watanzania waoga !
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Nov 18, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu hata mimi hilo kidogo linanipa wasiwasi wasimamizi si watakuwa hawa NEC ya Kivuyo ?
   
 8. d

  demolisher Member

  #8
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni ndoto ya mchana kwa tume hii ya uchaguzi itakayosimamia zoezi hilo.
   
 9. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #9
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Tatizo muda Mkuu,mpaka wakati wa kura tkifika muda utakua umeenda sana,the only solution ni MAANDAMANO tu.Kwani ktk hayo maandamano tutaibua vitu vingine vingi na ikiwezekana through hayohayo maandamano tuung'oe utawala wa kidhalimu wa CCM
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Tukirogwa tukakubali mchakato uendelee, mjue tumekwaa kisiki yawezekana hamkusikiliza hitimisho la Bi.Celena mchumba wangu.Amesema hivi: kura ya maoni itapigwa na wananchi waliojiandikisha ktk daftari la wapiga kura.Sote tunajua jinsi daftari lile lilivyo mtaji wa CCM, pili wa-magamba ni mabingwa wa kuchakachua hapo ndiyo itakuwa mwisho wa mchezo.

  Nini kifanyike: watanzania tukubali hasara ya baadhi yetu kufa kwa ajili ya wengi, tuingie barabarani tupigwe risasi baadhi yetu tufe na baadhi wajeruhiwa ili watakaobaki waje wale matunda.Kwa mfano mimi nina watoto wawili nikifa watakuja kula bata watoto wangu au mnasemaje??.
  Kinachotakiwa tulianzishe bila kuchelewa.
  Leo tunaongelea Rwanda inafanya vizuri tunajua vizuri walikotoka??? tuulizeni sisi wana-lake zone tuliwahi kula samaki waliokula miili ya wanyarwanda, lakini leo hii Rwanda wanakula bata, tunawashuhudia akina ALPHA wa TUSKER PROJECT wakitesa lakini baba zoa walikumbana na cha moto.Wajerumani leo wanauchumi imara lakini ukisimuliwa historia yao huwezi amini. TULIANZISHE ILI TUMUENZI LEMA
   
 11. Adolph

  Adolph JF-Expert Member

  #11
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 26, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Acha kabisa hiyo mambo..ccm wana phd ya uchakachuaji...yan kwenye kura ndo tutachakachuliwa vibaya mno..
   
 12. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #12
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Tena tusithubutu kuruhusu mchakato uendelee.Bora tubaki na katiba ya zamani watakuja kubadili watoto wetu.Kama tutashiriki kutengeneza katiba kupitia mswaada huu, wajukuu zetu watatushangaa tulisomaje!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. majata

  majata JF-Expert Member

  #13
  Nov 18, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 385
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Tunaikataa serikali dhalimu ya jk na makinda, tunataka baraza la mpito litakalo tuongoza kupata katiba ya wananchi, hii ya jk, makinda na ccm hatuitaki.
   
 14. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #14
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ni wazo zuri, lakini hiyo YES na NO itafanya kazi vizuri mahali ambapo mna tume huru inayosimamia huo upigaji kura. Lakini huo mswada unaipa madaraka tume tuliyo nayo ya uchaguzi (ya kikwete) jukumu la kuisimamia hiyo kura. Unategemea nini hapo?
   
 15. kalukamise

  kalukamise JF-Expert Member

  #15
  Nov 18, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 688
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Linapokuwa suala la katiba, mkuu hakuna u ccm / CDM /NCCR. Unaweza kuta ndani ya ccm half wako against na hiyo rasimu, ukiwatoa mavampire yanayonyonya damu zetu
   
 16. mbogo31

  mbogo31 JF-Expert Member

  #16
  Nov 18, 2011
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 687
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Nimetembea nchi yote hii, yaani ccm haipendwi na walio wengi, ila sema kinachowakomboa ccm ni wizi wa kura na uelewa mdogo wa baadhi ya watanzania wenzetu, ila kwa sasa vijijini wanaelimika kwa kasi kuliko hapa mjini.
   
 17. n

  nyantella JF-Expert Member

  #17
  Nov 18, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Sasa baada ya hapo iweje? Katiba inahitaji kabla ya 2015 voting no will send us into a dead end! suggest a better way forward rather than this Vote No thing.

   
 18. M

  Makomu Member

  #18
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kufanya hivyo ni kuruhusu kupoteza fedha zetu za kodi kwa kazi isiyo na maana. hapa hapa mpaka kieleweke!!!!!
   
 19. babad

  babad Member

  #19
  Nov 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 95
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acheni mambo ya ajabu nyie,eti tukatae wakati wa kupiga kura ina maana tukubali kuburuzwa wakati wa mchakato kwa kuundiwa tume yenye washkaji wa CCM,bunge la katiba lenye washkaji na hadidu za rejea za mtu mmoja?kama tulivyosema tukikubali sasa hivi tutaburuzwa na hata kuikataa baadaye tutashindwa.Acheni uoga nyie msidhani maandamano ndo vita kwani vita vinaweza kutokea bila hata maandamano
   
 20. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #20
  Nov 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mchakato huu hauna tofauti na mbuni aliyeficha kichwa chake shimoni hali mwili wote uko nje. Bunge limetumika kupitisha uozo mwingi sana wa serikali ya CCM, matokeo yake tunayajua. Hatujakoma tunazidi kufanya madudu yaleyale, na matokeo yatakuwa yaleyale. Mchakato mbovu, utazaa kamati mbovu, itakayokusanya maoni na kurudisha ripoti mbovu, itapelekwa kwenye bunge la katiba bovu, lenye idadi kubwa ya wawakilishi walioanzisha mchakato mbovu, watapitisha rasimu ya katiba mbovu, kwenda kupigiwa kura ya maoni itakayosimamiwa na tume mbovu. KATIBA ITAKUWA MBOVU
   
Loading...