...msione aibu tutangazieni hali ya hatari tu.........................!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

...msione aibu tutangazieni hali ya hatari tu.........................!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by only83, Jun 26, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...........WanaJF wenzangu kwanza awali ya yote napenda kuwapa pole kwa matatizo haya ya umeme yanayoendelea kwa kasi...mgao huu wa umeme unaweza ukawa unaenda kufanana na ule mgao wa umeme wa 2006..Ni hali ya kuhuzunisha sana ktk hali hii hakuna kiongozi mkubwa wa kitaifa halieye kubali kutoa tamko la wazi kuhusu hii hali tata..Na cha kushangaza wanawarushia mzigo TANESCO waseme..Juzi siku ya ijumaa Clouds Fm kupitia kipindi chao cha JAHAZI walifanikiwa kumpata injinia mmoja wa TANESCO kuzungumzia hilo baada ya kupata taarifa kuwa BADRA MASOUD msemaji wa TANESCO yuko nje ya nchi kikazi..kwakweli waliofanikiwa kumsikia halisema wazi kama ifuatavyo...
  1. Tuache siasa tatizo la umeme ni kubwa sana na akasema hitaji la Taifa ni megawatt zaidi ya 800 na kwasasa mashine zetu zinazalisha megawatt 500 tu..kwahiyo tunaupungufu wa megawatt 300 na zaidi..
  2. Na akasema kwa uwazi kabisa...mgao wa umeme utadumu kwa nusu mwaka wote kwa wastani wa masaa 10 mpaka 24..hii inamaana kuwa kuna siku tunaweza kosa umeme kwa siku nzima.....
  My concern is;kwanini hali hii itokee wakati matatizo tunayafahamu? Na kinachoniumiza ni kuwa viongozi wetu wakubwa kama Waziri mwenye dhamana ya umeme na Rais hawatoi tamko lolote kutokana na hali hii...Watanzania tutaendelea kuwa wapole kwa hawa watu mpaka lini?
  Inakera na inaumiza...mimi jana nimekosa umeme tangu saa 1 usiku mpaka saa 7 usiku....itakuwaje?
   
 2. Ziada Mwana

  Ziada Mwana JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itakuwa kama jusi, joto ya jiwe kwisa jua.
   
 3. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sikuelewi!!!!
   
 4. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Alipata kunene haya:
  "Tutahakikisha kuwa nchi haiwi gizani na kwamba umeme wa ziada unaotakiwa utapatikana na shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma zinaendelea kama kawaida."
  J.Kikwete-2009


  Tamko alilotoa ni hilo! Tusubiri akirudi (au kesharudi?) labda atatoa jingine.
   
 5. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Umenichekesha saaaaaaaaaanaaa! upweke wa weekend umeisha!
   
 6. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Wewe saa moja mpaka saa saba sie huku kwetu siku tatu mfululizo,hali ni mbaya na ni aibu kwa taifa
   
 7. m

  mambomengi JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 829
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kuna watu walitakiwa wawe jela toka miaka kenda ilopita. Ni vema tukawaiga wachina wanavyofanya. Vinginevyo tuache kulalama. Tukaekizani na umeme ukirudi uendelee kuunguza vifaa vya electroniki.
   
 8. RUMANYIKA

  RUMANYIKA JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Magamba ahsante sana kwa hali hii na kondoo wa kitz acha wataabike. Watu wamekua kama mbuzi hiyo ndo gharama ya kofia,khanga na scarf.
   
 9. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Watz wenzangu,sjui hawa viongozi wanawachukuliaje na kuwafikiria wananchi,hivi wo wanafikiri kuwa watu wote wanaishi kama wanavyo ishi wao na watoto wao,hakika isingekuwa kuogopa mods kwa ajili ya 'ban' ningewapa live.Miaka 50 baada ya uhuru,hatuna umeme wa kueleweka,nchi masikini,watu wankufa kw ajili ya huduma mbaya ya afya,elimu duni,walimu hamna,wakati wachache wananufaika na kushibisha mitumbo yao,tunaelekea wapi jamani,watu hawataki kubana matumizi sanasana ndo wameongeza matumizi ya kodi ya wavuja jasho!Ee Mungu sikiliza basi kilio cha watanzania
   
 10. only83

  only83 JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kuna jambo tunatakiwa tufanye.......huu ni uhuni kabisa......
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  waone aibu wapi wanajua hatuwezi kuwafanya chochote nakuambia sisi umeme unakuja hatuoni unaondoka hatuoni mtu anarudisha umeme saa tano anauchulua saa kumi na mbili kila siku haya si matusi siku zao zinahesabika
   
 12. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa China kweli viongozi wote wangekuwa wameshac.....Inabidi tuwaondolee uvivu hawa.
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  amesema TANZANIA itauza umeme nje na itakua gas seller duniani
   
 14. Ghost

  Ghost JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2011
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  anatafuta wawekezaji....cjui mwekezaji gani atawekeza kwenye nchi hii na hili giza....
   
Loading...