Msiotahiriwa Kagera jiandaeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiotahiriwa Kagera jiandaeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 21, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WANAUME wa kisiwa cha Goziba wilayani Muleba mkoani Kagera ambao hawajatahiriwa wametakiwa kujiandaa kushiriki uzinduzi wa tohara kwa wanaume Januari 22.

  Taarifa iliyotolewa jana na Ubalozi wa Marekani nchini, ilisema uzinduzi huo ni wa aina yake na utafanywa katika maeneo ya vijijini na watu wanaotarajiwa kuhudumiwa ni zaidi ya 3,500 katika miezi kadhaa ijayo.

  Tohara hiyo na huduma mbalimbali zinazohusu virusi vya Ukimwi zitatolewa bure visiwani humo ambako mahema yatasimikwa kutoka Serikali ya Marekani.

  Kampeni hiyo inakwenda pamoja na kanuni za msingi, kwamba tohara kwa wanaume ni sehemu ya kinga dhidi ya maambukizi ya Ukimwi na ilishathibitishwa katika maeneo ambako kuna maambukizi makubwa ya ugonjwa huo na idadi ya waliotahiriwa iko chini.

  Visiwa hivyo vilivyoko ndani ya Ziwa Victoria, vinatambulika kwa kuwa na kiwango cha juu cha vitendo vya ngono kutokana na asili ya biashara ifanyikayo hapo ya uvuvi wa samaki ambayo inamlazimu mvuvi kusafiri huku na huko.

  Hali hiyo inaendana na kiwango cha juu cha maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 20 huku idadi ya wasiotahiriwa ikiwa ni asilimia 30.

  Mpango wa tohara kwa wanaume kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi unafadhiliwa na Mpango wa Dharura wa Rais kwa ajili ya Kupambana na Ukimwi (Pepfar) kupitia Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) na kupitia pia Mipango ya Tiba, Huduma kwa Wagonjwa wa Ukimwi ya Kituo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Columbia (ICAP).

  Mpango huo unaendeshwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika Hospitali ya Mkoa ya Kagera na Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya.

  Mwaka jana, wanaume 1,158 walitahiriwa kisiwani Bumbile na zaidi ya 3,000 katika hospitali hizo mbili wakiwakilisha asilimia 50 ya lengo la ICAP Tanzania kwa mwaka 2010-2011.

  Marekani itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania katika kuimarisha afya ya Taifa na kukidhi matarajio ya Rais Jakaya Kikwete ya “Tanzania Bila Ukimwi, Inawezekana’.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,280
  Likes Received: 19,431
  Trophy Points: 280
  alienda marekani kuomba wazungu waje wakawatahiri watanzani nini? ukishangaa ya moses utayaona ya .....!! buta nakubaliana naye kweye hili jambo
   
 3. C

  Chan Senior Member

  #3
  Jan 21, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hahah kwa JK hilo linawezekana kabisa.. hao wanaoenda Tz kutahiri watu wao pia wana mikono ya sweta manake wazungu wengi kama sio wote hiyo siyo issue yao kivile...
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hv kabla ukimwi haujaingia wanaume walikua wanatahiriwa ili kukwepa nini?na wanawake pia
   
 5. Jaluo_Nyeupe

  Jaluo_Nyeupe JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 2,269
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  bila shaka kampeni hiyo haitaendelea kwenye maeneo mengine kanda ya ziwa eeeh?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,280
  Likes Received: 19,431
  Trophy Points: 280
  hivi kumbe unaweza kuchakachua bila mipira kwa vile umetahiriwa usiupate hata kama yeye anao? na posibility hapa sio 0.00000000000000000001?? hebu madokta tusaidiane jamani kwa sababu limtu likishatahiriwa linaweza kuingia chaka na kuanza kupiga n"gadu kwa n'gadu:banplease: si kabembelezwa kutahiriwa ili kupunguza possibility ya maambukizi?
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,280
  Likes Received: 19,431
  Trophy Points: 280
  usukumani:banplease:
   
 8. K

  Kisaa kyafo Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nendeni mkatairiwe uko mnatukalia mikono ya sweta apa!mlishindwa kujitairi sasa tutawatairi kinguvu,unatairiwa chini ya ulinzi wa mwema,teh teh teh
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wakimaliza tohara ya wanaume waanze ya wanawake!
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Jan 21, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Kampeni ingeanzia mkoa wa Mbeya.
  Hope mnaelewa what i mean
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  bado hatujakuelewa kwann mbeya!
   
Loading...