Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,842
- 50,556
Kuna jambo linakera sana humu JF. Kuna watu kila wakati wao ni kusema tu Lissu ni msaliti, lakini ukiwauliza usaliti wa Lissu ni nini hawana la kujibu zaidi ya kusema anashirikiana na wazungu kutuhujumu. Na ukiwauliza anashirikiana nao vipi wanakaa kimya kama wamepigwa shoti ya umeme.
Kama nyie watu mnaomuona Lissu ni msaliti hamna ushahidi ama hoja ya kuthibitisha hata kwa mazingira tu kwamba Lissu ni msaliti kaeni kimya. Kama mnadhani uzalendo ni kuunga mkono kila jambo linalofanywa na serikali basi nyie hamjui maana ya Uzalendo.
Wengine wanasema kwamba Lissu anavujisha siri kwa wazungu, ujinga mtupu. Yaani mkataba uko serikalini na kwa wawekezaji, sasa hapo nani wana siri kati ya Lissu na Serikali pamoja na wawekezaji wao?
Lissu kila siku anapigania mikataba iwekwe wazi kwa wabunge serikali inakataaa, leo mnasema kwamba Lissu anavujisha siri kwa wawekezaji wa kizungu, ni siri gani hizo alizo nazo Lissu ambazo Serikali na wawekezaji hawana?